Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w15 11/15 uku. 13
  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2015
  • Habari Zinazolingana
  • Pigano la Yeriko—Ni Hadithi Tu au Ni Uhakika?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
  • Yeriko
    Ufahamu wa Kina wa Maandiko
  • “Agano la Kale” Ni Lenye Kusadikika Kadiri Gani?
    Biblia—Neno la Mungu au la Binadamu?
  • Kutotii Maonyo ya Mungu Kunaleta Msiba
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1978
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2015
w15 11/15 uku. 13
Makuhani wakipuliza pembe, Yoshua akipiga kelele za vita, na ukuta wa Yeriko ukianguka

MASWALI KUTOKA KWA WASOMAJI

Ni nini kinachothibitisha kwamba Waisraeli walishinda jiji la kale la Yeriko baada ya kulizingira kwa muda mfupi?

Kulingana na kitabu cha Yoshua 6:10-15, 20, majeshi ya Israeli yalizunguka jiji la Yeriko mara moja kila siku kwa muda wa siku sita. Siku ya saba, walizunguka jiji hilo mara saba, na Mungu akasababisha kuta imara za Yeriko zianguke. Jambo hilo liliwawezesha Waisraeli kuingia Yeriko na kulishinda jiji hilo. Je, kuna jambo lolote linalothibitisha kwamba jiji la Yeriko lilizingirwa kwa muda mfupi kama Biblia inavyosema?

Zamani, ilikuwa kawaida kwa wavamizi kuzingira jiji lenye ngome. Haidhuru kuzingirwa huko kungedumu kwa muda gani, wavamizi wangepora mali za jiji na vyakula. Hata hivyo, katika jiji la Yeriko, wachimbuaji wa vitu vya kale wamekuta chakula kingi kilichokuwa kimehifadhiwa. Kitabu kimoja kinasema hivi kuhusu jambo hilo: “Mbali na vyombo vya udongo, nafaka ndiyo iliyopatikana kwa wingi sana katika magofu. . . . Hicho ni kisa cha pekee katika historia ya vitu vya kale ya Palestina. Huenda mtungi mmoja au miwili tu ya nafaka vingeweza kupatikana, lakini kupata kiasi kikubwa hivyo cha nafaka ni jambo lisilo la kawaida.”—Biblical Archaeology Review.

Biblia inaeleza sababu iliyowafanya Waisraeli wasipore nafaka za Yeriko. Yehova aliwaamuru wasifanye hivyo. (Yos. 6:17, 18) Waisraeli walishambulia katika majira ya kuchipua, mara tu baada ya mavuno, wakati ambapo nafaka ilipatikana kwa wingi. (Yos. 3:15-17; 5:10) Hivyo basi, kupatikana kwa masalio ya nafaka nyingi katika jiji la Yeriko kunathibitisha kwamba Waisraeli walilizingira jiji hilo kwa muda mfupi, kama Biblia inavyoeleza.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki