Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w74 7/15 uku. 333
  • Ufahamu Katika Habari

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ufahamu Katika Habari
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1974
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Amani Kupitia kwa Sheria
  • Ogofyo la Njaa
  • Ni Nini Kilicho Nyuma ya Sayari?
    Amkeni!—1999
  • Nyotamkia Yagonga Sumbula!
    Amkeni!—1997
  • Vimondo Hutoka Wapi?
    Amkeni!—1993
  • Njaa Ina Maana Gani?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1984
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1974
w74 7/15 uku. 333

Ufahamu Katika Habari

Amani Kupitia kwa Sheria

● Muda huu wa miaka kumi umekuwa muda ambao mengi yamesikiwa juu ya kupunguza mizozo, maendeleo ya hali za kisiasa za kati ya mataifa na mapatano ya kumaliza uundaji wa silaha. Mwendo wa kuelekea amani ya kweli ni wenye nguvu kadiri gani?

Majuzi Chuo cha London cha Uchunguzi wa Maarifa ya Vita kinatupasha habari katika taarifa yake kwamba silaha zaidi, si chache zaidi, zinaundwa. Na penye Mkutano wa Ulimwengu juu Amani ya Ulimwengu Kupitia kwa Sheria, msemaji C. S. Rhyne alisema kwamba hata “hatuna amani” na Umoja wa Mataifa. Sababu? Alijibu: “Hatuna amani, rafiki zangu, kwa sababu umbo na mwundo havionyeshi maana yenyewe. Bila nia ya kufuata njia ya amani, vyama vyote katika ulimwengu ni vya bure.”

“Amani ya Ulimwengu Kupitia kwa Sheria”​—ndiyo, lakini sheria ya nani na ikifikilizwa na serikali gani? Karibu mataifa yote yana mazoezi ya lazima ya vita. Hakuna yaliyo na mazoezi ya lazima ya amani.

Walakini, katika Isaya 2:2-4 Biblia inatabiri kwamba watu wengi wanaielekea serikali ya kimungu na kwamba “itatoka sheria” ya Mungu iwafikie wao. Matokeo kati yao ni ya kwamba “taifa halitainua upanga juu ya taifa lingine, wala hawatajifunza vita tena kamwe.” Njia ya kuifikiliza sheria hiyo katika dunia yote ni ufalme wa Mwana wa Mungu. Wale wanaoitafuta amani kwa unafiki bila kupitia kwa sheria ya Mungu wataondolewa karibuni na ufalme huo.​—1 The. 5:3.

Ogofyo la Njaa

● Kwa kuongezeka wataalamu wa kilimo wanaonya juu ya upungufu mkali wa chakula unaokuja kwa kadiri ya kuenea pote ulimwenguni. Kuna mataraja gani ya kuepuka njaa?

Wengi wanafarijiwa na mavuno mema yaliyomo katika nchi fulani kubwa. Lakini kipindi kimoja cha mavuno hakitoshi. Katika nchi ya U.S., ambayo ndiyo nchi kubwa katika ulimwengu yenye kulima chakula, haziko akiba zaidi tena za nafaka. Mtaalamu wa sayansi ya chakula Georg Borgstrom anasema: “Watu wangali wakisadiki kwamba njia fulani kubwa yenye akili ya ufundi itaondoa ugumu huo.”

Huenda wengine wakajaribu mmoja mmoja kuweka akiba ya chakula ili kuzuia njaa kuu za wakati ujao. Hii inatoa usalama wa kadiri gani? Ikiwa nguvu za umeme zinashindwa, ni jambo gani linalotukia kwa vile vyakula vya barafuni? Na ikiwa hali zinazidi kuwa mbaya sana, je! wale walio na vyakula vingi wasingekuwa watu wa kushambuliwa sana na watu wenye kuumizwa na njaa?

Biblia ilitabiri upungufu wa chakula kama sehemu ya ishara ya nyakati zetu. (Mt. 24:3, 7, 21; Ufu. 6:1-8) Zaidi ya haya, huenda katika “dhiki kubwa” inayokuja, wapinzani wa ufalme wa Mungu wakatafuta kwa nguvu kuwatia watumishi wake katika hali zenye njaa. Usalama wa Wakristo wa kweli hautakuwa katika akiba ya vyakula, bali katika ulinzi wa Mungu. Wanaweza kujiunga na nabii katika kusema kwa hakika hivi: ‘Mashamba yajapokuwa hayatoi chakula; walakini nitamshangilia Mungu wa wokovu wangu.’​—Hab. 3:17, 18; Ufu. 10, 14.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki