Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w84 2/15 uku. 23
  • Maswali kutoka kwa Wasomaji

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Maswali kutoka kwa Wasomaji
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1984
  • Habari Zinazolingana
  • Matibabu Mbalimbali na Masuala Yanayohusika
    Amkeni!—2004
  • Kutumia Nguvu za Upepo
    Amkeni!—1995
  • Ongezeko la Watoto Wanaozaliwa kwa Njia Zisizo za Asili
    Amkeni!—2004
  • Tumbo la Uzazi—Makao Yetu ya Kwanza ya Ajabu
    Amkeni!—1992
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1984
w84 2/15 uku. 23

Maswali kutoka kwa Wasomaji

● Je! lingekuwa kosa kwa Mkristo kutumia vidude vyenye kugongana na kutokeza mlio mzuri kama wa kengele vinapovumishwa na upepo ndani ya nyumba yake?

Watu wengi wametumia vidude vya namna hiyo kufanya nyumba yao iwe na milio mizuri ya kimuziki. Upepo unapovuma, vile vitu vya kioo, chuma au mbao vinagongana na kutokeza mlio. Walakini, katika nchi fulani kuna desturi ya kuweka vidude vya namna hiyo kwa wazo la kwamba vitazuia pepo waovu (mashetani) wasiingie ndani ya nyumba. Ni wazi kwamba Mkristo asingetumia vidude hivyo kwa kusudi hilo. Kwa hiyo ikiwa nchi au mtaa ambamo mtu anakaa ina imani ya ushirikina, lisingekuwa jambo la hekima kuwa na vidude hivyo ndani ya nyumba. Kwa njia hiyo hakuna mtu atakayekwazwa wala kuwa na maoni ya kwamba Mashahidi wa Yehova wanatumia vidude vyenye kugonganishwa na upepo kwa kusudi lisilopatana na Maandiko.​—1 Wakorintho 10:31-33.

Walakini, ikiwa kusudi la mtu la kuweka vidude hivyo nyumbani halihusiani hata kidogo na dini ya uongo, ushirikina wala ushetani, na havitaelekea sana kuwapa wengine maoni mabaya juu ya namna vinavyotumiwa nyumbani, hili ni jambo rahisi la kuamuliwa na mtu binafsi.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki