Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w88 11/1 uku. 31
  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1988
  • Habari Zinazolingana
  • Yesu Awatokea Wavuvi
    Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
  • Mtume Petro—Kwa Sababu Gani Anapendwa Sana na Wengi?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1978
  • Kwenye Ufuo wa Bahari ya Galilaya
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
  • Alishinda Woga na Shaka
    Igeni Imani Yao
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1988
w88 11/1 uku. 31

Maswali Kutoka kwa Wasomaji

■ Yesu alikuwa akirejeza kwenye kitu gani kwa kusema “hawa” wakati alipokuwa akiuliza Petro, “Wewe wanipenda kuliko hawa?”

Yesu mfufuliwa alikuwa kwenye Bahari ya Galilaya. Tunasoma hivi “Basi walipokwisha kula [kiamsha-kinywa, NW], Yesu akamwambia Simoni Petro, Je! Simoni wa Yohana, wewe wanipenda kuliko hawa? Akamwambia, Naam, Bwana, wewe wajua kuwa nakupenda [nina shauku kwako, NW]. Akamwambia, Lisha wanakondoo wangu.”​—Yohana 21:15.

Ingawa nyakati fulani ujinsia wa kiwakilishi (pronauni) cha Kigiriki huonyesha kiima chake (habari inayozungumziwa), wingi wa touʹton (“hawa”) unaweza kuwa na kiima cha ujinsia wa kiume, wa kike, au usio wa jinsia yoyote. Hivyo basi, wanachuo wamedokeza maana tatu zinazowezekana kwa swali la Yesu

1. Je! wewe unanipenda mimi kuliko vile wewe unapenda hawa wanafunzi wengine?

2. Je! wewe unanipenda mimi kuliko vile hawa wanafunzi wananipenda mimi?

3. Je! wewe unanipenda mimi kuliko vitu hivi, kama wale samaki?

Acheni tusababu-sababu juu ya mambo hayo matatu tuone ni jipi linaloelekea kuwa ndilo jambo lenyewe.

Namba 1. Kwa kutoboa mambo wazi, ni Wakristo wachache wanaweza kuwazia Kristo akiuliza, ‘Je! wewe unampenda mimi kuliko vile unavyowapenda wanafunzi?’ Ni wazi kwamba sisi tunapaswa kumpenda yeye. Lingeelekea kuwa jambo la kiajabu hasa kuuliza Petro swali kama hilo. Ni muda mfupi tu uliokuwa umepita tangu yeye awe katika mashua ile pamoja na wanafunzi sita wengine, lakini Petro alipomtambua Yesu akiwa kwenye ufuo wa bahari aliwaacha wanafunzi na kuogelea kwenda ufuoni. Akionyesha ufungamano wa jinsi iyo hiyo. wakati Kristo alipouliza kama mitume walitaka kwenda zao pamoja na wale waliojikwaa, Petro alisema kwamba yeye alipiga moyo konde kubaki kando ya Yesu.​—Yohana 6:66-69; 21:7, 8.

Namba 2. Namna gani juu ya ule uwezekano wa kwamba Yesu alimaanisha, ‘Petro, je! wewe una upendo mwingi kwa mimi kuliko ule ambao wanafunzi wale wengine wanao?’ Waelezaji wengi wameunga mkono rai hiyo, kwa kuwa mapema kidogo Petro alidai kwamba alikuwa na ushikamanifu mwingi kwa Yesu kuliko wale wengine. (Mathayo 26:33-35) Hata hivyo kuelewa Yohana 21:15 kwa njia hiyo kunataka kwamba kitenzi fulani kisichotaarifiwa hapo kimaanishwe kuwa kilikuwapo, kama vile “Je! wewe unanipenda mimi kuliko vile hawa [wanavyofanya]?” (Linganisha Yohana 7:31.) Lakini kitenzi hicho cha ziada hakimo katika swali la Yesu, wala muundo wa sarufi yenyewe haukitaki kiwepo. Waaidha, lingeelekea kuwa jambo lisilofaa Yesu kumwomba Petro alinganishe kiasi cha upendo wake na kiasi cha upendo ambao huenda wengine wakawa nao. Je! kwani Yesu hakusahihisha mitume wakati walipoangukia ushindani?​—Marko 9:33-37; 10.35-44; Luka 22:24-27.

Basi, je! ingeweza kuwa kwamba Yesu alikuwa akiuliza lile swali la Namba 3? Uwezekano huo unafaana na jinsi kifungu cha maneno ya swali lenyewe kilivyopangwa, kwa maana Petro alikuwa akiombwa achague kati ya mambo mawili (kati ya Yesu na “[vitu] hivi”). Swali kama hilo lingefaa pia kwa sababu ya mambo ya Petro ya wakati uliopita. Yeye alikuwa amekuwa mmoja wa wanafunzi walio wa kwanza kufuata Yesu. (Yohana 1:35-42) Ingawa hivyo, inaonekana Petro hakudumu katika kufuata Yesu wakati wote. Badala ya hivyo yeye alirudia kuvua samaki. Hivyo, miezi kadhaa baadaye Yesu alilazimika kumwita Petro atoke kwenye biashara hiyo kubwa ili awe ‘mvuvi wa watu.’ (Mathayo 4:18-20; Luka 5:1-11) Hata hivyo, baada ya kifo cha Yesu Petro alichukua hatua ya kwanza ya kurudia kazi hiyo ya maisha, akiambia baadhi ya wanafunzi hivi: “Naenda kuvua samaki.”​—Yohana 21.2, 3.

Kwa hiyo, inawezekana sana kwamba Yesu alikuwa akitia mkazo ili Petro ang’amue uhitaji wa kufanya uchaguzi wa kukata maneno kabisa. Ni jambo gani hasa ambalo yeye angeweka kwanza maishani​—kuwa mfuasi wa Yesu, au kuwa mfuatiaji kazi fulani ya maisha, kama ilivyodokezwa na samaki wale waliorundikwa mbele yao? Wale samaki, zile nyavu, zile mashua, na ule urafiki wa kuzoeleana sana na wavuvi-samaki wenzake ulikuwa na nafasi yenye umaana mkubwa kadiri gani katika moyo wa Petro? Je! kweli Petro angeacha vitu hivyo vyenye kufurahika ili aweke kwanza kabisa upendo kwa Kristo na ulishaji kondoo ambao ungefuatana na kufanya hivyo?

Sisi tunaweza kujiuliza wenyewe swali kama hilo kuhusu ‘vitu hivi’ ambavyo huenda vikatuvutia, kama vile kazi au biashara yetu yenye kupendeza, mfurahio wetu wa elimu ya kimwili, maskani yetu au namna ya tafrija tunayopendelea zaidi. Tunaweza kufikiria jambo hili kwa kuonyesha wazi maoni yetu: “Je! mimi napenda Yesu kuliko chochote cha vitu hivi au kuliko vyote hivyo?” Yesu alionyesha kwamba ikiwa jibu letu lenye uhakikisho m Ndiyo, sisi tutakuwa tukionyesha hivyo kwa kuwalisha kondoo.

[Picha Credit Line katika ukurasa wa 31]

Pictorial Archive (Near Eastern History) Est.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki