Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w87 5/15 kur. 8-9
  • Mmoja Asiyeelekea Kuwa Mwanafunzi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mmoja Asiyeelekea Kuwa Mwanafunzi
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1987
  • Habari Zinazolingana
  • Mmoja Asiyeelekea Kuwa Mwanafunzi
    Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
  • Ana Nguvu Kuliko Roho Wengi Waovu
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
  • Yesu Ana Nguvu Kuliko Roho Waovu
    Jifunze Kutoka kwa Mwalimu Mkuu
  • Je, Roho Waovu Ni Halisi?
    Amkeni!—1998
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1987
w87 5/15 kur. 8-9

Maisha na Huduma ya Yesu

Mmoja Asiyeelekea Kuwa Mwanafunzi

Nl JAMBO lenye kuogopesha kama nini analoona Yesu anapokanyaga pwani! Wanaume wawili wakali isivyo kawaida wanatoka makaburini yaliyo karibu na kukimbia kuelekea kwake. Wamepagawa na mashetani. Kwa kuwa inaelekea mmoja ni mjeuri zaidi na ametaabika kwa muda mrefu zaidi chini ya utawala wa shetani kuliko yule mwingine, anakuwa wa kukaziwa fikira zaidi.

Kwa muda mrefu mwanamume huyo amekuwa akiishi akiwa huko makaburini. Sikuzote, mchana na usiku, yeye hupaaza sauti na kujikata-kata kwa mawe. Yeye ni mjeuri sana hivi kwamba hakuna mtu aliye na ujasiri wa kupitia njia hiyo. Majaribio yamefanywa ya kumfunga, lakini yeye hukata minyororo na kuvunja vyuma na kuviondoa kwenye miguu yake. Hakuna mtu aliye na nguvu za kumtiisha.

Mwanamume huyo amkaribia Yesu na kuanguka miguuni pake, wale mashetani waliomtawala wanapaaza sauti hivi: “Tuna nini nawe, Yesu, Mwana wa Mungu Aliye Juu? Na kuapisha kwa Mungu usitutese.”

“Ewe pepo mchafu, mtoke mtu huyo,” Yesu anaendelea kusema. Lakini ndipo Yesu anauliza: “Jina lako nani?”

“Jina langu ni Legioni, kwa kuwa tu wengi,” ndilo jibu. Mashetani wanaterema kwa kuona mateso ya wale wanaoweza kupagaa, kwa wazi wakifurahia kuwavamia wakiwa kundi lenye roho ya woga. Lakini wakikabiliwa na Yesu, wanasihi wasipelekwe katika lile shimo refu. Tunaona tena uwezo mkubwa alio nao Yesu wa kushinda hata mashetani wakali mno. Hilo pia linafunua kwamba mashetani wanajua kwamba kutupwa kwao katika shimo refu pamoja na kiongozi wao, Shetani Ibilisi, ndiyo hukumu ya Yehova kwao hatimaye.

Kundi la nguruwe karibu 2,000 linajilisha karibu mlimani. Kwa hiyo wale mashetani wanasema: “Tupeleke katika nguruwe, tupate kuwaingia wao.” Kwa wazi mashetani wanapata namna fulani ya furaha yenye ukatili mwingi isiyo ya kiasili, katika kuingia miili ya viumbe wenye nyama. Yesu anapowaruhusu kuwaingia nguruwe hao, nguruwe wote 2,000 ghafula wanateremka kasi gengeni na kufa maji katika bahari.

Wakati wale wanaochunga nguruwe hao wanapoona hilo, wanaenda mbio kuripoti habari hizo katika mji na nchi iliyokuwa karibu. Kwa hiyo, watu wanakuja kuona ni jambo gani limetokea. Wanapofika, kumbe, yupo hapo yule mwanamume ambaye mashetani walikuwa wamemtoka, akiwa amevalia nguo na akiwa na akili zake timamu, ameketi miguuni pa Yesu!

Mashahidi waliojionea kwa macho yao wenyewe wanaripoti kwa watu jinsi mwanamume huyo alivyokuwa ameponywa. Wanasimulia pia kifo kisicho cha kawaida cha hao nguruwe. Wanaposikia hilo, wanashikwa na woga mwingi sana, nao wanamsihi Yesu kwa bidii aondoke eneo lao. Kwa hiyo yeye anakubali na kuingia merikebuni. Yule ambaye hapo kwanza alikuwa amepagawa na mashetani anamwomba Yesu amruhusu aende pamoja naye. Lakini Yesu anamwambia: “Enenda zako nyumbani kwako, kwa watu wa kwenu, ukawahubiri ni mambo gani makuu aliyokutendea [Yehova], na jinsi alivyokurehemu.”

Kwa kawaida Yesu huwaagiza wale anaowaponya wasimwambie mtu ye yote, kwa kuwa yeye hataki watu wakate maneno kwa msingi wa ripoti zenye kusisimua. Lakini jambo hili lililo tofauti linafaa kwa sababu mtu huyo ambaye hapo kwanza alipagawa na mashetani atakuwa akishuhudia watu ambao labda sasa Yesu hatakuwa na nafasi ya kuwafikia. Zaidi ya hilo, kuwapo kwa mwanamume huyo kutaandaa ushuhuda juu ya uwezo wa Yesu wa kufanya mema, na kupinga ripoti yo yote isiyopendeza ambayo huenda ikaenezwa juu ya hasara ya wale nguruwe.

Kupatana na maagizo ya Yesu, mtu huyo ambaye hapo kwanza alipagawa na mashetani aenda zake. Anaanza kutangaza kote kote katika Dekapoli mambo yote aliyomfanyia Yesu, nao watu wanastaajabu sana. Mathayo 8:28-34; Marko 5:1-20; Luka 8:26-39; Ufunuo 20:1-3.

◆ Ni kwa sababu gani huenda, mtu mmoja mwenye kupagawa na mashetani ndiye anakaziwa fikira hali walikuwapo wawili?

◆ Ni nini linaloonyesha kwamba mashetani wanajua juu ya kutupwa kwao katika shimo refu wakati ujao?

◆ Ni kwa nini, kwa wazi, mashetani wanapenda kuwapagaa binadamu na wanyama?

◆ Ni kwa sababu gani Yesu anafanya tofauti na mtu huyo ambaye hapo kwanza alikuwa amepagawa na mashetani, akimwagiza aende na kuwasimulia wengine juu ya yale ambayo Yeye alimfanyia?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki