Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w89 10/1 kur. 30-31
  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1989
  • Habari Zinazolingana
  • Msingi Imara wa Kuwa na Tumaini Hakika
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1976
  • Endeleeni Kuwa Tayari!
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1985
  • Kuhusu “Mwisho”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2009
  • Mitume Waomba Ishara
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1989
w89 10/1 kur. 30-31

Maswali Kutoka kwa Wasomaji

◼ Je! Wakristo wa karne ya kwanza waliamini kwamba mwisho wa mfumo mwovu huu ungekuja katika muda wa maisha yao?

Wafuasi wa Yesu katika karne ya kwanza walikuwa na hamu nyingi ya kuona mwisho ukija. Kama tutakavyoona, baadhi yao walikata shauri kwamba mwisho ulikuwa karibu sana, kwamba ungekuja upesi kabisa. Maoni yao yalihitaji kusahihishwa. Lakini kwa uhakika si vibaya Wakristo, wa wakati huo au wa sasa, kuamini kwa weupe wa moyo kwamba mwisho uliotabiriwa ni lazima utendewe kuwa karibu na waishi kila siku kupatana na kujua hivyo.

Katika kujibu swali la wanafunzi wake kuhusu “ishara” ya kuwapo kwake, Yesu aliwaonya hivi: “Endeleeni kulinda, basi, kwa sababu nyinyi hamjui ni siku gani Bwana wenu anakuja.” (Mathayo 24:3, 42, NW) Kukaa chonjo hivyo kwapasa kuathiri vitendo vyetu, kwa maana Kristo aliongezea hivi: “Jiangalieni, mioyo yenu isije ikalemewa na ulafi, na ulevi, na masumbufu ya maisha haya; siku ile ikawajia ghafula . . . Basi, kesheni ninyi kila wakati, mkiomba, ili mpate kuokoka katika hayo yote yatakayotokea, na kusimama mbele za Mwana wa Adamu.”—Luka 21:34-36.

Angalia kwamba Yesu alitoa ushauri huu mara tu baada ya kutoa mpangilio wa matukio ambayo yangejumlika kufanyiza “ile ishara.” Kwa hiyo mitume walifanywa chonjo waone uhakika wa kwamba ilikuwa lazima mambo fulani yasitawi kihistoria kabla ya ule mwisho. Hata hivyo, majuma machache baadaye, wao walimuuliza hivi Yesu mfufuliwa: “Je! Bwana, wakati huu ndipo unapowarudishia Israeli ufalme?” Yeye akajibu: “Si kazi yenu kujua nyakati wala majira, Baba aliyoyaweka katika mamlaka yake mwenyewe.”—Matendo 1:6, 7.

Twaweza kuona kutokana na jambo hili kwamba wafuasi wa Yesu wenye ukaribu mwingi zaidi naye walikuwa na hamu nyingi sana ya kuona mwisho ukija haraka hata wakasahau aliyokuwa amewaambia majuzi kuhusu shuhuda zenye kuonekana kwa macho ambazo ilikuwa lazima zisitawi wakati wa kuwapo kwake kabla ya mwisho huo.

Twapata kionyeshi kingine cha hamu yao katika barua za mtume Paulo kwa Wakristo Wathesaionike. Mwaka wa 50 W.K. hivi, yeye aliandika: “Ndugu, kwa habari ya nyakati na majira, hamna haya niwaandikie. Maana ninyi wenyewe mnajua yakini ya kuwa siku ya Bwana yaja kama vile mwivi ajavyo usiku. Basi tusilale usingizi kama wengine, bali tukeshe, na kuwa na kiasi.” (1 Wathesalonike 5:1,2, 6) Baadhi ya Wakristo hao waliopakwa mafuta kwa roho walichukua kwamba hiyo ilimaanisha kuwa kuwapo kwa Yesu (pamoja na siku ya Yehova ya kuwaua waovu) kulikuwa kukija wakati huo huo, mara hiyo.

Lakini sivyo. Kwa uhakika, Paulo aliwaandikia katika barua ya pili hivi: “Kwa habari ya kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo, na kukusanyika kwetu mbele zake, kwamba msifadhaishwe upesi hata kuiacha nia yenu, wala msisitushwe, kwa roho, wala kwa neno, wala kwa waraka unaodhaniwa kuwa ni wetu, kana kwamba siku ya Bwana [Yehova, NW] imekwisha kuwapo. Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yo yote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu; akafunuliwa yule mtu wa kuasi.”—2 Wathesalonike 2:1-3.

Hii haikumaanisha kwamba wangeweza kujikalia kitako tu kuhusiana na kuwapo kwa Yesu na mwisho wa mfumo. Kila mwaka ulipozidi kupita, onyo la Yesu liliwakabili kinaganaga zaidi: “Endeleeni kulinda, basi, kwa sababu nyinyi hamjui ni siku gani Bwana wenu anakuja.”

Hivyo, miaka mitano hivi baada ya kuandika Wathesalonike Pili, Paulo aliandika hivi: “Saa ya kuamka katika usingizi imekwisha kuwadia; kwa maana sasa wokovu wetu u karibu nasi kuliko tulipoanza kuamini. Usiku umeendelea sana, mchana umekaribia; basi na tuyavue matendo ya giza, na kuzivaa silaha za nuru.” (Warumi 13:11, 12) Baada ya miaka mitano zaidi, Paulo aliwapa Wakristo Waebrania ushauri huu: “Mnahitaji saburi [uvumilivu, NW], ili kwamba mkiisha kuyafanya mapenzi ya Mungu mpate ile ahadi. Kwa kuwa bado kitambo kidogo sana, yeye ajaye atakuja, wala hatakawia.” (Waebrania 10:36,37) Halafu, katika mstari unaotangulia ule wa mwisho kabisa wa Ufunuo, mtume Yohana aliandika hivi: “Yeye mwenye kuyashuhudia haya asema, Naam; naja upesi. Amina; na uje, Bwana Yesu.”—Ufunuo 22:20.

Bila shaka, Mkristo wa huko nyuma hakuwa akikosa kusababu mambo kiakili kwa kuhisi kwamba mwisho ungeweza kuja katika muda wa maisha yake. Na kama yeye angekufa kupitia aksidenti au kawaida za kiasili kabla ya ule mwisho, hapo yeye angalikuwa ameishi akiwa na hisia ifaayo ya kujali uharaka ambao Yesu na Maandiko yaliyovuviwa yaliutokeza.

Yote haya yatumika hata zaidi kwetu, kwenye saa hii iliyosonga sana ambamo sisi twaishi. Kwa kutaja maneno ya Paulo kimuhtasari, hatuwezi kukana kwamba ‘sasa wokovu wetu u karibu kuliko wakati ambapo Wakristo wa kwanza walipata kuwa waamini na hata kuliko wakati ambapo sisi wenyewe tulipata kuwa waamini. Usiku umeendelea sana, mchana umekaribia.’

Kuanzia Vita ya Ulimwengu 1 tumeweza kuona katika historia ushuhuda wenye kuonekana kwa macho ukipanda juu kama mlima, ushuhuda wenye kuthibitisha kwamba tumo katika umalizio wa mfumo wa mambo. Badala ya kujishughulisha mno kukisia-kisia ni lini hasa mwisho utatukia, yatupasa tujishughulishe na kuzihubiri habari njema, ambako kwaweza kuokoa maisha zetu na maisha za wengine wengi,—1 Timotheo 4:16.

Sisi tuna sababu za kutosha kutarajia kwamba kuhubiri huku kutamalizwa katika wakati wetu. Je! hiyo yamaanisha itakuwa hivyo kabla ya mwanzo wa mwezi mpya, mwaka mpya, mwongo mpya, karne mpya? Hakuna mwanadamu ajuaye, kwa maana Yesu alisema kwamba “hata malaika walio mbinguni” hawakujua jambo hilo. (Mathayo 24:36) Zaidi ya hilo, hatuhitaji kujua, huku tukifanya yale ambayo Bwana atuamuru tukaze fikira juu ya kuyafanya. Lililo la maana zaidi ni kwamba penzi la Mungu na kazi Yake ifanywe na kwamba sisi tuwe na ushiriki ulio kamili kabisa katika kazi hiyo. Hivyo huenda ‘tukapata kuokoka katika hayo yote yatakayotokea, na kusimama mbele za Mwana wa Adamu.’—Luka 21:36.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki