Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w79 8/15 kur. 20-21
  • Mwenye Hekima Alikuwa na Maana Gani?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mwenye Hekima Alikuwa na Maana Gani?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1979
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Kufuatia Anasa Na Utamaduni Kunathawabisha Kidogo tu
  • Ni Nini Kinachofanya Maisha Yawe Yenye Kusudi?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2008
  • ‘Uone Mema kwa Sababu ya Kazi Yako’
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1978
  • Mwenye Hekima Alikuwa na Maana Gani?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1979
  • Kitabu Cha Biblia Namba 21—Mhubiri
    “Kila Andiko, Lenye Pumzi ya Mungu, Lafaa”
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1979
w79 8/15 kur. 20-21

Mwenye Hekima Alikuwa na Maana Gani?

Kufuatia Anasa Na Utamaduni Kunathawabisha Kidogo tu

Mfalme Sulemani alipata kuona kwamba kujipatia hekima na maarifa si mradi unaoridhisha. Kwa sababu hiyo alichunguza sehemu nyingine za maisha, kutia na anasa na utamaduni.

Je! Sulemani alipata uradhi wa kweli kutokana na anasa, kujifurahisha na kicheko? Aliandika hivi: “Nikauambia moyo wangu, Haya, nitakujaribu kwa njia ya furaha; basi ujifurahishe kwa anasa. Na tazama, hayo nayo yakawa ubatili. Nikasema juu ya kicheko, Ni wazimu; na juu ya furaha, Yafaa nini?​—⁠Mhu. 2:1, 2.

Ilikuwa bure tu kwamba Sulemani alitafuta jambo linalofaa katika kujifurahisha na kicheko. Kufuatia anasa hakuleti furaha ya kweli na yenye kudumu. Kucheka pamoja na kujifurahisha kunaweza kumsaidia mtu asahau taabu zake kwa kitambo tu. Walakini taabu hazitaisha, baada ya kujifurahisha, huenda hata zikaonekana zikiwa kubwa zaidi. Kwa kufaa Sulemani angeweza kukiita kicheko “wazimu,” kwa kuwa kucheka bila kutumia akili kunazuia mtu kufanya maamuzi timamu. Kicheko kinaweza kumfanya mtu achukue mambo mazito kwa urahisi hivyo awaudhi au kuwakasirisha wengine. Mchezo au namna ya kujifurahisha kunakoshirikishwa na maneno na matendo ya mcheshi hakuna maana. Hakuwezi kuonyeshwa kukileta jambo lo lote la maana.

Kwa kuwa hakufurahishwa na matokeo ya anasa, kujifurahisha na kicheko, Sulemani alijaribu matokeo yanayoletwa na divai. Anaendelea kuandika hivi: “Moyoni mwangu nikapeleleza jinsi ya kuuburudisha mwili kwa mvinyo, na (moyo wangu ukali ukiniongoza kwa hekima) jinsi ya kushikana na upumbavu, hata niyaone yaliyo mema ya kuwafaa wanadamu, ili wayafanye hayo chini ya mbingu siku zote za maisha yao.” (Mhu. 2:3) Katika kuutumia mvinyo, Sulemani aliongozwa na hekima. Yeye hakupata kuwa mlevi, bali aliendelea kujiweza. Kwa hiyo, ‘kushikamana kwake na upumbavu,’ hakukumaanisha kwamba alitupilia mbali kiasi. Mahali pake, alipokuwa akipeleleza (akichunguza) namna ya maisha ya urahisi alitumia kujiweza yeye hakupata kuwa mtafuta-anasa mfisadi. Kwa kuwa Sulemani aliendelea kushikilia akili zake zote, yeye angeweza kwa kufaa kuona thamani ya matokeo ya uchunguzi wake,

Akieleza utendaji wake zaidi, anasema: “Nikajifanyizia kazi zilizo kubwa; nikajijengea nyumba; nikajipandia mashamba ya mizabibu; nikajifanyizia bustani na viunga, na kuipanda humo miti yenye matunda ya kila namna; nikajifanyizia birika za maji, ya kuunyeshea mwitu mlimopandwa miti michanga. Nami nikanunua watumwa na wajakazi, nikawa na wazalia nyumbani mwangu; tena nikawa na mali nyingi za ng’ombe na kondoo, kupita wote walionitangulia katika Yerusalemu; tena nikajikusanyia fedha na dhahabu, na tunu za kifalme na kutoka katika majimbo. Nikajipatia waimbaji, waume kwa wake, nao wale ambao wanadamu wanawatunuka, masuria wengi sana. Basi nikawa mkuu, nikaongezeka kupita wote walionitangulia katika Yerusalemu; pia hekima yangu nikakaa nayo. Wala sikuyanyima macho yangu cho chote yalichokitamani; wala sikuuzuia moyo wangu katika furaha yo yote; maana moyo wangu ulifurahi kwa sababu ya kazi yangu yote, na hii ilikuwa sehemu yangu katika kazi yangu yote.”​—⁠Mhu. 2:4-10.

Akiwa na cheo cha mfalme, Sulemani alikuwa na mali iliyomwezesha kufanya lo lote alilotaka kufanya. Hata hivyo yeye kakutupilia mbali hekima alipofuatia kazi bora pamoja na utamaduni​—⁠ujenzi, ukulima, michoro ya sehemu za nchi zenye kupendeza pamoja na muziki. Kwa hiyo Sulemani hakutumia mali zake zote bali alizidi kulundika fedha na dhahabu zaidi. ‘Aliendelea kuwa na hekima yake,’ ikimwongoza katika utendaji wake mwingi. Pia aliweza kupata furaha kadiri fulani kutokana na aliyotimiza. Lakini je! Kweli Sulemani alipata kuona kitu chenye thamani yenye kudumu katika kufuata mambo haya mbalimbali? Jibu lake ni: “Kisha nikaziangalia kazi zote zilizofanywa kwa mikono yangu, na taabu yote niliyotaabika katika kuzitenda; yote ni ubatili na kujilisha upepo, wala faida hakuna chini ya jua.” (Mhu. 2:11) Ndiyo, hata mambo ambayo yanaweza kufikiriwa kuwa mambo yanayofaa, aliyaona kuwa kazi bure, ubatili. Alijua kwamba angepatwa na mauti naye hakuwa na njia yo yote ambayo katika hiyo angejua ambayo yangeipata kazi zake alizojitaabisha nazo.​—⁠Mhu. 2:17-19.

Kweli, kufuatia sana anasa na utamaduni hakumletei mtu maisha yenye furaha na uradhi. Kwa kweli, yeye ambaye jambo kubwa maishani mwake ni kufuatia mambo kama hayo huenda mwishowe akaona kwamba maisha yake hayana maana na kwamba anahitaji chakula cha kiroho.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki