Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w84 10/15 kur. 3-4
  • 1914 Ni Historia Tu? Au Una Matokeo Juu Yako?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • 1914 Ni Historia Tu? Au Una Matokeo Juu Yako?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1984
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Kizazi Kilichotiwa Alama
  • 1914—Kizazi Ambacho Hakitapita
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1984
  • Ufalme wa Mungu Huanza Kutawala Katikati ya Adui Zake
    Kweli Iongozayo Kwenye Uzima wa Milele
  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1997
  • Ambayo 1914 Ungemaanisha Kwako Wewe
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1984
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1984
w84 10/15 kur. 3-4

1914 Ni Historia Tu? Au Una Matokeo Juu Yako?

“KATIKA mji wa Kibosnia wa Sarajevo asubuhi ya Juni 28, 1914, dereva aliyeajiriwa alielewa vibaya maagizo aliyopewa, akapiga kona mahali asipopaswa, . . . na kwa kufanya hivyo akawapeleka abiria wake mahali ambapo muuaji aliyekuwa akingojea hakuwa na haja ya kulenga ili kuwapiga risasi.

“Mitupo miwili ya risasi kutoka bunduki moja ikatetemesha ulimwengu. Uhalifu huo ulikuwa kajambo kadogo ambako, kalitokeza, kakaleta mambo makubwa sana. Kukafuata miaka minne ya jeuri ya ulimwengu wote. Mamilioni wakafa ghafula.”​—Kitabu The American Heritage History of World War I.

Kuuawa kwa Mtawala Mkuu Francis Ferdinand wa Austria pamoja na mkeye, Sofia, kulichochea matukio ambayo yameutia alama mwaka wa 1914 kuwa mahali penye kuleta badiliko katika historia ya wanadamu. Na matukio hayo yamekuwa na matokeo juu yako. Kwa sababu gani? Kwa sababu “mambo makubwa sana” hayo yakawa ni ile Vita Kuu ya 1914-18. Tangu wakati huo vita na jeuri havijakoma kamwe.

Kizazi Kilichotiwa Alama

Kuhusu umaana wa Vita ya Ulimwengu ya Kwanza, mbuni wa vitabu Mwingereza J. B. Priestley aliandika hivi: “Kama ulizaliwa mwaka 1894, kama mimi, ghafula uliona mwatuko mkubwa uliochongoka kwenye kioo. Baada ya hapo akili yako ikawa na wazo la ulimwengu uliokwisha mwaka 1914 na mwingine ukaanza mwaka 1919 hivi, na jangwa lenye moshi na mchafuko mkubwa . . . ukiwa katikati.”

Waokokaji wa “kizazi kilichotolewa dhabihu” hicho cha 1914, kama ambavyo kimeitwa,a wamepitia nyakati zenye maana kubwa ambazo zilianza na mahandaki na mizinga yenye kutupa makombora madogo na ambazo zinafikia kwenye upeo wa mizinga yenye makombora yanayoruka kutoka bara moja mpaka bara jingine. Nayo ina uwezo wa kutokeza maangamizi ya ulimwengu. “Maendeleo” hayo yanapatana na maneno ya kiunabii ya Yesu Kristo: “Taifa litaondoka kupigana na taifa, na ufalme kupigana na ufalme; . . . na katika nchi dhiki ya mataifa wakishangaa kwa uvumi wa bahari na msukosuko wake; watu wakivunjika mioyo kwa hofu, na kwa kutazamia mambo yatakayoupata ulimwengu. Kwa kuwa nguvu za mbinguni zitatikisika.”​—Luka 21:10, 25, 26.

Maneno hayo ya Yesu ni sehemu ya ishara yenye sehemu nyingi ambayo inatia alama “mwisho wa ulimwengu huu.” Kama ambavyo imeonyeshwa mara nyingi katika gazeti hili, tangu 1914 unabii huu umekuwa ukitimizwa kwa kadiri kubwa. Lakini Yesu aliongeza jambo lenye maana sana kuhusu kizazi cha 1914. Ni jambo gani? Yeye alisema: “Mwonapo hayo yanaanza kutokea, tambueni ya kwamba ufalme wa Mungu u karibu. Amin, nawaambieni, Kizazi hiki hakitapita hata hayo yote yatimie.”​—Mathayo 24:3 Phillips; Luka 21:29-32.

Maneno hayo yanatimiaje kwa kizazi cha 1914 kinachoendelea kuisha haraka? Ni matukio gani yanayongojewa? Nayo yatakuwa na matokeo gani juu yako wewe?

[Maelezo ya Chini]

a Robert Wohl, katika kitabu The Generation of 1914.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki