Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w81 2/15 kur. 3-4
  • Utafutaji wa Usalama

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Utafutaji wa Usalama
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1981
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Je! Nguvu za Kijeshi Ndilo Jibu?
  • Kutamani Usalama ni Jambo la Kawaida kwa Wote
  • Amani na Usalama wa Kweli Ni Karibu!
    Amani na Usalama wa Kweli—Wewe Unaweza Kuupataje?
  • Kuhisi Usalama Sasa na Kuwa Salama Milele
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2002
  • Usalama wa Kweli—Sasa na Milele
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1996
  • Wewe Unaweza Kupataje Usalama wa Kweli?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1977
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1981
w81 2/15 kur. 3-4

Utafutaji wa Usalama

BWA. NA BI. A​——​ na watoto wao watatu matineja (vijana) walikuwa wanaishi Afrika. Kwa miaka 20 walikuwa wametengeneza shamba lao lenye kupendeza nao walikuwa wametumia fedha zao kwa nyumba iliyo starehe, mazao ya shambani, wanyama wa kufugwa na mashine za ukulima. Hiyo ikawa ngome yao ndogo, kimbilio lao wakati wa taabu na huzuni, chanzo chao cha kuburudisha na kupumzika baada ya kila siku ya kufanya kazi kwa bidii. Walijiona kuwa salama.

Kwa haraka, mambo yalibadilika. Kwa muda fulani vyama vya kisiasa vilikuwa vinapata nguvu katika nchi hiyo. Wanaume waliokuwa wameazimia kuleta badiliko kwa kutumia nguvu walikuwa wanafanya vitendo vya ujeuri nao walikuwa wameweka baruti katika barabara zenye mashimo zisizo na kokoto za maeneo hayo ya ukulima. Bwa. A​——​ alipokuwa akirudi akiwa katika gari lake la Land Rover kutoka safari yake ya mjini aliyokuwa akifanya kila juma, alikanyaga baruti moja ikalipuka akauawa papo hapo.

Bi. A​——​ na jamaa yake hawakujiona tena kuwa salama. Kwa sababu ya kuongezeka kwa vitisho vya jeuri katika ujirani, mahangaiko katika kulitunza shamba na bila mwanamume katika nyumba, alijiona ana lazima ya kuondoka katika shamba ambalo wakati mmoja lilikuwa ni mahali salama. Jamaa hiyo ikahama kwenda nchi nyingine ikiwa na tumaini la kupata njia salama zaidi ya maisha.

Katika nchi iyo hiyo ya Afrika, mambo yalibadilika kwa kadiri kubwa kwa muda wa miaka michache. Nyumba za mashambani zilizozungukwa na mimea mingi na zenye ishara inayosema “karibu” zilizungukwa na boma refu la chuma chenye seng’enge juu yake. Mifuko yenye changarawe iliwekwa kuzunguka kuta za nyumba, nayo madirisha yalilindwa kwa waya za chuma.

Vilevile maisha ya mjini yalibadilika wakati watu wengi zaidi na zaidi walipoweka kengele za kujulisha kuna wevi wa kuvunja nyumba, wakaweka malango makubwa yenye kufuli na minyororo katika maingilio ya nyumba zao, nao wakaweka mbwa wa kulinda ili kuzuia wavamizi wasiotakiwa. Madirisha ya maduka yalitiwa utepe wa pekee ili kuyazuia yasivunjike-vunjike. Walinzi waliwekwa ili wawapekue wanunuzi walipokuwa wakiingia katika maduka makubwa. Wenye kwenda likizoni walilipa polisi ili walinde nyumba zao wakati wa vipindi wasipokuwapo.

Katika maeneo mengi, kuendesha gari katika mashamba ya Afrika ambako wakati mmoja kulikuwa kwenye amani kukawa kwenye kutia wasiwasi kutoka mji mmoja kwenda mwingine. Wasafiri walishauriwa wawaarifu polisi kabla ya kuondoka, na wengi wakasafiri katika vikundi vyenye kulindwa na magari yenye silaha. Sheria za kijeshi na kuzuiwa kutoka nje saa fulani yakawa mambo ya maisha ya kila siku kwa watu.

Pamoja na kuchukua hatua hizo za usalama, wengi ambao walikuwa na uwezo walifanya mipango ya ziada kwa ajili ya usalama wao kwa kuweka mali zao kwa namna ya dhahabu, fedha, vito vya thamani na vitu vilivyochorwa au kwa kuweka fedha zao katika benki za nchi nyinginezo. Walifanya hivyo ili kwamba mambo yakiharibika, waendelee kuwa na mali fulani.

Mambo hayo hayapo katika nchi hiyo peke yake. Inawezekana kwamba katika ujamii wako umeona baadhi ya mipango iyo hiyo ya usalama na kukaza fikira zaidi kwa watu wengi kwa ajili ya usalama wa nyumba zao na jamaa zao. Ulizo ni hili, Je! jitihada hizo zinaleta kweli kweli amani ya akili na usalama ambao sote tunataka?

Je! Nguvu za Kijeshi Ndilo Jibu?

Wasiwasi uo huo unaonyeshwa na vitendo vya serikali. Serikali nyingi zinachukua hatua ambazo hazijapata kuchukuliwa hapo mbeleni ili zilinde mipaka yazo na kulinda mabalozi wao. Ziara ya malkia wa Uingereza katika kusini mwa Afrika na ziara ya papa katika Ireland zilifanya mamia ya wanaume wawekwe tayari wakiwa na silaha kwa makusudi ya usalama peke yake. Kwenda kwa meli, ndege au wanajeshi kwenye sehemu zinazoonwa kuwa ni zenye kufaa katika vita kunafasiriwa na nchi fulani kuwa ni tisho la usalama wa taifa zima na mara nyingi jambo hilo linatokeza hatua za kijeshi za kujikinga zichukuliwe.

Serikali nyingi zinaamini kwamba usalama wa taifa zima unategemea kujitayarisha kijeshi. Kuonyesha hilo, UNESCO (Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni) hivi karibuni iliripoti kwamba fedha zinazotumiwa na ulimwengu juu ya silaha ni “karibu shilingi milioni saba kwa dakika moja” na kwamba asilimia 75 (750) yazo inatumiwa na nchi zinazoendelea kusitawi. (The Courier, Aprili 1979, uku. 19) Walakini matumizi hayo makubwa ya kijeshi yanaleta maono ya usalama wa kweli kwa watu wanaoishi katika nchi hizo ambako wanaona njaa na maradhi yenye kuenezwa na maji yakiua maelfu kila siku?

Kwa mara nyingine twauliza hivi, Je! nguvu za kijeshi kweli kweli zinamaanisha usalama? Ni kweli kwamba mtu anaweza kuondoa mawazo hayo katika akili yake. Walakini je! kweli kweli anaweza kujiona salama anapofikiri kwa uzito juu ya uhakika wa kwamba serikali katika ulimwengu wote zina makombora yanayotosha kuweza kutuua sote mara nyingi? Kuonyesha jambo hilo: Je! unaweza kupumzika kwa amani wakati wa usiku ukiwa na bombom (bunduki inayopiga risasi nyingi kwa mfululizo) chini ya kitanda chako huku ukifahamu kwamba jirani yako anayo kama hiyo akiielekeza nyumbani mwako na kwamba anatamani nafasi ya kuitumia anapoona kwamba kufanya hivyo kusingeleta hatari yo yote kwake?

Kutamani Usalama ni Jambo la Kawaida kwa Wote

Ni jambo la kawaida kwamba sote twataka kujiona salama. Hata katikati ya wanyama kuna tamaa waliyoumbwa nayo ya kuwa salama. Ndege wanatengeneza viota vyao katika sehemu ambazo zimefichika sana au ambazo haziwezi kufikiwa kwa urahisi. Kindi wanaweka akiba karanga kwa ajili ya matumizi ya wakati wa baridi wa mwaka. Paka wanaokaribia kuzaa wanachunguza kila kabati katika nyumba ili watafute kificho cha kulishia watoto wao.

Ulizo linalotuelekea sote leo ni hili. Twaweza kutafuta usalama wapi? Kwa kuongozwa na silika wanyama wanatafuta usalama kwa vitu vya kimwili. Lakini namna gani wanadamu? Je! usalama wetu unapatikana katika vitu vya kimwili, hivyo kutufanya tusiwe bora zaidi ya wanyama? Je! inategemea kuajiriwa kazi au, pengine, kulundika mali kwa namna ya dhahabu, fedha au akiba katika benki? Je! silaha zinaweza kufanya maisha yetu yawe salama? Au, je! usalama unapatikana katika namna fulani ya serikali ambayo inaonekana kuwa imara zaidi kuliko nyinginezo?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki