Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • it kur. 34-36
  • Yeriko

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Yeriko
  • Ufahamu wa Kina wa Maandiko
  • Habari Zinazolingana
  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2015
  • Pigano la Yeriko—Ni Hadithi Tu au Ni Uhakika?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
  • Kutotii Maonyo ya Mungu Kunaleta Msiba
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1978
  • Jinsi Lilivyo Tukufu Jina la Yehova!
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
Pata Habari Zaidi
Ufahamu wa Kina wa Maandiko
it kur. 34-36

YERIKO

(Yeriko) [huenda, Jiji la Mwezi].

Jiji la kwanza la Kanaani lililoshindwa na Waisraeli, lililokuwa upande wa Magharibi mwa Yordani. (Hes 22:1; Yos 6:1, 24, 25) Linahusianishwa na jiji la Tell es-Sultan (Tel Yeriho) ambalo liko kilomita 22 Mash. Kask. Mash. mwa Yerusalemu. Karibu na jiji hilo kuna jiji la Tulul Abu el-ʽAlayiq na inawaziwa kwamba Yeriko la karne ya kwanza lilikuwa hapo. Yeriko lina hali ya hewa yenye joto na mvua na liko mita 250 (futi 820) chini ya usawa wa bahari katika Bonde la Yordani. Leo, kilimo cha machungwa, ndizi, na tini kinafanywa katika eneo hilo na kama ilivyokuwa zamani, mitende bado inanawiri katika eneo hilo.

Ushindi wa Kwanza wa Waisraeli. Mwishoni mwa miaka 40 ya kutangatanga nyikani, Waisraeli walifika kwenye Nyanda za Moabu. Wakiwa huko, Musa alipanda kwenye Mlima Nebo na kutazama Nchi ya Ahadi, kutia ndani Yeriko, “jiji la mitende,” na eneo lake tambarare.​—Hes 36:13; Kum 32:49; 34:1-3.

Baada ya Musa kufa, Yoshua aliwatuma wapelelezi wawili katika jiji la Yeriko. Walifichwa na Rahabu, hivyo hawakuonekana na baadaye walitoroka kupitia kamba iliyoshushwa kupitia dirisha la nyumba ya Rahabu, ambayo ilishikamana na ukuta wa Yeriko. Wanaume hao walijificha kwenye eneo lenye milima lililokuwa karibu kwa siku tatu, na baadaye wakavuka mto Yordani na kurudi kwenye kambi ya Waisraeli.​—Yos 2:1-23.

Lazima iwe kwamba mfalme wa Yeriko na wakazi wake waliingiwa na woga mwingi kwa sababu ya kusikia au kushuhudia maji mengi ya mto Yordani yakijikusanya kimuujiza, jambo lililowawezesha Waisraeli kuvuka kupitia nchi kavu. Baadaye, ingawa wanaume Waisraeli walitahiriwa na walilazimika kusubiri hadi wapone ili waweze kujilinda, hakuna mtu aliyethubutu kuwashambulia huku Gilgali. Bila usumbufu wowote, Waisraeli walifanikiwa pia kuadhimisha Pasaka wakiwa kwenye jangwa tambarare la Yeriko.​—Yos 5:1-10.

Baadaye, wakiwa karibu na Yeriko, mkuu wa jeshi la malaika alimtokea Yoshua na kumweleza utaratibu watakaofuata ili kuliteka jiji, ambalo kufikia wakati huo malango yake yalikuwa yamefungwa kabisa kwa sababu ya Waisraeli. Kwa utii, wanajeshi Waisraeli walilizunguka jiji hilo mara moja kila siku kwa siku sita, wakifuatwa na makuhani saba walioendelea kupiga pembe mfululizo, na nyuma yao kulikuwa na makuhani waliobeba sanduku la agano, na nyuma yao, walinzi wa nyuma​—wote walilizunguka jiji la Yeriko. Lakini katika siku ya saba walilizunguka jiji mara saba. Walipolizunguka mara ya mwisho na pembe zikapigwa, watu walipiga kelele kubwa za vita, na kuta za jiji hilo zikaanza kuanguka chini.​—Yos 5:13–6:20.

Kisha Waisraeli wakaingia moja kwa moja Yeriko, na kuua kila mtu na wanyama wote wa kufugwa. Lakini kwa sababu ya fadhili ambazo Rahabu aliwaonyesha wapelelezi kwa kuwaficha, yeye na watu wa familia yake hawakuuawa, walikuwa salama ndani ya nyumba yake iliyokuwa kwenye sehemu fulani ya ukuta ambayo haikuanguka. Jiji lote liliteketezwa, lakini dhahabu na fedha ziliwekwa katika hazina ya nyumba ya Yehova. (Yos 6:20-25) Hata hivyo, Mwisraeli mmoja, Akani, aliiba kipande cha dhahabu, kiasi fulani cha fedha, na vazi rasmi maridadi na kuvificha chini ya hema lake. Kwa sababu hiyo, yeye pamoja na familia yake waliuawa.​—Yos 7:20-26.

Marejeo ya Baadaye Katika Historia. Baadaye, jiji la Yeriko lililoharibiwa lilikuja kuwa sehemu ya eneo la Benjamini lililopakana na Efraimu na Manase. (Yos 16:1, 7; 18:12, 21) Inaonekana muda mfupi baadaye, watu walianza kuishi katika eneo hilo. Lilitekwa na Mfalme Egloni wa Moabu, na lilibaki chini ya utawala wake kwa miaka 18. (Amu 3:12-30) Wakati wa utawala wa Mfalme Daudi watu waliendelea kukaa eneo la Yeriko. (2Sa 10:5; 1Nya 19:5) Lakini halikujengwa tena hadi Hieli kutoka Betheli alipolijenga wakati wa utawala wa Ahabu. Kisha laana iliyotolewa na Yoshua zaidi ya miaka 500 hivi mapema ikatimia, Abiramu, mzaliwa wa kwanza wa Hieli alikufa alipojenga msingi na Segubu mwana wake wa mwisho alikufa alipoweka malango yake.​—Yos 6:26; 1Fa 16:34.

Katika kipindi hichohicho baadhi “wana wa manabii” waliishi Yeriko. (2Fa 2:4, 5) Baada ya Yehova kumchukua nabii Eliya katika dhoruba ya upepo, Elisha alibaki Yeriko kwa muda fulani na akaponya maji ya jiji hilo. (2Fa 2:11-15, 19-22) Maji ya ʽAin es-Sultan (kwa wenyeji kinajulikana kama kisima kilichoponywa na Elisha) yamefafanuliwa kuwa maji mazuri na matamu nayo hunywesha mashamba ya Yeriko ya leo.

Wakati wa Mfalme Ahazi mtawala mwovu wa Yuda, Yehova aliruhusu majeshi ya Israeli yakiongozwa na Mfalme Peka yashambulie Yuda lililokuwa limeasi, na kuua watu 120,000 na kuwachukua mateka watu 200,000. Lakini Odedi, nabii wa Yehova alikutana na washindi hao na kuwaonya wasiwafanye mateka hao kuwa watumwa. Kwa sababu hiyo, baada ya kupewa mavazi na chakula, mateka hao walipelekwa Yeriko na kuachiliwa huru.​—2Nya 28:6-15.

Baada ya kuharibiwa kwa Yerusalemu mwaka wa 607 K.W.K., Mfalme Sedekia alikimbia kuelekea Yeriko lakini Wababiloni walimfikia na kumkamata kwenye jangwa tambarare la Yeriko. (2Fa 25:5; Yer 39:5; 52:8) Baada ya kuwekwa huru kutoka uhamishoni Babiloni, ‘wana 345 wa Yeriko’ walikuwa miongoni mwa wale waliorudi pamoja na Zerubabeli katika mwaka wa 537 K.W.K. na inaonekana waliishi Yeriko. (Ezr 2:1, 2, 34; Ne 7:36) Baadaye, baadhi ya wanaume wa Yeriko walisaidia katika ujenzi wa ukuta wa Yerusalemu.​—Ne 3:2.

Kuelekea mwishoni mwa mwaka wa 32 na mwanzoni mwa mwaka wa 33 W.K., Yeriko lilikuwa miongoni mwa majiji ambayo Yesu alihubiri. Karibu na jiji hilo Yesu Kristo alimponya kipofu Bartimayo na mwenzake. (Mk 10:46; Mt 20:29; Lu 18:35; ona BARTIMAYO.) Katika jiji la Yeriko, Yesu alikutana na Zakayo na baadaye akawa mgeni nyumbani mwake. (Lu 19:1-7) Awali huko Yudea, alipokuwa akitoa mfano wa Msamaria mwema, Yesu alirejelea barabara iliyotoka Yerusalemu kwenda Yeriko. (Lu 10:30) Kulingana na uthibitisho wa kale wa kihistoria, barabara hiyo ilikuwa na wezi wengi.

Je, wachimbuzi wa vitu vya kale wamepata uthibitisho kwamba Yeriko liliharibiwa katika siku za Yoshua?

Profesa John Garstang, kiongozi wa uchunguzi wa Waingereza katika eneo la Tell es-Sultan kati ya mwaka wa 1929 na 1936, alivumbua kile ambacho anasema kilikuwa moja ya majiji yaliyokuwa yameteketezwa kwa moto na kuta zake zilikuwa zimeanguka. Alihusianisha jiji hilo na Yeriko la wakati wa Yoshua na kusema kwamba liliharibiwa mwaka 1400 K.W.K. hivi. Ingawa leo baadhi ya wasomi bado wanaunga mkono maneno ya Garstang, wengine wanatafsiri uthibitisho huo kwa njia tofauti. Mwanaakiolojia G. Ernest Wright anaandika hivi: “Kuta mbili zilizozunguka kilele cha jiji hilo la kale ambalo Garstang . . . anaamini ziliharibiwa na tetemeko la ardhi na moto wakati wa Yoshua, ziligunduliwa kuwa za miaka ya 3000 K.W.K na zinawakilisha kuta mbili tu kati ya kuta 14 tofauti-tofauti au visehemu vya kuta zilizojengwa wakati wa kipindi hicho.” (Biblical Archaeology, 1962, uku. 79, 80) Watu wengi wanahisi uchimbuzi wa mapema katika eneo hilo uliondoa chochote ambacho huenda kilinusurika kutoka katika uharibifu huo, hivyo hakuna, au ni mabaki machache sana yaliyosalia ya Yeriko la siku za Yoshua. Kama Profesa Jack Finegan anavyosema: “Hivyo, kwa sasa hakuna uthibitisho wowote katika eneo hilo unaoweza kutusaidia kutambua Yoshua alishinda Yeriko wakati gani.”​—Light From the Ancient Past, 1959, uku. 159.

Kwa sababu hiyo wasomi wengi wanajaribu kujua wakati ambapo Yeriko lilianguka kwa kutegemea uthibitisho uliopo, na wanapendekeza tarehe mbalimbali ndani ya kipindi cha miaka 200 hivi. Kwa sababu ya ukosefu huo wa uhakika, Profesa Merrill F. Unger anasema hivi: “Wasomi wanapaswa kuwa waangalifu sana wanapohusianisha makadirio ya kipindi cha wakati kinachotajwa na wachimbuzi na kueleweka kwa habari hizo. Kwa msingi wa maoni yanayotofautiana kutoka kwenye vyanzo vyenye kutegemeka, ni wazi kwamba tarehe za tukio na mikataa hususa inayofikiwa kutokana na uvumbuzi wa wachimbuzi mara nyingi hutegemea jambo fulani hususa.”​—Archaeology and the Old Testament, 1964, uku. 164.

Hivyo, ingawa maoni ya wachimbuzi hayapatani na mfuatano wa matukio wa Biblia unaoonyesha mwaka 1473 K.W.K. kuwa mwaka ambao Yeriko liliharibiwa, hiyo si sababu ya kutuhangaisha. Tofauti kati ya maoni ya Garstang na wachimbuzi wengine kuhusu Yeriko inaonyesha umuhimu wa kuwa waangalifu tunapokubali ushahidi wa wachimbuzi iwe wanaunga mkono au la, masimulizi ya Biblia na mfuatano wake wa matukio.

[Picha katika ukurasa wa 35]

Kuchimbuliwa kwa kuta za Yeriko la kaleYERIKO

Kuchimbuliwa kwa kuta za Yeriko la kale

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki