Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w83 6/15 kur. 3-4
  • Wewe Umepata Kukatishwa Tamaa na Kibandiko?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Wewe Umepata Kukatishwa Tamaa na Kibandiko?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1983
  • Habari Zinazolingana
  • Ukristo wa Kisasa Ni wa Kweli Kiasi Gani?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1983
  • Waumini Wako Wapi?
    Amkeni!—1996
  • Jinsi Jumuiya ya Wakristo Ilivyokuja Kuwa Sehemu ya Ulimwengu Huu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1993
  • Rafiki Bandia ya Biblia
    Biblia—Neno la Mungu au la Binadamu?
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1983
w83 6/15 kur. 3-4

Wewe Umepata Kukatishwa Tamaa na Kibandiko?

JE! UMEPATA kununua bidhaa fulani yenye kibandiko kinachovuta macho, halafu unakuja kukuta kwamba haikuwa nzuri sana kama ilivyoonyeshwa na kibandiko hicho? Ulikata tamaa, sivyo? Labda uliamua kwamba hutanunua bidhaa hiyo tena. Mamilioni ya watu leo wamepatwa na hali kama hiyo kuhusiana na dini. Hapo kwanza walivutwa na kibandiko cha neno “Ukristo” kisha wakajitengea mbali kwa sababu ya mambo waliyoona na yaliyowapata.

Kulingana na takwimu (hesabu), karibu mtu mmoja kati ya kila watu wanne wa idadi ya ulimwengu mzima anasemwa kuwa Mkristo. Katika zile bara mbili za Amerika na katika Ulaya hesabu yenyewe ni kubwa kuliko hiyo. Lakini je! takwimu zinaeleza mambo kama yalivyo? Namna gani wewe mwenyewe? Je! ulibatizwa ukaingia katika dini ya Kikristo? Ikiwa ndivyo, je! unajihesabu kuwa Mkristo? Au ni kibandiko tu?

Kuonyesha tunavyomaanisha, acha tuchukue mifano miwili: Spania, ambayo ni nchi ya Kikatoliki, na Uingereza, ambayo ni nchi ya Kiprotestanti. Ensaiklopedia (kitabu) moja inapanga uhusiano wa watu na dini muda wa katikati ya miaka ya 1960 kama hivi: Katoliki ya Roma, watu 31,200,000; Uprotestanti, watu 43,000; Dini ya Kiyahudi, watu 5,000. Hivyo, kwa maneno tu, nchi ya Spania ina Ukristo wa asilimia 99.85. Lakini, kama hali ilivyo katika nchi zilizo nyingi, Spania ina kiasi fulani cha watu wasioamini Mungu yuko, wanaoamini kwamba habari za Mungu haziwezi kujulikana, na Wakatoliki na Waprotestanti walioacha kuamini mambo ya Mungu. Ni jambo la uhakika kwamba asilimia 99.85 hawaendi kanisani kila juma, hata kila mwaka!

Ndivyo ilivyo katika Uingereza, ingawa huko hali hiyo imezidi. Ensaiklopedia ile ile inatoa idadi hizi kuhusiana na dini: Kanisa la Uingereza, watu 27,500,000; Katoliki ya Roma, watu 6,000,000, halafu tarakimu nyingine kwa dini kubwa-kubwa zilizobaki. Ni wangapi wa hao 27,500,000 walio Waanglikana wenye kwenda kanisani kikweli? Ni wachache sana, ikiamuliwa kulingana na tarakimu rasmi za wenye kwenda kanisani. Hesabu yenyewe hata haifiki asilimia 10 wakati ule ambao ni kawaida ya watu wengi kwenda kanisani, yaani, wakati wa sherehe ya Pasaka.

Basi jambo hilo linaonyesha nini? Kwamba mara nyingi kuna tofauti kati ya kibandiko cha kanisa na bidhaa yenyewe. Ni jambo moja kujisema kuwa Mwanglikana au Mkatoliki, lakini ni jambo tofauti kabisa kuwa mshiriki mwenye matendo wa imani hizo. Vivyo hivyo, ni jambo moja kujisema kuwa Mkristo, lakini ni jambo tofauti kabisa kuwa Mkristo, au mtu mwenye kufuata mfano wa Kristo.

‘Kusema Mkristo ndiyo kusema nini?’ huenda ukauliza. Maoni ya watu yanatofautiana kuhusu jambo hilo, lakini angalia kama unapatana na yo yote ya maoni yafuatayo ambayo yanaonyeshwa na watu wengi:

Mkristo ni mtu ye yote anayeamini Yesu Kristo.

Mkristo ni mtu ye yote aliyebatizwa katika kanisa la Kikristo.

Mkristo ni mtu wa kanisa fulani la Kikristo ambaye analihudhuria.

Mkristo ni mtu ye yote asiyefanya madhara yo yote kwa jirani yake na ambaye anasaidia watu anapoweza.

Ni mtu anayeishi kulingana na vile Biblia inavyosema.

Wakristo ni wale tu ambao ‘wamezaliwa mara ya pili.’

Ni wale tu wanaomwamini papa (popu).

Ndiyo, watu wana maoni mengi yenye kutofautiana. Yametofautiana sana mpaka yakamfanya mwandikaji wa mambo ya kidini ambaye pia ni mhadhiri wa chuo kikuu, Ninian Smart, aandike hivi: “Ukristo ndio dini isiyoeleweka zaidi ya dini zote zilizo kubwa-kubwa. . . . Uko tofauti kuanzia Uorthodoksi wa Mashariki, kufikia Ukatoliki, mpaka kwenye namna nyingi sana za makanisa na madhehebu za Kiprotestanti. . . . Unaweza kukubali vita na unaweza kukubali kupatanisha watu wawe na amani. Unaweza kukubali watu wakae katika makao ya watawa wenye kujitenga na ulimwengu na bado ukubaliana na nia za kilimwengu. Unaweza kukubaliana na utawala wa viongozi wa kidini na bado ukubaliane na demokrasi, Unaweza kuhubiri na bado ukubali desturi za ibada tu. Unaweza kukubaliana na wanafalsafa na bado ukubaliane na wale wanaokataa falsafa.”

Lakini hiyo ni kweli kabisa? Je! Ukristo wa kweli unaweza kukubali vita, nia za kilimwengu na utendaji mwingine mwingi unaopingana ambao umeachiliwa uwe katika Jumuiya ya Wakristo muda wa miongo kadha ya miaka iliyopita? Ukristo wa kweli ni nini? Na je! Ukristo wa kisasa ni wa kweli?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki