Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w86 4/1 kur. 8-9
  • Sababu Iliyomfanya Yesu Aje Duniani

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Sababu Iliyomfanya Yesu Aje Duniani
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
  • Habari Zinazolingana
  • Sababu Iliyomfanya Yesu Aje Duniani
    Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
  • Apanua Huduma Yake Huko Galilaya
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
  • Miujiza Ambayo Yesu Alifanya Katika Mji Alimokaa
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1977
  • Bidii kwa Ajili ya Ibada ya Yehova
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1985
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
w86 4/1 kur. 8-9

Maisha na Huduma ya Yesu

Sababu Iliyomfanya Yesu Aje Duniani

KAMA tulivyojifunza katika toleo lililotangulia la gazeti hili, siku ambayo Yesu alikaa Kapernaumu akiwa na wanafunzi wake wanne ilikuwa yenye shughuli nyingi. Kwanza, yeye alimponya katika sinagogi mwanamume yule aliyekuwa amepagawa na mashetani, halafu nyumbani kwa Petro akamponya mama mkwe wa Petro, na mwishowe jioni watu wa Kapernaumu wakamletea wagonjwa wao wote ili waponywe. Hakuwa na wakati wa faragha.

Sasa ni asubuhi na mapema kesho yake. Kunapokuwa kungali na giza, Yesu anainuka na kwenda nje akiwa peke yake. Anaenda mahali anapokuwa peke yake aweze kupelekea Babaye sala kwa faragha. Lakini faragha ya Yesu ni ya muda mfupi kwa sababu wakati Petro na wengine wanapotambua kwamba yeye hayupo wanaenda nje wakamtafute.

Wanapompata Yesu, Petro anasema “Watu wote wanakutafuta.” Watu wa Kapernaumu wanataka Yesu akae pamoja nao. Wanathamini mambo ambayo amewafanyia! Lakini je, Yesu alikuja duniani afanye maponyo ya kimuujiza hasa? Yeye anasema nini?

Kulingana na usimulizi mmoja wa Biblia, Yesu anawajibu wanafunzi wake hivyo: “Twendeni mahali pengine, mpaka vijiji vilivyo karibu, nipate kuhubiri huko nao, maana kwa hiyo nalitokea.” Ingawa watu wanamhimiza Yesu akae nao, yeye anawaambia: “Kwenye miji mingine pia lazima mimi nizitangaze habari njema ufalme wa Mungu, kwa sababu kwa ajili ya jambo hilo mimi nilitumwa.”

Ndiyo, Yesu alikuja duniani kwa kusudi hasa la kuhubiri juu ya Ufalme wa Mungu utakaoondoa malaumu juu ya jina la Babaye kisha uondoe daima mabaya yote yanayopata wanadamu. Lakini, ili atoe ushuhuda wa kwamba ametumwa na Mungu, Yesu anafanya maponyo ya kimuujiza. Musa pia alitumia njia iyo hiyo ya kufanya miujiza karne nyingi zilizopita ili athibitishe haki zake za kuwa mtumishi wa Mungu.

Sasa, wakati Yesu anapoondoka Kapernaumu akaihubiri miji mingine, wanafunzi wake wanne wanaenda pamoja naye. Hao wanne ni Petro na Andrea nduguye, na Yohana na Yakobo nduguye. Utakumbuka kwamba, juma tu lililotangulia wao walikaribishwa wawe wafanya kazi wenzi wa Yesu wenye kusafiri naye.

Ziara ya Yesu ya kuhubiri katika Galilaya pamoja na wanafunzi wake wanne inapata mafanikio makubwa! Kwa kweli, ripoti juu ya utendaji wake inaenea hata katika Shamu yote. Makutano makubwa kutoka Galilaya, Yudea, na ng’ambo ya Yordani wanafuata Yesu na wanafunzi wake. Marko 1:35-39; Luka 4:42, 43; Mathayo 4:23-25; Kutoka 4:1-9, 30, 31.

◆ Ni jambo gani linalotokea asubuhi inayoifuata siku ile ambayo Yesu anakuwa na shughuli nyingi katika Kapernaumu?

◆ Kwa sababu gani Yesu alitumwa duniani, na miujiza yake ilikuwa ya kusudi gani?

◆ Ni nani aliyeenda pamoja na Yesu katika ziara ya kuhubiri katika Galilaya, na utendaji wa Yesu uliitikiwaje?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki