Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w83 12/1 kur. 3-4
  • Wafu Wako Wapi?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Wafu Wako Wapi?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1983
  • Habari Zinazolingana
  • Namna Ambavyo Ufufuo Unavyowafaidi Wafu Wote Waliomo Katika “Hell”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1974
  • Je, Moto wa Mateso Ni Halisi? Kuzimu Ni Wapi Kulingana na Biblia?
    Maswali ya Biblia Yajibiwa
  • Ni Nani Wanaoenda Kuzimu?
    Maswali ya Biblia Yajibiwa
  • Je! Kweli Kuna Mahali Penye Moto wa Mateso?
    Unaweza Kuishi Milele Katika Paradiso Duniani
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1983
w83 12/1 kur. 3-4

Neno la Mungu Li Hai

Wafu Wako Wapi?

MWANAMUME ambaye analia hapa ni Yakobo. Anahuzunika sana kwa sababu anaamini mwana wake mpendwa, Yusufu, ameuawa. Lile vazi refu lililojaa damu ambalo Yakobo ameshika ni la Yusufu. Yakobo analia akisema, “Mnyama mkali amemla; bila shaka Yusufu ameraruliwa”!—Mwanzo 37:33.

Wale watu waliomzunguka Yakobo ni watoto wake. Wanajaribu kumfariji baba yao. Lakini, kama inavyoeleza tafsiri ya Biblia ya Union Version: “Akakataa kutulizwa, akasema, La! nitamshukia mwanangu, nikisikitika, hata kuzimu.”​—Mwanzo 37:35.

Yakobo aliamini Yusufu alikuwa wapi? Je! aliamini kwamba Yusufu alienda mahali pa mateso akakae huko milele, na je! Yakobo alitaka kwenda huko wakakutane? Au, badala ya hivyo, Yakobo aliwaza tu kwamba mwana wake mpendwa alikuwa amekufa na alikuwa kaburini na hivyo Yakobo mwenyewe akataka kufa?

Mtazame mwanamume huyu anayeona maumivu makali. Yeye ni Ayubu mwaminifu. Katika dhiki yake anapelekea Mungu sala inayosema: “Laiti ungenificha kuzimuni, ukanilinda kwa siri, hata ghadhabu zako zitakapopita, na kuniandikia muda ulioamriwa, na kunikumbuka!”​—Ayubu 14:13.

Ni wazi kwamba Ayubu anataka kufa ili aepuke taabu na maumivu yake. Kwa hiyo yeye anaamini hali yake itakuwa nini akifa? Wafu wako wapi? Ayubu haamini kwamba atakuwa hai mahali atakapoteswa akiwa motoni. Ayubu anajua kwamba mtu anapokufa mahali panapoitwa na Biblia hii ya Union Version kuzimu, anaenda kaburini tu. Huko mtu hawi na fahamu na kwa hiyo hakuna mateso. (Mhubiri 9:5, 10) Neno la Kiebrania lililotumiwa huko mwanzoni kabisa kutaja mahali hapa pa wafu ni Sheoli, nalo lina maana ya kaburi la ujumla la wanadamu wote. Kwa hiyo, katika maandiko yaliyoonyeshwa hapa kwa maneno, Biblia nyingine zinasema “kaburi” badala ya “kuzimu.”

Je! kuna tumaini lo lote kwa wale wasio na fahamu huko kaburini? Je! wanaweza kuishi tena? Ndiyo, Biblia inasema: “Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake.” (Ufunuo 20:13, 14) Ni habari njema kama nini! Mungu atawarudishia uhai watu ambao wamekufa, atimize tumaini la watu kama Ayubu walioamini kuna ufufuo​—Ayubu 14:14, 15.

[Picha katika ukurasa wa 3]

Wakati Yakobo anapoambia jamaa yake kwamba mwanaye yuko kuzimu, ana maana gani?

[Picha katika ukurasa wa 4]

Kuzimu​—sababu gani Ayubu akasali aende huko?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki