Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w89 12/15 uku. 26
  • “Siku ya Mtakatifu Nicholas” Ilitoka Wapi?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • “Siku ya Mtakatifu Nicholas” Ilitoka Wapi?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1989
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • “Mtakatifu” Nicholas na Odin
  • Desturi za Ki-Siku-Hizi Kuhusu Nguvu za Uzazi
  • Uamuzi kwa Waabudu wa Kweli
  • “Kwa Kweli Hilo Ni Jina la Mungu Ambalo Ni Takatifu na Kuu Zaidi”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2008
  • Ukweli Kuhusu Krismasi
    Amkeni!—2010
  • Krismasi (Noёl) Ilianza Zamani Sana
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1979
  • Mapokeo ya Krismasi—Yana Mianzo Gani?
    Amkeni!—1990
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1989
w89 12/15 uku. 26

“Siku ya Mtakatifu Nicholas” Ilitoka Wapi?

TEMBEA katika barabara za Ubelgiji mapema Desemba, nawe utaona mwono wenye kuvuta macho: vikundi vidogo vya watoto wakienda nyumba kwa nyumba, wakiimba tenzi fupi ambazo zaitwa “nyimbo za Mtakatifu [Saint] Nicholas.” Wenye nyumba huitikia watoto hao wenye kuvutia kwa kuwapa zawadi za matunda, vitu vitamu vitamu, au pesa.

Pindi hiyo ni nini? Ni “Siku ya Mtakatifu Nicholas”! Katika United States na mabara mengine, “Mtakatifu Nicholas,” au “Mtakatifu [Santa] Claus,” ahusianishwa na siku ya Krismasi. Lakini katika Ubelgiji, “mtakatifu” huyo mwenye ndevu ana siku yake mwenyewe. Kweli kweli, “Mtakatifu Nicholas” (Sinterklaas, au Sint Nicolaas), ambaye sikukuu yake hufika tarehe sita ya Desemba, ni mmoja wa “watakatifu” walio maarufu zaidi katika Ubelgiji na Uholanzi. Makanisa, vikanisa, barabara, au makao mengi yameitwa jina lake. Kulingana na mapokeo yeye ajulikana kuwa “yule rafiki mkubwa wa watoto” ambaye huwagawi zawadi wakati wa sikukuu yake.

Jioni yenye kutangulia holidei hiyo, watoto wachanga huweka kimoja cha vitu au ndara (slipa) zao kwenye bomba la kutoa moshi katika nyumba, huku wakiimba tenzi zao dogo-ndogo. Wao wameambiwa kwamba “Mtakatifu” Nicholas na mtumishi wake mweusi (aitwaye Petro Mweusi) atawasili usiku huo kwa meli-stima kutoka Hispania. Baadaye, “mtakatifu” huyo atapanda farasi wake wa kijivujivu apite juu ya dari za nyumba, akifuatwa na Petro Mweusi, mwenye kubeba fimbo na mfuko mkubwa wenye vitu vya kuchezea na peremende. Pia Nicholas huleta matofaa, njugu, na mazao mengine ya shamba. Mara nyingi yeye huacha ana fulani ya biskuti ya kahawia, iliyotiwa vikolezo ambayo huitwa speculaas, au biskuti za askofu, ambazo huokwa zikawa na maumbo maalumu, yaliyofanyizwa kwa njia ya kuvutia.

Ni nani huzipokea? Ni watoto ambao wamekuwa wema mwaka uliopita. Ingawa hivyo, wale waliokuwa si watiifu husemwa kwamba huipata ile fimbo; au kwa ubaya zaidi, huenda wakaingizwa ndani ya mfuko wa Petro Mweusi na kubebwa wapelekwe mbali! Basi, yaeleweka ni kwa nini watoto huwa na hamu nyingi ya kutuliza wageni hawa wenye kuzuru usiku. Hivyo, bilauri moja ya gini (kileo) humngojea mtakatifu” huyo, na karoti moja au vipande vichache vya sukari iliyoshikamana huwekwa tayari kwa ajili ya farasi wake.

Wazazi wengi katika Ubelgiji huiona “Siku ya Mtakatifu Nicholas” kuwa ndio wakati wa shangwe nyingi zaidi mwakani. Wao hupendezwa sana kutazama nyuso zenye matazamio makubwa za wadogo-wadogo wao ambao huwa na hamu nyingi ya kujua wameletewa nini na yule “mtakatifu mwema”! Kwa hiyo wao hupitishia watoto wao hadithi za mapokeo, bila kujua vizuri desturi hizi zilitoka wapi. Kama wangejua, labda wangeshtuka.

“Mtakatifu” Nicholas na Odin

Oosthoeks Encyclopedia yaeleza hivi: “Mwadhimisho [wa Mtakatifu Nicholas ambao hufanywa ndani ya nyumba ulitokana na sherehe ya kanisa (yenye kuhusisha ndani kuwapa watoto vitu wasivyotazamia), nayo pia ikiwa imetokana na vyanzo vya kabla ya Ukristo. Mtakatifu Nicholas, ambaye hupanda [farasi] akipita juu ya dari za nyumba, ni yule mungu Wodan [Odin ] wa kipagani. . . . Mtakatifu Nicholas ndiye pia aliyekuwa kiongozi wa ile kukuru-kakara isiyoeleweka vizuri ambamo nafsi za wafu huizuru dunia.”

Ndiyo, Wateutoni waliamini kwamba Odin, au Wodan, mungu wao mkuu, aliongoza nafsi za wafu kupanda farasi kwa kupita nyikani kwa mbio zenye kiruu kingi wakati wa zile “siku kumi na mbili mbaya” zilizo kati ya Krismasi na Epifani (Januari 6). Upepo mkali uliovuma kutokana na mpando huo uliambatana na mbegu za mazao ya mashamba, ukichochea nguvu za uzazi. Namna gani matofaa, njugu, na mazao mengine ya majira ya vuli ambayo hutolewa karibu na “Siku ya Mtakatifu Nicholas”? Hayo yalikuwa vifananishi vya nguvu za uzazi. Watu wa kale waliamini kwamba wangeweza kutuliza miungu yao kwa kuipa zawadi wakati wa zile siku za giza, zenye baridi ya kipupwe. Kufanya hivyo kungeongezea nguvu za uzazi za mwanadamu, za mnyama, na za udongo.

Odin aliandamwa na Eckhard mtumishi wake, aliyekuwa mtangulizi wa Petro Mweusi, ambaye pia alibeba fimbo. Hivi majuzi tu katika zile Enzi za Katikati, kulikuwa na imani maarufu kwamba miti na mimea fulani ingeweza kuwapa wanadamu nguvu za uzazi na kwamba kupiga mwanamke tu kwa tawi moja la mti wa jinsi hiyo kulitosha kumtia mimba.

Kitabu Feesten Vierdagen in kerk en volksgebruik (Holidei na Miadhimisho Iliyo Katika Kanisa na Katika Desturi Zilizo Maarufu) hutaja mifanano mingine michache kati ya Odin na “Mtakatifu” Nicholas: “Wodan, pia, aliyajaza mabuti na viatu vya mbao vilivyowekwa karibu na bomba la kutoa moshi katika nyumba lakini yeye alijaza dhahabu humo. Majani makavu na nyasi ziliwekwa ndani ya kile kiatu cha mbao ili ziwe kwa ajili ya farasi hodari wa Wodan. Mganda ulio wa mwisho shambani ulikuwa kwa ajili ya farasi huyo pia.”

Kitabu Sint Nicolaas, kilichotungwa na B. S. P. van den Aardweg, chaonyesha mifanano mingine ya kustaajabisha:

“Mtakatifu Nicholas: mtu mrefu mwenye maungo yenye nguvu akiwa juu ya farasi mweupe. Yeye ana ndevu nyeupe zilizo ndefu, fimbo ya kiaskofu mkononi mwake, na kofia ya kiaskofu juu ya kichwa chake . . . akiwa na joho refu pana la askofu.

“Wodan: mtu mwenye kimo kirefu aliye na ndevu nyeupe. Yeye huvaa kofia yenye ukingo mpana ikiwa imevutwa kwa kufunika sana macho yake. Katika mkono wake yuashika mkuki wa mizungu ya kiuchawi. Ana vazi pana la kujitanda na amepanda Sleipnir farasi wake wa kijivujivu aliye mwaminifu-mshikamanifu.

“Kuna visa zaidi vya hii ambayo yaonwa kuwa mifanano: Wodan alipanda farasi wake wa kijivujivu akipita hewani na watu wenye kutetemeka wakamtolea keki zilizotiwa kikolezo, licha ya kumtolea nyama na mazao ya shamba. Mtakatifu Nicholas hupanda [farasi] akipita juu ya dari za nyumba na watoto hutayarisha majani makavu, karoti, na maji kwa ajili ya farasi huyo. Ile mikate midogo ya tangawizi na ile fimbo zilikuwa ishara za kufananisha nguvu za uzazi muda mrefu kabla ya kuanza kwa sherehe za Mtakatifu Nicholas.”

Desturi za Ki-Siku-Hizi Kuhusu Nguvu za Uzazi

Desturi kadhaa nyinginezo ambazo zahusiana na “Mtakatifu” Nicholas huonyesha pia kwamba zina vyanzo vya kipagani. Kwa kielelezo, katika maeneo ya kaskazini katika siku ya Desemba 4, wavulana wachanga wa miaka kuanzia 12 hadi 18 hutokea katika mabarabara. Wakiwa wamevaa mavazi ya kiajabu-ajabu yaliyopambwa manyoya ya ndege, magamba, na vitu vingine vya kijimbo, wavulana hao waliovaa kifunika-uso huwakilisha “akina Mtakatifu Nicholas wadogo,” au Sunne Klaezjen. Katika jioni ya siku inayofuata, wanaume wenye umri wa miaka 18 na zaidi hupata zamu yao. Mapema jioni, wao hutanga-tanga mabarabarani. Wakitumia fagio, pembe za nyati, na marungu, wao hufukuza wanawake wote, wasichana, na wavulana wadogo wenye kukutana nao. Wasichana wachanga hufanywa wacheze dansi au waruke juu ya kijiti fulani.

Kusudi la hayo yote ni nini? Hapo tena, lilikuwa ni nguvu za uzazi—lile hangaiko lenye kutukia upya daima la tamaduni za kale. Majira ya kipupwe yalikuwa kipindi chenye giza na cha wasiwasi, na mara nyingi yalionwa kuwa ndio wakati ambapo yule mungu wa nguvu za uzazi alilala au akawa ni mfu. Ilifikiriwa kwamba kwa kutumia njia mbalimbali mungu huyo angeweza kupewa uhai mpya au kwamba mungu-mume au mungu-mke huyo angeweza angalau kupewa usaidizi fulani. Zawadi, dansi, kelele, mapigo kutokana na fimbo ya nguvu za uzazi—zote hizi zilionwa kuwa njia za kufukuza roho waovu na kuongezea nguvu za uzazi katika wanadamu, wanyama, na udongo.

Kwa hiyo wakati wasichana wachanga warukapo juu ya kijiti kile, wao huwa wakiiga wazazi wao wa kale waliokufa ambao waliamini kwamba kimo ambacho waliruka kingekuwa ndicho kimo ambacho mmea wa kitani ungekua. Kwa kufukuza wanawake na watoto, wale vijana wa kiume huwa wanaigiza ile desturi ya kufukuza roho waovu.

Uamuzi kwa Waabudu wa Kweli

Kwa nini desturi hizo zimekuwa sehemu ya ule uitwao Ukristo eti? Kwa sababu karne kadhaa zilizopita, wamisionari wa makanisa hawakusisitiza kwamba waongofu wao wafuate amri hii ya Kimaandiko: “Tokeni kati yao, mkatengwe nao . . . msiguse kitu kilicho kichafu.” (2 Wakorintho 6:17) Badala ya kukomesha mazoea ya kipagani, kwa kweli wamisionari wa Jumuiya ya Wakristo waliendeleza daima desturi hizi kwa kuzifanyia marekebisho mapya na kuzitumia. Desturi hizo ndipo zikaenea katika sehemu zote za ulimwengu.

Wahamiaji Waholanzi ambao walilowea katika Amerika ya Kaskazini walipeleka huko ule mwadhimisho wa “Mtakatifu” [Saint] Nicholas. Baada ya muda fulani jina hilo likatamkwa isivyofaa likawa “Mtakatifu [Santa] Claus.” Yule askofu mwenye fahari aligeuzwa akawa jamaa fulani mwenye mashavu mekundu, tena mnene-mnene, mwenye kuvaa suti nyekundu-nyangavu. Ile kofia yake ya kiaskofu ilibadilishwa kwa kofia ya kizimwi (mzuka) na yule farasi mweupe akabadilishwa kwa sleji (kitelezo) yenye kukokotwa na kulungu. Hata hivyo, Mtakatifu [Santa] Claus aliendelea kuwa mleta-zawadi, ingawa ziara yake ilibadilishwa ikawa ya Jioni Tangulizi ya Krismasi.

Katika maeneo ya Ujeremani yaliyo ya Kiprotestanti, nafasi ya “Mtakatifu” Nicholas wa Kikatoliki ilichukuliwa na “Baba Krismasi” mwenye tabia chache zaidi za kutambulisha alivyo. Hata hivyo, vile vyanzo vya kipagani vingali vyatambulikana wazi hadi leo hii.

Yesu Kristo alisema kwamba “waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli.” (Yohana 4:23) Desturi za “Mtakatifu” Nicholas zatokeza dai la kweli kweli kwa wenye kuabudu wakiwa na moyo mweupe: Je! waabudu hawa wataendeleza daima yale mazoea ya kale ya kidhehebu cha Odin, au watajitenga wawe huru na masalio ya upagani? Huu ni wakati mzuri wa mwaka kufikiria swali hilo lenye uzito.

[Hisani katika ukurasa wa 26]

Harper’s Weekly

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki