Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w87 8/15 kur. 3-4
  • Cheo cha Wanawake Chenye Maendeleo Katika Nyakati za Kisasa

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Cheo cha Wanawake Chenye Maendeleo Katika Nyakati za Kisasa
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1987
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Wanawake Katika Siasa
  • Wanawake Katika Kazi ya Kuajiriwa
  • Katika Elimu, Ufundi, na Dini
  • Matokeo Yamekuwa Nini?
  • ‘Wanawake Wenye Bidii Katika Bwana’
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1991
  • Heshima na Staha Chini ya Utunzaji wa Mungu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2012
  • Cheo cha Wanawake Chenye Maendeleo Je! Ni Baraka Yenye Mchanganyiko?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1987
  • Je, Kweli Mungu Anawajali Wanawake?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2012
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1987
w87 8/15 kur. 3-4

Cheo cha Wanawake Chenye Maendeleo Katika Nyakati za Kisasa

HUKO nyuma katika 1906 Czar Nicholas wa Urusi alipokea ombi kutoka kwa wanawake fulani Warusi wa mashambani ambalo, miongoni mwa mambo mengine, lilisema hivi:

“Kwa vizazi vingi wanawake wa tabaka ya chini wameishi bila kuwa na haki zo zote. . . . Sisi hata hatuonwi kuwa wanadamu, bali punda tu. Tunadai tufunzwe kusoma na kuandika; tunadai binti zetu wapewe vifaa vile vile vya kujifunzia kama wanavyopewa wana wetu. . . . Sisi tunajua kwamba tu wajinga, lakini si sisi wenyewe kulaumika.”

Hali hiyo yenye kuhuzunisha ni tofauti sana na yale maelezo ambayo Biblia inatoa kuhusu mke mwema na mwenye kuheshimiwa, yakimwonyesha kuwa mfano unaostahili kuigwa na kusifiwa. (Mithali 31:10-31) Lakini maelezo hayo kutoka Urusi yanaonyesha ukweli wa maneno yaliyosemwa katika Biblia na mfalme Sulemani mwenye hekima muda mrefu uliopita: “Mwanadamu amemtawala mwanadamu kwa maumivu yake.” (Mhubiri 8:9, NW) Hakika maumivu hayo hayakuwekewa mpaka kwa wanaume. Huenda mstari huo ukachukuliwa katika njia pana zaidi kumaanisha: ‘wanaume wamewatawala wanaume wengine na wanawake kwa maumivu yao.’ Lakini ni badiliko lililoje katika fungu la wanawake, kama hali katika Urusi inavyoonyesha!

Leo, “hesabu kubwa zaidi ya madaktari na walimu wa Urusi ni wanawake. Wanawake wanafanyiza karibu theluthi mbili za hesabu ya ujumla ya wastadi wa uchumi na robo tatu ya wafanya kazi wa kitamaduni. Asilimia 40 ya wale wanaofanya kazi katika mambo ya sayansi ni wanawake . . . Kati ya wanawake elfu moja wanaohusika na uchumi wa kitaifa, 862 wana elimu (kamili au isiyo kamili) ya juu zaidi au ya sekondari.”—Women in the USSR.

Wanawake Katika Siasa

Yale ambayo yamesitawi katika Urusi yamesitawi pia kwa kadiri iliyo kubwa zaidi au ndogo zaidi katika nchi nyingine nyingi. Taifa la kwanza kuwapa wanawake haki ya kupiga kura lilikuwa New Zealand, huko nyuma katika 1893. Kati ya 1917 na 1920, walipewa haki hiyo katika Urusi, Uingereza, United States, na Kanada, lakini Uswisi haikuwapa haki hiyo mpaka 1971, ijapokuwa wanawake wa Uswisi waliruhusiwa kuwa na vyeo vya kisiasa.

Leo wanawake hawapigi kura tu bali wanashindana na wanaume ili wapate vyeo vya kisiasa. Israeli ilikuwa na waziri mkuu mwanamke, Golda Meir, na ndivyo ilivyokuwa na India, Indira Gandhi. Hivi majuzi zaidi wanawake wamechaguliwa kuwa mawaziri wakuu katika Uingereza na Yugoslavia. Katika Baraza Kuu la Urusi, 492, au kati ya asilimia 30 na 40, ni wanawake. Sasa mwanamke mmoja ni mshiriki wa Mahakama Kuu ya U.S. na katika kampeni ya 1984 ya kugombea kiti cha urais, kwa mara ya kwanza mwanamke aligombea kiti cha makamu wa rais katika chama kikubwa cha kisiasa. Katika Ufaransa, karibu asilimia 15 ya viti vyote vya baraza la mawaziri inashikiliwa na wanawake.

Wanawake Katika Kazi ya Kuajiriwa

Katika United States, badala ya kupata ishara zikisomwa “Wanaume Wanafanya Kazi,” sasa ishara nyingi zinasoma “Watu Wanafanya Kazi.” Kwa sababu gani? Kwa sababu ya badiliko katika ushiriki wa wanawake katika sehemu ya kiuchumi. Hesabu ya wanawake wanaofanya kazi nje ya nyumba imekuwa maradufu katika miaka 25 iliyopita. Huko nyuma katika 1970 wanawake walishikilia asilimia 27 ya kazi za afisini; miaka 14 baadaye, wanawake walishikilia asilimia 65 ya kazi hizo. Kwa wengine, kufanya kazi ya kuajiriwa ni jambo linalohitajiwa sana kiuchumi; kwa wengine ni jambo la hiari tu. Katika sehemu fulani, mishahara ya wanaume na wanawake wanaofanya kazi zinazofanana inaendelea polepole zaidi kulingana.

Katika Elimu, Ufundi, na Dini

Wanawake wamefanya maendeleo makubwa sana kuhusu elimu karibu ulimwenguni pote. Hesabu ya wanawake walio shuleni imeongezeka kutoka milioni 95 katika 1950 mpaka milioni 390 katika 1985. Katika Hispania miaka 25 iliyopita, hesabu ya wanawake wasiojua kusoma na kuandika ilikuwa mara mbili ile ya wanaume. Kufikia 1983 hali hiyo imefanyiwa maendeleo hivi kwamba asilimia 30 ya wanafunzi wa koleji ni wanawake. Gazeti Women in Britain linaripoti “ongezeko lenye kustaajabisha katika hesabu ya wanawake walio wanafunzi wa wakati wote wa chuo kikuu.”

Katika muda wa miaka iliyopita, wanawake wamekuwa mashuhuri katika mambo ya kimuziki wakiwa wanaimba wakiwa peke yao kwa sauti na kwa kutumia chombo pia. Lakini katika United States kabla ya 1935, wanawake pekee waliocheza katika jamii ya wapigamuziki walikuwa wapiga vinubi tu, sehemu ambayo wanaume walionekana wakiepuka. Tofauti na hilo, kwa sasa asilimia 40 ya wale wanaocheza katika jamii kubwa za wapigamuziki, za kimkoa, na wanaocheza katika miji mikubwa-mikubwa ni wanawake.

Kumekuwa na ongezeko linalofanana na hilo katika mambo ya dini. Wanawake wengi wamejiandikisha katika seminari, hivi kwamba katika United States kuanzia asilimia 29 hadi 52 ya wanafunzi hao ni wanawake. Wanawake wanahutubu jukwaani, na pia kuna marabi wanawake. Karibu asilimia 11 ya mapasta wa Uswedi ni wanawake, na kuna makasisi wanawake Waanglikana katika Mashariki. Gazeti The New York Times la (Februari 16, 1987) lilisema hivi “kuna wanawake 968 waliowekwa rasmi katika Kanisa la Episkopali.”

Matokeo Yamekuwa Nini?

Kwa hiyo hatuwezi kukana kwamba hali ya wanawake imebadilika kwa njia yenye kustaajabisha sana katika nyakati za hivi karibuni. Huenda wewe mwenyewe umeona au kuhisi mabadiliko hayo kibinafsi. Lakini yapasa ulizo hili lizushwe: Je! mabadiliko yote haya yamekuwa baraka isiyo na mchanganyiko?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki