Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w79 1/15 kur. 20-22
  • Mwenye Hekima Alikuwa na Maana Gani?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mwenye Hekima Alikuwa na Maana Gani?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1979
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Tumia kwa Hekima Nguvu za Ujana
  • Mkumbuke Muumba Wako Mtukufu!
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1999
  • Enyi Vijana—Je! Mnaelekea Kufaulu Kweli Kweli
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1979
  • Tumia Maisha Yako kwa Njia Ifaayo Kabisa
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1998
  • Vijana Wanaofurahisha Moyo wa Yehova
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1979
w79 1/15 kur. 20-22

Mwenye Hekima Alikuwa na Maana Gani?

Tumia kwa Hekima Nguvu za Ujana

Mtu anapokuwa na uwezo na nguvu za ujana, maisha yanaweza kuwa yenye furaha. Mfalme Sulemani mwenye hekima aliandika hivi: “Wewe, kijana, uufurahie ujana wako, na moyo wako ukuchangamshe siku za ujana wako, ukaziendee njia za moyo wako na katika maono ya macho yako; lakini ujue wewe ya kwamba kwa ajili ya hayo yote Mungu atakuleta hukumuni. Kwa hiyo ondoa majonzi moyoni mwako, nawe uuondoe ubaya mwilini mwako; kwa maana ujana ni ubatili, na utu uzima pia.”​—⁠Mhu. 11:​9, 10.

Muumba anataka vijana wafurahie maisha naye hawi na maoni mabaya juu ya mapendezi ya vijana pamoja na tamaa zinazovutia mioyo na macho ya vijana. Hata hivyo, vijana wanahitaji kukumbuka kwamba watatoa hesabu kwa Mungu juu ya matendo yao. Ajapowaruhusu vijana uhuru wa kuchagua, Aliye Juu Zaidi hatawakinga wasipatwe na matokeo mabaya ya kufuata mwendo mbaya. Kwa kujiepusha na njia ya maisha yenye upotovu na ujinga, vijana wanaweza kujikinga na kila namna ya ubatili na madhara.

Sulemani akiongozwa na Mungu anaandika kwamba “ujana ni ubatili, na utu uzima pia.” Kwa sababu gani hivyo? Sababu moja ni kwamba, kwa wazi mtu haendelei kuwa kijana milele. Vilevile, furaha na faida za uwezo na nguvu za ujana ni za muda wenye mashaka. Hata vijana hupatwa na ugonjwa na mauti. Kijana anayedharau uhakika huu huenda akakosa kutumia aliyo nayo kwa hekima, akitumia nguvu na uwezo wa mwili wake katika njia ya maisha ambayo inaweza kufanya maisha yake ya baadaye anapokuwa mtu mzima yawe magumu sana.

Kwa hiyo, kwa kufaa sana, Mfalme Sulemani anaelekeza vijana kwa Yeye ambaye wanapaswa kumtolea maisha zao. Anasema hivi: “Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako, kabla hazijaja siku zilizo mbaya, wala haijakaribia miaka utakaposema, mimi sina furaha katika hiyo.” Kabla jua, na nuru, na mwezi, na nyota, havijatiwa giza; kabla ya kurudi mawingu baada ya mvua.”​—⁠Mhu. 12:​1, 2.

Hakuna wakati unaofaa zaidi wa kufikiri kwa uzito juu ya Muumba kuliko wakati mtu anapokuwa katika upeo wa maisha yake, wakati anapoweza kupata matokeo yaliyo bora zaidi katika utumishi wa Aliye Juu Zaidi. Uwezo huo unatoweka wakati wa “siku zilizo mbaya” za uzee wakati mwili unapokuwa dhaifu na kupatwa na magonjwa. Sana sana mtu ambaye ametumia vibaya ujana wake atakuwa ‘hana furaha’ na miaka ya mwisho ya maisha yake. Sulemani anafananisha wakati wa ujana na wakati wa kiangazi katika Palestina wakati jua, mwezi na nyota hutoa nuru zao kutoka mbingu zisizo na mawingu. Katika wakati wa uzee, wakati huo huwa umetoweka nazo siku huwa kama zile za majira ya baridi, yenye mvua, zikiwa na taabu nyingi moja baada ya nyingine.

Akieleza juu ya matokeo yanayoletwa na uzee katika mwili wa mwanadamu, ambao anafananisha na nyumba, Sulemani anaendelea kusema hivi: “Siku ile walinzi wa nyumba [mikono ambayo huangalia mwili na kuupa mahitaji yake] watakapotetema; hapo [wanaume] wenye nguvu [miguu] watakapojiinamisha; [nao wanawake, meno] wasagao kukoma kwa kuwa ni haba; na hao [wanawake] wachunguliao madirishani [macho] kutiwa giza; na milango [ya kinywa, midomo] kufungwa katika njia kuu [kwa kuwa kinasema mara chache sana hadharani] sauti ya kinu itakapokuwa ni ndogo [kwa kuwa sauti ya kutafuna kwa ufizi usio na meno huwa ndogo sana na isiyosikika], na mtu kusituka [huamuka] kwa sauti ya ndege [kwa sababu usingizi ni mwepesi sana]; nao binti za kuimba watapunguzwa [kwa kuwa kuna shida ya kusikia; tena, sauti ni dhaifu, ikifanya kuimba ko kote kwa nyimbo kuwe dhaifu]”​—⁠Mhu. 12:​3, 4.

“Naam, wataogopa kilichoinuka [kwa kujua kwamba huenda wakaanguka], na vitisho vitakuwa njiani [sasa njia kuu zajawa na hatari kwa kutoweza kuona na kusikia vizuri na kutokumbuka mambo kwa urahisi]. Na mlozi utachanua maua [nywele zinakuwa na mvi na kuanguka kama vile maua meupe ya mlozi yanavyoanguka chini], na panzi [mtu mzee, mwili wake ukiwa umejikaza na kuinama, viko vya mikono yake vikiwa vimerudishwa nyuma, huenda akafanana na panzi] atakuwa ni mzigo mzito [atajikokota, NW]—; na pilipili hoho itapasuka [kwa kuwa inashindwa kuamsha tamaa ya kula chakula katika mzee ambaye hamu yake ya chakula imepungua], maana mtu aiendea nyumba yake ya milele [kaburi], nao waombolezao wazunguka njiani. Kabla haijakatika kamba ya fedha [uti wa mgongo]; au kuvunjwa bakuli la dhahabu [fuvu la kichwa linalouchukua ubongo linalofanana na bakuli], au mtungi [moyo] kuvunjika kisimani; au gurudumu [la kisima; mzunguko wa damu] kuvunjika birikani; nayo mavumbi kuirudia nchi kama yalivyokuwa, nayo roho [nguvu ya uhai] kumrudia Mungu aliyeitoa.” (Mhu. 12:5-7) Kurudi huku kwa roho au nguvu ya uhai kwa Mungu kunamaanisha kwamba Aliye Juu Zaidi ndiye mwenye mamlaka juu ya roho hiyo sasa. Mungu peke yake ndiye awezaye kumrudisha hai aliyekufa.

Kijana mwenye hekima kweli kweli ni yule anayetumia wakati na nguvu zake vizuri kwa kumtumikia Muumba wake. Yeye hatajutia hili anapokuwa mtu mzima naye atakuwa katika hali bora zaidi anaposhindana na hali ya kupungukiwa na nguvu za mwili wake. Licha ya hayo, kwa kuishi kulingana na amri za Muumba, analindwa asipoteze afya na nguvu zake mapema mno isivyofaa.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki