Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w82 6/1 uku. 24
  • Yehova ni Mnara Wenye Nguvu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Yehova ni Mnara Wenye Nguvu
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1982
  • Habari Zinazolingana
  • Jikoni Kwaweza Kuvutia
    Amkeni!—1997
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1997
  • Endelea Kuwa Mtulivu na Kumtumaini Yehova
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2021
  • 2. Dumisha Usafi
    Amkeni!—2012
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1982
w82 6/1 uku. 24

Yehova ni Mnara Wenye Nguvu

WOKOVU unatokana na kumtumaini Yehova, kama walivyojionea dada wawili wa tumbo moja katika upande wa kusini-mashariki wa Ufaransa. Mmoja wao anasimulia hivi:

“Ilikuwa saa 6:30 baada ya usiku wa manane nasi wawili tulikuwa tumelala kwa utulivu. Ghafula, tuliamshwa na sauti ngeni iliyokuwa ikitoka jikoni, halafu mwanamume mmoja akatokea mlangoni. Akiwa amepigwa na bumbuazi (wasiwasi), dada yangu alipiga kelele hivi: ‘Yehova, Yehova, tafadhali tusaidie!’ Baada ya kusema maneno hayo mwanamume huyo alituamuru tukae kimya huku akitutisha kwa kisu na kwa chua (chuma cha kukwaruzia). Yehova na ashukuriwe kwa kuwa tulitulia na tukavaa nguo.

“Mvamizi huyo alikuwa amepanda kwenye varanda yetu iliyokuwa katika orofa ya tano na alikuwa ameukata mkono wake alipokuwa akivunja dirisha la jikoni ili aingie ndani. Kwa hiyo nikaushughulikia mkono wake na nikatayarisha chakula na kahawa ili nimsaidie atokwe na matokeo ya kileo yaliyokuwa yamesalia ndani yake. Vilevile, nilizungumza naye juu ya Yehova, na nikamwonyesha namna tunavyopaswa kumtumaini Yeye. Alijibu kwamba yeye hakumjua Yehova, hata akalitukana jina lake. Huku akitazama-tazama, dada yangu aliisoma Biblia nami nilitoa sala nikiwa kimya. Kwa kuwa inaonekana aliudhiwa na utulivu huo alichukua kipande cha dirisha kilichovunjika, akakiwekelea kwenye koo la dada yangu, huku akiwa amekiweka kisu kwenye shingo yake, na akasema hivi: ‘Acha nifinye kidogo damu ianze kutiririka!’ Nilisimama na nikasema kwa sauti yenye kusikika wazi; ‘Wewe huwezi kutuogopesha, kwa maana Yehova yupo atutegemeze na atuokoe. Hata ukituua tuna tumaini la kufufuliwa.’ Akaacha alipotatizwa na maneno hayo.

“Ilikuwa saa 8:45 baada ya usiku wa manane aliposema angeondoka, nami nikamsindikiza mpaka mlangoni. Alipokuwa akitoka nje, alisema hivi: ‘Haya Nimefahamu. Yehova ni mwenye nguvu zaidi yangu.’ Baada ya kufunga pazia za jikoni, tulitoa sala kumshukuru Yehova Mungu wetu, ambaye hakuwa ametuacha.​—Mithali 18:10.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki