Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • jv kur. 724-725
  • Kutangaza Mnara wa Mlinzi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutangaza Mnara wa Mlinzi
  • Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
  • Habari Zinazolingana
  • Kukesha Kwa Miaka 100 Moja
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1979
  • Amkeni!—Gazeti Linalovutia Sana Umma
    Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
  • Biblia Zaidi na Vitabu vya Kusaidia Kujifunza Biblia
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1975
  • ‘Juu ya Mnara wa Ulinzi Mimi Ninasimama’
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1987
Pata Habari Zaidi
Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
jv kur. 724-725

Kutangaza Mnara wa Mlinzi

Lilipotokezwa kwa mara ya kwanza, katika Julai 1879, liliitwa Zion’s Watch Tower and Herald of Christ’s Presence. Gazeti hili, lililokuwa mtetezi wa dhabihu ya fidia ya Yesu Kristo, lilichapwa ili kuandaa chakula cha kiroho kwa nyumba ya imani. Ili kukaza fikira kwa udhahiri zaidi juu ya kusudi la gazeti hili, Januari 1, 1909, kichwa chalo kilibadilishwa kuwa The Watch Tower and Herald of Christ’s Presence. Kuanzia Januari 1, 1939, huku likiweka mkazo zaidi juu ya uhakika wa kwamba Kristo alikuwa tayari anatawala kutoka mbinguni akiwa Mfalme, kichwa kilibadilishwa kusomeka The Watchtower and Herald of Christ’s Kingdom. Kisha mnamo Machi 1, 1939, kwa kubadilisha kichwa kuwa The Watchtower Announcing Jehovah’s Kingdom, fikira zilielekezwa kihususa zaidi kwa Yehova akiwa Mwenye Enzi Kuu wa Ulimwengu Wote Mzima, yule aliyempa Mwanae mamlaka ya kutawala.

Lilipotangazwa kwa mara ya kwanza, Watch Tower lilikuwa kichapo cha kurasa nane, kikitokezwa mara moja kwa mwezi. Ukubwa walo uliongezwa hadi kurasa 16 katika 1891, na likawa gazeti la kutokezwa mara mbili kila mwezi katika 1892. Mpangilio wa kurasa 32 ulianzishwa katika lugha nyingi katika 1950.

Kutafsiriwa kwa Watch Tower katika lugha nyinginezo kulianza polepole. Toleo moja la kielelezo lilichapwa katika Kisweden katika 1883 ili litumiwe kuwa trakti. Kuanzia 1886 hadi 1889, chapa ndogo ya gazeti hili ilichapwa katika Kijerumani. Lakini haikuwa hadi 1897 kwamba Watch Tower lilitokea tena katika Kijerumani na likaendelea kutangazwa bila kukoma. Kufikia 1916 lilikuwa likichapwa katika lugha saba—Kidenmark-Kinorway, Kifaransa, Kifinland, Kiingereza, Kijerumani, Kipoland, na Kisweden. Wakati kuhubiriwa kwa habari njema kulipoongeza mwendo zaidi katika 1922, hesabu ya lugha ambazo gazeti hilo lilitangazwa iliongezwa kuwa 16. Hata hivyo, kufikia 1993, lilikuwa likitokezwa kwa ukawaida katika lugha 112—zile zinazotumiwa na sehemu kubwa ya idadi ya watu duniani. Hiyo ilitia ndani si lugha kama vile Kiingereza, Kihispania, na Kijapani tu, ambazo kwazo mamilioni ya nakala za kila toleo zilichapwa, bali pia Kipalau, Kituvalu, na nyinginezo ambazo ni mia chache zilizokuwa zikigawanywa.

Kwa miaka mingi Mnara wa Mlinzi lilionwa kuwa gazeti hasa la “kundi dogo” la Wakristo waliojitakasa. Hesabu ya nakala zilizotokezwa ilikuwa ndogo; kufikia 1916 ni nakala 45,000 tu zilizokuwa zikichapwa. Lakini kuanzia 1935, mkazo wa mara kwa mara uliwekwa juu ya kuwatia moyo “Wayonadabu,” au “umati mkubwa,” wapate na kusoma Mnara wa Mlinzi kwa ukawaida. Katika 1939, wakati jalada la gazeti hilo lilipoanza kukazia Ufalme, maandikisho ya Mnara wa Mlinzi yalitolewa kwa umma wakati wa kampeni ya uandikishaji ya kimataifa ya miezi minne. Kama tokeo, orodha ya maandikisho ilipanda ikawa 120,000. Mwaka uliofuata, Mnara wa Mlinzi lilikuwa likitolewa kwa watu barabarani kwa ukawaida. Hesabu ya nakala zilizotokezwa iliongezeka upesi. Kufikia mapema 1993 uchapaji wa kila toleo ulikuwa 16,400,000.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki