Je! Kulikuwako Msalaba wa Kikristo Kabla ya Konstantino
“ISHARA ya msalaba imekuwa mfano wa desturi za kale, iliyokuwako katika karibu kila utamaduni unaojulikana. Maana ya mfano huu umewatatiza wale wanaojifunza juu ya mapokeo, dini na desturi za watu, ingawa kutumiwa kwayo katika sherehe za maziko kungeweza kuelekeza kwenye ulinzi dhidi ya mabaya. Kwa upande mwingine, crux ansata ya Misri inayojulikana sana inayoonyeshwa kuwa inatoka kinywani, lazima ielekeze kwenye uhai au pumzi. Matumizi ya ishara ya msalaba ulimwenguni pote yanafanya utokeze zaidi ule ukosefu wa misalaba katika masalio ya Ukristo wa kwanza, hasa marejezo yo yote halisi kwenye tukio katika Golgotha. Wanachuo walio wengi sasa wanakubali kwamba msalaba, kama rejezo la sanaa kwenye lile tukio lenye maumivu makali, hauwezi kupatikana kabla ya wakati wa Konstintino.”—Ante Pacem—Archaeological Evidence of Church Life Before Constantine (1985), cha Profesa Graydon F. Snyder, ukurasa 27.