Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w84 1/1 uku. 8
  • Israeli na Zile “Nyakati za Mataifa”

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Israeli na Zile “Nyakati za Mataifa”
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1984
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Masihi Azinyenyekea Nyakati za Mataifa
  • Mfalme Atawala!
    “Ufalme Wako Uje”
  • “Israeli wa Mungu” na Mwisho wa Nyakati za Mataifa
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1984
  • Yerusalemu—“Sababu ya Shangwe”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1983
  • Nyakati Zilizowekwa za Mataifa
    Ufahamu wa Kina wa Maandiko
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1984
w84 1/1 uku. 8

Israeli na Zile “Nyakati za Mataifa”

“Yerusalemu utakanyagwa-kanyagwa na Mataifa [Goyimu], mpaka nyakati za Mataifa ziwe zimetimizwa.”​—LUKA 21:24, The New American Bible.

1. Maneno ya Yesu juu ya Yerusalemu yalitimizwaje, lakini ni ulizo gani linalobakia kujibiwa?

MIAKA 37 baada ya Yesu Kristo kuyasema maneno hayo yaliyo juu, mji wa Yerusalemu uliharibiwa na malejioni ya Kiroma yakiwa chini ya uongozi wa Jemadari Tito, katika mwaka wa 70 W.K. Lakini namna gani sehemu ile nyingine yote ya unabii wake, ile inayohusu kipindi ambacho katika hicho Yerusalemu ungekanyagwa-kanyagwa na Mataifa, akina Goyimu, kama wanavyoitwa leo na Wayahudi?

2. (a) Maneno ya Yesu yalimaanisha kwamba mji huo usingejengwa tena wala kukaliwa tena? (b) Ijapokuwa mji huo mtakatifu ulikaliwa kwa muda na wapiganaji wa vyenye kuitwa vita vitakatifu, Yerusalemu uliendeleaje kukanyagwa-kanyagwa na Mataifa mpaka zile “nyakati” zikamalizika?

2 Maneno hayo hayakumaanisha kwamba Yerusalemu usingejengwa tena na kukaliwa tena “mpaka nyakati za Mataifa [Goyimua] ziwe zimetimizwa.” Wakati wa karne iliyofuata ule mji ulijengwa Upya, na wale wenye kuitwa Wapiganaji wa Vita Vitakatifu wakafanya vita ili wajitwalie mji huo siku zile zilizotangulia kumalizika kwa karne ya kumi na sita. Wapiganaji hao wa Jumuiya ya Wakristo wenye madoa ya damu walijithibitisha kuwa ni Mataifa, au akina Goyimu, sawasawa na wale waliowatangulia katika kuusimamia mji huo na pia sawasawa na wale ambao waliwanyang’anya kwa jeuri wapiganaji hao wa vita vitakatifu mji huo! Akina Goyimu hao (“makafiri,” kama walivyokuwa wakiitwa na Jumuiya ya Wakristo) waliendelea kuukanyaga-kanyaga mji huo unaoonekana na Wayahudi kuwa mtakatifu sana.

3. Askari Waingereza walipokaribia kuuteka Yerusalemu katika mwezi Desemba wa mwaka 1917, Lord Rothschild aliambiwa nini na Katibu wa Uingereza wa Mashauri ya Kigeni, jina lake Balfour, lakini baada ya vita eneo la Palestina liliwekwa mikononi mwa nani?

3 Tarehe ya Desemba 9, 1917, askari wa Uingereza wakiwa chini ya uongozi wa Jemadari Allenby walinyang’anya Waturuki mji wa Yerusalemu, waliokuwa wamefanya mwungano na Kaiser Wilhelm wa Milki ya Ujeremani. Tukio hilo la ushindi lilipokuwa likikaribia, Katibu wa Uingereza wa Mashauri ya Kigeni, Arthur Balfour, alimpelekea Lord Rothschild wa jamaa mashuhuri ya Kiyahudi ya akina Rothschild barua yake ya Novemba 2, 1917. Alimtajia kwamba serikali ya Mfalme wa Uingereza ilipendelea Wayahudi waimarishiwe nchi katika Palestina iwe makao yao. Lakini, Vita ya Ulimwengu ya Kwanza ilipomalizika, Ushirika wa Mataifa (Goyimu) ulioanzishwa mwaka wa 1920 uliipa Serikali ya Uingereza mamlaka rasmi ya kusimamia Palestina (kutia ndani Yerusalemu), iisimamie mpaka mwaka wa 1948. Haikutajwa wazi ni nani angemiliki Yerusalemu baada ya kumalizika kwa muda wa hiyo Mamlaka Rasmi.

4. Baada ya ile Mamlaka Rasmi iliyotolewa na Waingereza juu ya eneo la Palestina kumalizika mwaka wa 1948, kulitukia nini huko upande wa vikundi vya wenye kupendezwa na eneo hilo?

4 Wakati Mamlaka Rasmi iliyotolewa na Uingereza ilipomalizika katika mwaka wa 1948, makundi ya wenye kupendezwa na nchi hiyo yalichukua hatua bila kukawia. Wafuasi wa Muhamadi walisimamia sehemu kubwa ya kipande cha mashariki cha eneo hilo, kutia ndani ule mji wenye kuta wa Yerusalemu na hekalu lake likawa la kuabudia Allah. Wayahudi walichukua kipande cha magharibi ya Palestina wakalitokeza lile taifa la kisasa la Israeli. Lakini ilipotokea ile Vita ya Siku Sita ya mwaka wa 1967 Waarabu walipokonywa mji wa Yerusalemu wenye kuta, kutia ndani ule Ukuta wa Kuombolezea ambao kwenye sehemu yake ya juu sana hekalu la ibada ya Wayahudi lilikuwa limesimama zamani Za kale. Wayahudi walisonga mbele kwa ushindi wakauteka ukingo wa magharibi wa Mto Yordani na wakaaji wake walio wafuasi wa Muhamadi.

5. (a) Yerusalemu wa leo uliachaje kukanyagwa-kanyagwa na Mataifa kwa sababu ya ile Vita ya Siku Sita ya mwaka wa 1967? (b) Ijapokuwa Yerusalemu ulikuwa katika cheo cha kuwa huru tangu mwaka wa 1967, kwa sababu gani tunaona kuna jambo fulani lenye kukosekana?

5 Kwa hiyo Yerusalemu wa kidunia uliendelea kukanyagwa-kanyagwa na Mataifa mpaka mwaka wa 1967. Lakini tangu wakati huo, kwa kuonekana kijuu-juu Yerusalemu umekoma kukanyagwa-kanyagwa na Mataifa. Lakini, tunajisikia tukilazimika kuuliza, “Halafu?” Je! hatua ya Israeli ya kukomesha Mataifa yasiukanyage-kanyage Yerusalemu huko nyuma katika mwaka wa 1967 ililetea wanadamu wote baraka? Mataifa mengi yanaona uchungu juu ya kuwako kwa taifa la Israeli, badala ya kuikubali hatua iliyochukuliwa nalo kuwa baraka. Kwa uhakika kufanyizwa kwa taifa la kisasa la Israeli hakukuanzisha Ufalme wa Masihi wa Kiyahudi. Ni jambo la wazi kwamba taifa la Israeli halimtegemei Mungu wa Abrahamu, Isaka na Yakobo, yaani, Yehova, ili kupata msaada na wokovu. Serikali ya taifa hilo si ufalme ulio na mzao wa kweli wa ukoo wa kifalme wa Mfalme Daudi wa kale mwenye kukalia kiti cha kifalme huko Yerusalemu.

6. Tunalazimika kukubali nini juu ya cheo cha Yerusalemu wa kidunia tangu mwaka wa 1967 na juu ya unabii wa Isaya 2:1-4?

6 Kwa hiyo, kwa habari ya Yerusalemu wa kidunia tangu mwaka wa 1967, sisi hatuyaoni maneno ya unabii wa Isaya 2:2-4 yakiwa yametimizwa:

“Na itakuja kuwa katika ule mwisho wa siku, mlima wa nyumba ya Bwana utasimamishwa ukiwa ndio kilele cha milima, nao utainuliwa juu ya vilima; na mataifa yote [goyimu] yatamiminika kuuelekea. Na makundi mengi ya watu yataenda na kusema: ‘Njoni enyi, acheni twende juu kwenye mlima wa Bwana, kwenye nyumba ya Mungu wa Yakobo; na Yeye atatufundisha juu ya njia Zake, na sisi tutatembea katika vijia Vyake.’ Kwa maana kutoka Saioni itatokeza sheria, na neno la Bwana kutoka Yerusalemu. Na Yeye atahukumu kati ya mataifa [goyimu], na ataamua kwa ajili ya makundi mengi ya watu; nao watafua panga zao ziwe majembe ya kukokotwa katika ukUlima, na mikuki yao iwe miundu; taifa [goyi] halitainua upanga dhidi ya taifa [goyi], wala wao hawatajifunza vita tena.”​—JP.

7. Leo sisi tunaona nini tofauti kabisa na unabii wa Isaya 2:1-4, na namna gani juu ya ule unabii wa Zekaria 8:23?

7 Badala ya kufua silaha za vita ziwe vyombo vya amani, mataifa yasiyo ya Kiyahudi yana silaha nyingi sana za vita wakati wa sasa kuliko wakati mwingineo wote uliotangulia, na ni hali moja kuhusu ile Jamhuri ya Israeli yenyewe. Zaidi ya hilo, sisi hatuoni leo unabii wa Zekaria 8:23 ukiendelea kutimizwa, yaani:

“Hivi asema Bwana wa vikosi: Katika siku hizo itakuja kuwa, kwamba watu kumi watashika, kutoka lugha zote za mataifa, naam watalishika rinda la huyo aliye Myahudi, wakisema: Sisi tutakwenda na wewe, kwa maana sisi tumesikia kwamba Mungu yu pamoja na wewe.”​—JP. Angalia pia tafsiri ya Douay Version na JB.

8. Habari yote iliyotangulia inatia shaka juu ya jambo gani kuhusiana na tarehe ya 1967?

8 Habari yote iliyotangulia inatokeza shaka juu ya usahihi wa tarehe ya ule mwaka wa 1967, ule mwaka wa Vita ya Siku Sita, kuwa ndiyo wakati unabii huu ulipotimizwa: “Yerusalemu utakanyagwa kanyagwa na Mataifa, mpaka nyakati za Mataifa ziwe zimetimizwa.” (Luka 21:24 The New American Bible; AV) Kwa kweli “nyakati za Mataifa” zilikwisha mapema kabla ya tarehe hiyo. Acheni tuuchunguze ushuhuda wenye kuonyesha hivyo.

9. (a) Wakati Yesu aliposema, “Yerusalemu utakanyagwa-kanyagwa,” alimaanisha “Yerusalemu” gani, na ni nini kilichowakilishwa na “Yerusalemu” huo? (b) Ni nini kitakachotukia kwa upatani wakati kukanyagwa-kanyagwa kwa “Yerusalemu” kutakapokuwa kumekamilika?

9 Katika kutaja juu ya kukanyagwa-kanyagwa kwa “Yerusalemu” na Mataifa, Yesu alikuwa na wazo la vile Yerusalemu wa kidunia ulivyokuwa kabla haujaanza kukanyagwa-kanyagwa na Mataifa. Yeye mwenyewe alikuwa amesema hivi kitambo kidogo kabla ya hapo: “Usiape kabisa; hata kwa mbingu, kwa maana ndicho kiti cha enzi cha Mungu . . . wala kwa Yerusalemu, kwa maana ndio mji wa Mfalme mkuu.” (Mathayo 5:34, 35) Kwa hiyo, wakati Mataifa yalipoanza kuukanyaga-kanyaga Yerusalemu kwa kuutawala ulimwengu, yalikuwa yakiukanyaga-kanyaga Ufalme wa Mungu uliowakilishwa na ule mji wa kifalme, Yerusalemu. Basi, kwa njia yenye upatani, wakati kilichowakilishwa na Yerusalemu kilipokwisha kukanyagwa-kanyagwa kwa ukamili kwenye umalizio wa Nyakati za Mataifa, Ufalme wa Mungu ulisimamishwa tena ukiwa mikononi mwa mzao wa kifalme wa Mfalme Daudi, yule Masihi.

10. (a) Ni maneno gani katika Ezekieli aliyoambiwa mfalme wa mwisho wa ukoo wa Daudi? (b) Ni nani aliyethibitika kuwa ndiye mwenye “haki” ya kutawala, na Mungu alimfanyia nini?

10 Katika habari hiyo unabii wa Ezekieli 21:25-27, uliotolewa ukielekezwa kwa mfalme wa mwisho wa mji huo aliyekuwa wa ukoo wa Daudi, ulisema hivi: “Na wewe, Ewe mtu mwovu, uliyetiwa jeraha kiasi cha kukuua, mkuu wa Israeli, ambaye siku yako imekuja, katika wakati wa uovu wa mwisho; Bwana [Yehova] asema hivi; Kiondoe kilemba, ivue taji; haya hayatakuwa tena kama yalivyo; kikweze kilicho chini, kakishushe kilichoinuka. Nitakupindua, nitakipindua, nitakipindua; hiki nacho hakitakuwa tena, hata atakapokuja yeye ambaye ni haki yake; nami nitampa.” Yule aliyekuwa na “haki” ya kutawala hakuwa mwingine ila Yesu Kristo, yule Mzao wa Mfalme Daudi. Huko nyuma katika mwaka wa 33 W.K. walikuwako Wayahudi zaidi ya 500 ambao walipata kuwa mashahidi wenye kujionea uhakika wa kwamba Huyo alikuwa amefufuliwa na Mungu siku ya tatu ya kifo chake cha kufia imani.​—1 Wakorintho 15:3-20.

Masihi Azinyenyekea Nyakati za Mataifa

11. Kwa sababu gani Yesu hakujaribu kujifanya mwenyewe mfalme huko Yerusalemu, na kwa hiyo yeye alimwambia nini yule gavana, Pontio Pilato?

11 Yesu yule masihi hakujaribu kujiketisha mwenyewe kuwa Mfalme kwenye Yerusalemu wa kidunia wala kabla wala baada ya kufufuliwa kwake kutoka kwa wafu. Yeye hakufanya jitihada yo yote ya kumpindua Pontio Pilato, aliyekuwa wakati huo gavana Mroma wa Yuda na Yerusalemu. Sababu moja ya kutokufanya hivyo ilikuwa kwamba “nyakati za Mataifa,” ambazo Yesu alizinena kwenye Luka 21:24 (JP), zilikuwa tayari zikiendelea wakati huo. Kwa hiyo yeye aliunyenyekea mpango huo wa kimungu. Kupatana na hilo, yeye alimwambia Pilato: “Ufalme wangu si sehemu ya ulimwengu huu. Kama ufalme wangu ungalikuwa sehemu ya ulimwengu huu, wahudumu wangu wangalikuwa wamepiga vita kwamba nisitolewe nipewe kwa Wayahudi. Lakini, kama ilivyo, ufalme wangu si wa kutoka chanzo hiki.”​—Yohana 18:36, NW.

12. Kwa kuwa alikuwa mwanafunzi mwenye kuchunguza Maandiko ya Kiebrania, Yesu alijua kwamba Nyakati za Mataifa zilianza lini na kwa tukio gani, na kwa hiyo sasa ni ulizo gani linalotokea juu ya “nyakati” hizo?

12 Kwa kuwa Yesu Masihi alikuwa mwanafunzi mwenye kuchunguza Maandiko ya Kiebrania yaliyoongozwa na Mungu, yeye alijua kwamba Nyakati za Mataifa zilikuwa zimeanza kabla Waroma hawajaja kukaa Yerusalemu na kusimamisha magavana wao huko. Alijua kwamba zilikuwa zimeanza wakati Yerusalemu ulipofyekwa kwa mara ya kwanza katika mwaka wa 607 kabla ya Wakati wa Kawaida wetu. Mungu alitumia Nebukadreza Mfalme Mtaifa wa Babuloni, aliyemwita ‘mtumishi Wangu,’ ili kupindua Yerusalemu na Yuda. (Yeremia 43:10) Ulimwengu uliendelea kutawalwa na Mataifa kupita siku za Yesu Masihi na moja kwa moja mpaka wakati uliowekwa na Mungu wa Nyakati za Mataifa kumalizika. Ufalme wa Masihi ambao haungekuwa “sehemu ya ulimwengu” ulipaswa kungoja mpaka wakati huo. Kwa hiyo, ikihesabiwa kuanzia mwaka wa 607 K.W.K., utawala wa Mataifa ungeendelea muda wa “nyakati” ngapi?

13. Mungu alitumia njia gani kuonyesha mfalme wa Babuloni hesabu ya “nyakati” hizo, na matokeo ya kufanya hivyo yalikuwa nini juu ya mfalme huyo?

13 Yehova Mungu alionyesha zingekuwa nyakati ngapi katika ndoto aliyopelekea Nebukadreza, ambaye alikuwa amemtumia kuwa “mtumishi” Wake. Ingawa Nebukadreza alikuwa ametumiwa kuuharibu “mji wa Mfalme mkuu,” Yerusalemu, bado yeye alilazimika kumkiri Yehova kuwa “Yeye aliye juu” na “Mfalme wa mbinguni” kwa sababu ya ndoto hiyo kutimizwa juu yake. (Mathayo 5:35; Danieli 4:34, 37) Tangu wakati wa huyo “mtumishi” wake, Mungu Aliye Juu Zaidi, aliye pia Mfalme wa mbingu, alianzisha zile “nyakati za Mataifa” katika mwaka wa 607 K.W.K.

14. Kwa sababu ya mambo yaliyotokezwa na vita katika Mashariki ya Kati mwaka wa 1917, ni mitajo gani iliyosemwa na viongozi wa kidini wanane katika Taarifa waliyoitoa wakiwa London?

14 Jambo la kupendeza ni kwamba, kuelekea mwisho wa mwaka wa 1917, mwaka ambao Yerusalemu wa kisasa uliojengwa upya ulitekwa na askari wa Uingereza wakati wa Vita ya Ulimwengu ya Kwanza, wanane kati ya viongozi wa kidini wa Uingereza walio mashuhuri zaidi walikutana huko London, Uingereza, kisha wakatoa Taarifa yenye mitajo saba ya wazi-wazi. Inayofuata ni mingine kati ya hiyo:

“WA KWANZA. Kwamba hali ya hatari iliyopo sasa inaelekeza kwenye mwisho wa nyakati za Mataifa. . . .

“WA NNE. Kwamba taifa la Israeli litarudishwa katika nchi yalo lenyewe likiwa katika hali ya kutokuamini, na baadaye ligeuzwe katika imani Kristo akitokea ili kulisaidia.

“WA TANO. Kwamba mipango yote ya kibinadamu ya kurekebisha mambo yarudie hali ya kawaida ni lazima iwe chini ya kuja kwa pili kwa Bwana wetu, kwa sababu mataifa yote yatatiishwa chini ya utawala wake. . . .

“WA SABA. Kwamba zile kweli zilizotiwa katika taarifa hii ni zenye mafaa makubwa kupita mambo yote katika kuamua tabia na matendo yanayopasa kufuatwa na Wakristo kuhusiana na matatizo ya sasa yanayoleta mkazo mwingi.”

15. (a) Katika ndoto ya Nebukadreza, ni nini kilichofananishwa na ule mti wenye kupanuka sana? (b) Wakati wa uwazimu wa Nebukadreza, utawala wa ulimwengu wenye kusimamiwa na Milki ya Babuloni ulikuwa namna gani? (c) Utawala wa ulimwengu uliendelezwaje baada ya Babuloni kukoma kuwa milki ya ulimwengu?

15 Katika ile ndoto ambayo Yehova Mungu alimpelekea “mtumishi” wake, yaani Mfalme Nebukadreza, ni “nyakati saba” zilizoamriwa na mbingu ziwepo. Hizo zinashikanaje au zinalinganaje na “nyakati za Mataifa”? Kwa njia hii: Katika ile ndoto ya kiunabii, ule mti wenye urefu mkubwa kwenda juu na wenye kupanuka sana unafananisha utawala wa ulimwengu mzima kwa njia ya kutokuonekana. Kwa kuwa wakati wa kutolewa kwa ndoto hiyo Nebukadreza, yule “mtumishi” wa Yehova Mungu, alikuwa akitawala huo ulimwengu, mti huo unashirikishwa naye kibinafsi, na kwa hiyo unaweza kusemwa unamfananisha yeye. Lakini je! utawala wake wa ulimwengu ulikatwa ukaangushwa alipoenda uwazimu akawa hakikalii kiti cha ufalme wenye makoloni mengi? Je! Milki ya Babuloni iliacha kutawala ulimwengu? Hapana, bali iliendelea kuutawala mpaka Nebukadreza akarudishwa kwenye kiti chake na hata ikazidi kuwako muda wote wa zile tawala za warithi wake, Evil-Merodaki, Nabonido na Belshaza. Baada ya hapo, Mataifa yaliendelea kutawala ulimwengu hata muda wa zile serikali za ulimwengu zenye kufuatana, Uajemi Wenye Makoloni, Ugiriki Wenye Makoloni, Roma Yenye Makoloni, pamoja na chipukizi lililotokana nayo, yaani serikali kuu ya ulimwengu ya mwungano wa Waingereza na Waamerika.

16. Kwa kweli ni utawala wa ulimwengu wa nani 1 uliokatwa ukaangushwa chini wakati wa mfuatano I wote huo wa serikali kuu za ulimwengu za Mataifa, na ! ni “nyakati” ngapi zingepita juu ya kisiki cha ule mti j wa mfano?

16 Wakati wote wa muda huo mrefu, ni utawala wa nani wa ulimwengu, hasa ukiwa unawakilishwa na Yerusalemu “mji wa Mfalme mkuu,” uliokatwa kweli ukaangushwa chini na kulala kifudifudi? Ni ule wa Yule ambaye Nebukadreza alimwita “Yeye aliye juu” na “Mfalme wa mbinguni,” Yehova. Kisiki cha mti, pamoja; na vifungo vya chuma na shaba, kilionyesha kwamba utawala Wake wa ulimwengu ungekomeshwa kwa muda fulani. “Nya kati saba” ziliamriwa na Yehova Mungu zipite juu ya kisiki hicho cha mfano.

17. (a) Badala ya kusema “nyakati saba,” hesabu I kadha ya watafsiri wanafasirije maneno hayo ya Kiebrania? (b) Ni kwa njia gani ingeweza kuwa kwamba Yerusalemu uliendelea kukanyagwa-kanyagwa na Mataifa hata baada ya mji huo kujengwa tena?

17 Maneno “miaka saba” yanatumiwa badala ya “nyakati saba” na tafsiri za The Living Bible, Moffatt, Today’s English Version, na An American Translation, Uwazimu wa Nebukadreza, ambao labda ulikuwa ni ile hali ya mtu kujifikiria amekuwa mnyama inayoitwa likanthropi, ulimpata muda wa miaka saba. Alipopona alimkiri Mungu aliyemponya, lakini yeye hakuwarudisha watu wa Mungu kwenye nchi ya kwao. Yehova Mungu alikuwa ameamuru Yerusalemu na nchi ya Yuda ikae katika hali ya ukiwa kwa miaka 70. Kwa hiyo Yerusalemu uliendelea kukanyagwa-kanyagwa na Mataifa, hata baada ya Yerusalemu kujengwa tena na Wayahudi waliorudishwa kwao kuanzia mwaka wa 537 K.W.K. Namna gani hivyo? Kwa sababu waliendelea kuwa chini ya usimamizi wa Mataifa, bila ya mzao ye yote wa ukoo wa kifalme wa Daudi kuketi juu ya kiti cha ufalme huko Yerusalemu akiwa mfalme mwenye kujitegemea. Kwa hiyo ni wazi kwamba zile “nyakati saba” ni za j mfano zinapotumiwa kumhusu Yehova I Mungu, na kwa hiyo ni ndefu kuliko miaka I saba zikihesabiwa kuanzia mwaka wa I 607 K.W.K.​—Danieli 4:16, 23, 25, 32.

18. Hizo “nyakati saba” zilikuwa jumla ya muda gani, zikichukuliwa kwa njia ya mfano, na kwa hiyo zilimalizika lini?

18 Katika njia ya kiunabii ya Biblia ya kuhesabu wakati, mwaka unaopimwa urefu kulingana na mizunguko ya mwezi unahesabiwa kuwa wenye siku 360. Kwa hiyo mwaka mmoja wa mfano, au ‘wakati’ mmoja, ungekuwa ni miaka 360. Basi, “nyakati” saba za mfano au “miaka” saba ya mfano, ingekuwa 7 X 360, au miaka 2,520. Ikihesabiwa kuanzia mwaka wa 607 K.W.K., wakati Yerusalemu, “mji wa Mfalme mkuu,” uliharibiwa na “mtumishi” wa Yehova, Nebukadreza, na kwa njia hiyo Yerusalemu ukaanza kukanyagwa-kanyagwa na Mataifa, hiyo miaka 2,520 ingemalizika katika vuli ya mwaka wa 1914 Wakati wa Kawaida wetu.

19. (a) Hapa duniani palitokea nini mwaka wa 1914? (b) Mwaka huo ulikuwa wakati wa “Mfalme wa mbingu” kufanya nini akiwa katika makao yake?

19 Katika mwaka huo Vita ya Ulimwengu ya Kwanza ilitokea kwa ghafula hapa duniani, nayo ilipigwa ili kung’ang’ania suala la anayepaswa kuutawala ulimwengu. Lakini, huko juu katika makao ya “Mfalme wa mbingu,” wakati wake ulikuwa umefika wa kuonyesha kwamba “Aliye Juu Zaidi atawala katika ufalme wa wanadamu, naye humpa mtu awaye yote amtakaye.” (Danieli 4:22, 29, JP) Sasa ulikuwa umefika wakati wa “yeye ambaye ni haki yake” na wa Yeye Aliye Juu Zaidi ‘kumpa.’ (Ezekieli 21:30-32; 21:25-27) Huyo alikuwa ndiye Masihi aliyetukuzwa, yule ambaye Mfalme wa mbingu alimzaa awe Mwana wake wa kiroho, yaani, Yesu Kristo, aliyefufuliwa akapata uzima mbinguni. (Zaburi 2:1-7) Huo ulikuwa ndio wakati wa Mfalme wa mbingu kumwambia hivi: “Nenda uwe ukishinda katikati ya adui zako.” (Zaburi 110:1, 2, NW) Kwa uhakika jambo hilo lilimaanisha kwamba kweli “nyakati za Mataifa” zilikuwa zimekwisha.

[Maelezo ya Chini]

a Katika Mwanzo 14:1, angalia maneno ya cheo yanayosema “Tidali mfalme wa Goimu.” (The Holy Scriptures [1952], The Jewish Publication Society of America) Biblia ya Authorized Version inayatafsiri hivi: “Tidali mfalme wa mataifa.” Ili kuona matumizi ya neno Goimu, ona pia Mwanzo 14:9, Union Version; Yoshua 12:23, NW. Angalia pia The Jerusalem Bible.

Wewe Unaweza Kujibu?

◻ Ni kitu gani kilichoonekana kama kimekoma wakati Yerusalemu wa kidunia ulipotekwa na Wayahudi mwaka wa 1967, lakini je! tukio hilo lilimaliza ‘kukanyagwa-kanyagwa’kwa “Yerusalemu”na Mataifa?

◻ “Nyakati za Mataifa” zilianza lini, na kwa tukio gani?

◻ Inathibitishwaje kwamba Nyakati za Mataifa zingeendelea kwa miaka 2,520, au mpaka mwaka wa 1914 W.K.?

◻ Ni nini kinachofananishwa na ule mti wenye kupanuka sana unaotajwa na unabii wa Danieli, na ni nini maana ya kukatwa kisha kuchipuka tena kwa mti huo?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki