‘Wamewanda na Kung’aa’
Yeremia 5:28 huwaeleza wale ambao hujitajilisha katika njia za uvunjaji wa sheria: “Wamewanda sana, wang’aa; naam, wamepita kiasi kwa matendo maovu.” Watu hao waovu walikuwa wamewanda (wamenona) katika maana ya kwamba walikuwa wamejilisha chakula cha kuwapa afya. Hivyo, ngozi yao haikuwa ikining’inia kana kwamba walikuwa wakifa njaa. Hapana, ilikuwa imejazwa kabisa na kuwa laini, ‘imeng’aa.’ Walakini utajiri wao ulikuwa wa kitambo tu. Yehova angetaka hesabu kwao.—Yer. 5:29.