Maswali Kutoka Kwa Wasomaji
● Kwa sababu ya namna miji ya Dresden, Stalingrad, Hiroshima na Nagasaki ilivyoharibiwa vibaya sana katika Vita ya Pili ya Ulimwengu, Yesu angewezaje kueleza yale yaliyoupata Yerusalemu katika mwaka wa 70 W.K. kuwa ‘dhiki kubwa ambayo haijapata kutokea kamwe, wala haitatokea tena’?
Unabii huo ulikuwa na utimizo wa wakati ujao ambao ungetukia baada ya yale yaliyoupata Yerusalemu na Wayahudi katika mwaka 70 W.K., walakini yaliupata mji huo na taifa hilo vilevile.
Haya maneno ni sehemu ya jibu la Yesu la kinabii alipokuwa akijibu ulizo la mitume wake juu ya kuwapo kwake kwa wakati ujao na juu ya mwisho wa taratibu ya mambo. (Mt. 24:3, 21; Marko 13:19) Mashahidi wa Yehova wamesema mara nyingi kwamba mengi ya yale yaliyotabiriwa na Yesu wakati huo yalikuwa na utimizo wa mara mbili; Kwanza, utimizo mdogo wa mambo yaliyotukia mpaka na kutia kuharibiwa kwa Yerusalemu na taratibu ya mambo ya Kiyahudi na Warumi katika mwaka 70 W.K. Pili, Utimizo mkubwa tangu mwaka 1914 W.K., wakati Yesu alipoanza kuwapo kwake kusikoonekana mbinguni akiwa mfalme wa ufalme wa Kimasihi, kutia na mwisho ambao bado ni wa wakati ujao wa taratibu mbovu ya mambo ya ulimwenguni pote.—Tazama Mnara wa Mlinzi wa Februari 1, 1971, kurasa 29-43, na wa Machi 1, 1975, kurasa 110-113, Machi 15, 1975, kurasa 123-126.
Katika unabii huo Yesu alitilia mkazo uhitaji wa kukesha na kuwa tayari. Alisema hivi: “Ombeni, ili kukimbia kwenu kusiwe wakati wa baridi, wala siku ya sabato. Kwa kuwa wakati huo kutakuwapo dhiki kubwa, ambayo haijatokea namna yake tangu mwanzo wa ulimwengu hata sasa, wala haitakuwapo kamwe.”—Mt. 24:20, 21.
Onyo hilo la kukesha lilikuwa la maana sana kwa Wakristo waliokuwa wakiishi Yerusalemu na Uyahudi ambao wangepatwa na matokeo ya mwisho wa taratibu ya mambo ya Kiyahudi. Majeshi ya Kirumi yaliuzunguka mji huo katika mwaka 66 W.K., kisha bila kutazamiwa wakaondoka. Hiyo ndiyo iliyokuwa ishara ya pekee iliyokuwa imetajwa na Yesu katika Luka 21:20-22. Nayo historia hutuambia kwamba Wakristo watiifu waliitikia kwa kukimbia kutoka katika mji wa Yerusalemu na Uyahudi. Kwa hiyo, ni jambo la akili kutumia pia juu ya mji halisi wa Yerusalemu na Uyahudi yale yaliyosemwa na Yesu baadaye juu ya “dhiki kubwa.”
Uharibifu ulioletwa na Warumi katika mwaka 70 W.K., ulikuwa mkubwa na mbaya zaidi ya ule wa wakati Wababeli walipouharibu mji wa Yerusalemu katika mwaka 607 K.W.K. Vilevile, dhiki ya mwaka wa 70 W.K. ilileta uharibifu wa mwisho wa milele kwenye mji na hekalu lililokuwa limejengwa na Wayahudi pamoja na taratibu ya kidini iliyokuwa ikiendeshwa humo. Kwa hiyo, Yesu alisema kweli alipokuwa akitoa maelezo ya kinabii ya matukio yaliyotukia katika mwaka 70 W.K. kuwa “dhiki kubwa, ambayo haijatokea namna yake [katika mji huo, taifa pamoja na taratibu ya mambo] tangu mwanzo wa ulimwengu hata sasa, wala haitakuwapo kamwe.”
Walakini kuna zaidi. Sisi tunapaswa. Kwa sababu gani? Kwa sababu maneno ya Yesu katika Mathayo 24:21 kwa wazi yalikuwa na maana kubwa zaidi. Kuwapo kwa Kristo kusikoonekana akiwa mfalme wa Kimasihi akitawala juu ya dunia yote hakukuanza katika mwaka 70 W.K. Yeye mwenyewe alionyesha kwamba hata jambo hilo halingetazamiwa. Wakati mmoja wanafunzi wake “[walipokuwa wakidhani] ya kuwa ufalme wa Mungu utaonekana mara,” Yesu alitoa mfano unaojulikana kama mfano wa fedha. Ulihusu ‘mtu mmoja aliyesatiri katika nchi ya mbali ili ajipatie ufalme kisha arudi,’ ulionyesha kwamba kutawala kwake akiwa mfalme wa Kimasihi kulikuwa bado kuko mbali sana.—Luka 19:11-27.
Utimizo wa unabii wa Yesu katika kizazi kimoja juu ya vita, njaa, matetemeko ya nchi yasiyo na kifani (mfano) na mengineyo, unahakikisha kwamba utimizo mdogo juu ya Yerusalemu kabla ya mwaka 70 W.K. ulikuwa mfano tu wa yale yanayotupata sasa.a Kulingana na hayo, kipindi hiki cha sasa ni mwisho wa taratibu nzima mbovu ya mambo, ambao upeo wake utakuwa “dhiki, jinsi isivyokuwa tangu mwanzo wa kuumba.” (Marko 13:19) Itakuwa kubwa zaidi ya ilivyokuwa juu ya Yerusalemu, Uyahudi pamoja na taratibu ya mambo ya Kiyahudi katika mwaka wa 70 W.K. Kwa kweli, utakuwa mkubwa hata zaidi ya gharika ya wakati wa Nuhu wakati “dunia [yote] ya wakati ule iligharikishwa na maji, ikaangamia.” (2 Pet. 3:6) Hautapasa miji michache tu iliyo peke yake kama ile iliyoharibiwa katika vita vya karibuni. Utawapasa watu wote wanaoishi juu ya uso wa dunia, ambao sasa idadi yao ni kama 4,000,000,000.—2 Pet. 3:7-13.
Usahihi wa maneno ya Yesu katika Mathayo 24:21 kwa habari ya yale yaliyotukia katika mwaka 70 W.K. unapaswa ukazie ndani yetu uhakika wa utimizo mkubwa zaidi wa maneno hayo katika wakati wetu.
[Maelezo ya Chini]
a Tazama Amani ya Kweli na Usalama wa Kweli—Kutoka Chanzo Gani?, kurasa 78-89.