Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w90 7/15 uku. 7
  • Pigano la Yeriko—Ni Hadithi Tu au Ni Uhakika?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Pigano la Yeriko—Ni Hadithi Tu au Ni Uhakika?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
  • Habari Zinazolingana
  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2015
  • Yeriko
    Ufahamu wa Kina wa Maandiko
  • “Agano la Kale” Ni Lenye Kusadikika Kadiri Gani?
    Biblia—Neno la Mungu au la Binadamu?
  • Kutotii Maonyo ya Mungu Kunaleta Msiba
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1978
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
w90 7/15 uku. 7

Pigano la Yeriko—Ni Hadithi Tu au Ni Uhakika?

KWA miongo kadhaa, wanaakiolojia wamejaribu kutilia shaka usimulizi wa Biblia wa Yoshua na pigano la Yeriko. Kulingana na Biblia, Yoshua na jeshi la Israeli walipiga miguu kuzunguka Yeriko kwa siku saba, mpaka Mungu akaziangusha kuta madhubuti sana za jiji hilo. Hiyo iliwaruhusu Waisraeli kuingia na ‘kuchoma jiji kwa moto na kila kitu kilichomo ndani yalo.’—Yoshua 6:1-24, NW.

Lakini wanaakiolojia wengi, kwa kuongozwa na kichapo cha Kathleen Kenyon chenye kuheshimiwa sana katika miaka ya 1950, walisadiki kwamba Yeriko hata halikuwako wakati wa ule uvamizi wa Waisraeli. Naam, walishikilia kwamba jiji hilo lilikuwa limeharibiwa zaidi ya karne moja mapema! Hivyo, usimulizi wa Kibiblia wa Yoshua na Waisraeli ulipuuzwa mahali pengi. Ingawa hivyo, hivi majuzi Dakt. Bryant G. Wood, mwanaakiolojia wa kutoka Chuo Kikuu cha Toronto, Kanada, ameutazama upya uthibitisho wa kutoka Yeriko. Kulingana na The New York Times, yeye amekata shauri kwamba Dakt. Kenyon “alikuwa amekuwa akitafuta vigae vya vyungu vya aina isiyofaa, tena katika mahali pasipofaa,” na kwamba kwa kweli uthibitisho huo ‘unaafikiana kwa njia nzuri ajabu’ na Biblia.

Dakt. Wood hutaja tabaka la majivu meta 1 kwa maki (unene) yaliyojaa vigae vya vyungu, vijipande vya matufali kutoka ukuta ulioanguka, na miti, vyote vikiwa vyeusi kana kwamba vimegeuzwa rangi na moto ulioenea jijini. Vijipande hivyo vya vyungu vya usanii vimepewa tarehe (kwa njia zipatikanazo ambazo zakiriwa kuwa si kamili) kuwa vya mwaka 1410 kabla ya Wakati wa Kawaida wetu, kwa kuruhusu uwezekano wa kwamba ni vya miaka 40 kabla au baada ya hapo—hiyo ikiwa si mbali hata kidogo na 1473 K.W.K., ile tarehe ya pigano la Yeriko yenye kupatikana kutokana na Biblia.

Wachimbuzi wamepata kwamba nyumba zilizokuwa katika Yeriko la kale zilikuwa na akiba nyingi za nafaka. Hilo linapendeza, kwa kuwa Biblia huonyesha kwamba Yeriko lilianguka muda mfupi baada ya mavuno ya masika na bila mazingira yenye kurefushwa ili kufisha watu njaa. (Yoshua 3:14-16) Hizo zote mbili ni sababu nzuri kwa nini nyumba za Yeriko zingekuwa zina akiba ya nafaka ya kutosha wakati jiji hilo lilipoharibiwa.

Wanasayansi ni kama wana nongwa ya kutotaka kuukubali usahihi wa Biblia. Hivyo, Times hunukuu mwanachuo mmoja mwenye sifa kuwa akisema hivi kwa kujibu maoni ya uchimbuzi wa Wood: “Hakuna shaka kwamba kadiri kubwa ya habari zipatikanazo katika Biblia zina chembe ya ukweli ndani yazo.” Hata hivyo, kadiri masimulizi zaidi na zaidi ya Kimaandiko yaungwavyo mkono na magunduo ya kisayansi na ya kiakiolojia, ni wazi kwa wasio na maoni ya kuegemea upande mmoja kwamba hata kidogo Biblia si mkusanyo wa mambo mabandia ambayo pindi kwa pindi yametiliwa-tiliwa chembe za ukweli. Kama vile Biblia yenyewe isemavyo: “Mungu aonekane kuwa amini na kila mtu mwongo.”—Warumi 3:4.

Ingawa fasiri za sasa za machimbuo ya kiakiolojia huko Yeriko yapendeza kuangaliwa, Wakristo wa kweli ‘huenenda kwa imani, si kwa kuona.’ (2 Wakorintho 5:7) Imani yao haitegemei akiolojia. Kukiwako au kukiwa hakuna uthibitisho wa kiakiolojia, Biblia hurudia-rudia kuthibitika kuwa chanzo chenye kutegemeka cha habari zinazohusu wakati uliopita, wakati uliopo, na wakati ujao.—Zaburi 119:105; 2 Petro 1:19-21.

[Picha katika ukurasa wa 7]

Magofu ya Yeriko, ambako Yehova aliwapa Waisraeli ushindi

[Hisani]

Pictorial archive (Near Eastern History) Est.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki