Mnara wa Mlinzi Unaanza Kuchapwa Wakati Mmoja na Kiingereza Katika Lugha Nyingi
Katika Julai 1879 toleo la kwanza la gazeti hili lilisema: “Kama jina lalo linavyoonyesha, lina lengo la kuangalia lione ni kutoka wapi mambo ya kupendeza na ya faida yanaweza kutangaziwa ‘kundi dogo.’” Leo, Mnara wa Mlinzi linapakua chakula cha kiroho pia kwa “mkutano mkubwa” wa watu wanyofu ambao wanatazamia kupata uzima wa milele hapa duniani.—Luka 12:32; Ufunuo 7:9-17.
Mwenezo wa Mnara wa Mlinzi ulivyoongezeka ndivyo hesabu ya lugha ambazo linatokea ilivyoongezeka. Leo, lugha hizo zinajumlika kuwa 102. Ripoti zinaonyesha kwamba maandikisho mapya ya Mnara wa Mlinzi na gazeti-jenzi lake, Amkeni!, yameongezeka kwa kutokeza sana wakati wa miaka zaidi ya 70 iliyopita. Uangushaji wa nakala moja moja shambani umeongezeka pia. Hizi ni baadhi ya tarakimu zinazopatikana:
Mwaka Maandikisho Mpya Magazeti Yaliyoangushwa
1914 2,746 95,973
1944 292,258 9,293,913
1964 1,551,436 127,055,165
1984 1,812,221 287,358,064
Sasa tumefikia hatua nyingine kubwa katika mwaka wa 105 wa historia ya Mnara wa Mlinzi—ni kuchapwa wakati mmoja na Kiingereza katika lugha zaidi ya 20. Hilo ni tukio lenye furaha kama nini! Yehova na aendelee kutumia gazeti hili kwa njia kubwa zaidi katika kutangaza Ufalme wake kupitia Kristo Yesu!
[Picha katika ukurasa wa 8]
Swedish
Danish
Norwegian
Finnish
Portuguese
German
Sepedi
Sesotho
Tsonga
Zulu
Dutch
French
Spanish
Italian
Afrikaans
Japanese
Tswana
Venda
Xhosa
Cibemba