Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g90 10/8 kur. 22-25
  • Mapokeo ya Krismasi—Yana Mianzo Gani?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mapokeo ya Krismasi—Yana Mianzo Gani?
  • Amkeni!—1990
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Mianzo Iliyotangulia Ukristo
  • Haikuadhimishwa na Wakristo wa Mapema
  • Mapokeo ya Krismasi Yafufuliwa
  • Krismasi—Wakati wa Balaa
  • Maoni Tofauti
  • Ni Nini Kilichoipata Krismasi ya Kidesturi?
    Amkeni!—1993
  • Krismasi—Kwa Nini Inapendwa Sana Katika Japani?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1991
  • Je! Ni Lazima Wewe Usherehekee Krismasi?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
  • Krismasi Inamaanisha Nini Kwako?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1994
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1990
g90 10/8 kur. 22-25

Mapokeo ya Krismasi—Yana Mianzo Gani?

KATIKA Kizio cha Kaskazini na Kizio cha Kusini, miadhimisho ya Krismasi ni miongoni mwa iliyo maarufu kabisa, miongoni mwa waamini na wasio waamini pia. Katika Japani, ambako watu walio wengi ni Washinto wasio Wakristo, Krismasi hufanywa kwa njia iliyo sawa na miadhimisho mingineyo na huo umekuwa wakati wa sherehe yenye makelele yasiyozuiliwa na wa ubiashara. Lakini je! sikuzote sherehe za Krismasi zimekuwa za kilimwengu kadiri hiyo? Sherehe hii ya msimu kwa msimu ilianzaje?

Kutazama jinsi Krismasi ilivyoadhimishwa katika mileani ya kwanza ya Wakati wa Kawaida kwasaidia kufuatilia mwanzo wayo hadi huko nyuma kwenye vyanzo vilivyotangulia Ukristo. Akiandika katika gazeti History Today, Alexander Murray wa Chuo Kikuu cha Oxford akazania kwamba binadamu wa enzi za katikati “alichanganya viasili vilivyokuwapo vya desturi za kipagani za katikati ya kipupwe pamoja na theolojia yenye kusitawi ya Krismasi.” Hilo lilifanywa jinsi gani na kwa sababu gani?

Mianzo Iliyotangulia Ukristo

Vikundi vya watu wa tamaduni za kale za Ulaya viliona jinsi jua lilivyoonekana kuwa likisimama tuli (mahali pamoja) wakati wa katikati ya kipupwe karibu na upeomacho wa kusini kabla ya kupanda juu tena angani polepole. Huu mtuliojua (au solistasi, ambalo ni neno lililotolewa katika maneno ya Kilatini ya “jua” na “simama tuli”) ulipangiwa tarehe ya Desemba 25 hapo kwanza, kulingana na kalenda ya Kijulia. Watu awa hawa waliona ikiwa rahisi kufanya ulinganifu fulani kati ya jua na Mungu kuwa Chanzo na Mwendelezaji wa uhai. Katika 274 W.K., maliki Mroma alijulisha Sol in victus (jua lisiloshindwa) kuwa ndilo mtegemezaji mkuu wa milki, hiyo ikiwa ni katika Desemba 25, hivyo kuheshimu Mithras, mungu wa nuru.

Juu ya kuibuka kwa Jumuiya ya Wakristo kuwa dini mpya ya kimilki, Murray aandika hivi: “Baada ya mashaka-mashaka mengi, ushindi ungekuwa wa mpinzani mkuu [wa mawazo ya Mithras], Ukristo. Lakini kwenye mwaka wa 300 hivi mpinzani huyu bado alilazimika kuwa mwerevu. Hapo ndipo kanisa liliamua kufanyiza sherehe ya kuzaliwa kwa Kristo (Kilatini: nativitas). (Sherehe hiyo haikutiwa miongoni mwa orodha za sherehe za kuanzia karne ya tatu, na kwa mara ya kwanza sherehe mpya hiyo imeandikwa katika hati ya 336.)” Ni tarehe gani iliyochaguliwa kwa mwadhimisho huo? Ni Desemba 25, hilo likiwa ni tokeo la “uamuzi wa busara na wenye matokeo mazuri kwa upande wa mababa wa kanisa la mapema,” kulingana na kitabu Discovering Christmas Customs and Folklore. Kwa nini?

Muda wa katikati ya kipupwe ulikuwa tayari umeimarishwa kuwa msimu wa shamrashamra za sherehe ya siku saba ya ukulima wa Kiroma ya moto na nuru, Saturnalia. Halafu kukawa na Calends, msherehekeo wa siku tatu wa kuadhimisha kuwekwa rasmi kwa maofisa-wasimamizi wa Kiroma waliotumikia kwa mwaka mmoja kuanzia siku ya kwanza, au “calends,” ya Januari. Hivyo, kwa sababu Saturnalia, Calends, na siku ya Kimithras ya uzaliwa wa jua lisiloshindwa zilitukia pamoja katika kipindi kifupi hivyo kila mwaka, Desemba 25 ikawa ndiyo tarehe iliyochaguliwa kwa mwadhimisho wa “Misa [Masi] ya Kristo” katika kuvutia vikundi vya wapagani vigeukie dini mpya ya kiserikali ya Milki ya Roma.

Kadiri wakati ulivyopita, Yule, sikukuu ya Kijeremani ya katikati ya kipupwe ambayo si ya Kikristo, iliimarisha desturi za kufanya karamu na shamrashamra, na pia utoaji wa zawadi. Mishumaa myembamba, magogo, mapambo ya mimea yenye ubichi daima, na miti ilitumiwa sana katika miadhimisho ya Krismasi. Lakini, huenda watu fulani wakasababu kwamba, mwadhimisho wa uzaliwa wa Kristo ni lazima kwa uhakika uwe ulifanywa kwa umaarufu miongoni mwa Wakristo kabla ya kuja kuhusianishwa baadaye na mapokeo ya kipagani. Je! ndivyo ilivyo?

Haikuadhimishwa na Wakristo wa Mapema

Biblia haifunui tarehe halisi ya uzaliwa wa Yesu. Zaidi ya hilo, “Wakristo wa mapema hawakuadhimisha uzaliwa Wake,” chaeleza The World Book Encyclopedia. Na kwa nini sivyo? “Kwa sababu waliona kwamba kuadhimisha uzaliwa wa mtu yeyote kulikuwa desturi ya kipagani.” Augustus Neander, katika The History of the Christian Religion and Church, During the Three First Centuries, hukubali hivi: “Wazo la sikukuu ya siku ya kuzaliwa lilikuwa mbali na maoni ya Wakristo wa kipindi hiki kwa ujumla.”

Kutokana na uchunguzi huu, waweza kuona kwamba mizizi ya miadhimisho ya Krismasi imo katika desturi za kipagani. Kama vile The Economist kielezavyo, baadaye tu ndipo “wajulishaji [wa habari za kidini] waliamua kuuchukua ‘msherehekeo huu wa nuru [siku ya kuzaliwa kwa jua lisiloshindwa], kwa maana Kristo ndiye nuru ya ulimwengu’, nao wakasingizia (wakiwa na ukosefu wa uthibitisho ambao haungekubaliwa na wenye ujuzi wa Ukweli katika Utangazaji) kwamba mtoto mchanga Yesu alizaliwa katika Desemba. Hiyo ndiyo sababu Scotland yenye kufuata Upresbiteri iliidharau Krismasi kwa muda mrefu, kama vile ilivyodharauliwa na Amerika isiyotaka desturi za kufuata sherehe, mpaka wakati ilipoumbwa upya na mapendezi ya kibiashara.”

Mapokeo ya Krismasi Yafufuliwa

Mwanzoni mwa utawala wa Malkia Victoria (1837-1901), kulingana na Gavin Weightman na Steve Humphries, watungaji wa Christmas Past, “hakuna watoto Waingereza walioangika stokingi [soksi ndefu] zao karibu na mahali pa kuotea moto Jioni-Tangulizi ya Krismasi; hakuna mtu aliyekuwa amesikia juu ya Santa Claus [Baba Krismasi]; fataki za Krismasi hazikuwako; ni watu wachache sana waliokula bata mzinga Siku ya Krismasi; haikuwa kawaida kutoa zawadi; na ule mti wa Krismasi wenye kupambwa na kutiwa taa ulikuwa hata haujulikani sana nje ya ua wa kifalme. Kwa uhakika, Siku ya Krismasi haikuwa tarehe ya maana sana katika kalenda kwa ajili ya desturi ya kijamii ya aina yoyote.” Basi, ni jambo gani lililotendeka likafufua umaarufu wa sherehe za Krismasi?

“Huku kubadilika umbo kwa sikukuu za kale ili ziwe tukio fupi lenye kustahiwa na familia kulianza kwenye miaka ya 1830 hivi . . . na likawa lakaribia kukamilika kwenye miaka ya 1870, na wakati huo ndipo umbo la Santa Claus lilipotokea kwanza katika Uingereza,” chataarifu Christmas Past. Wakati uo huo, kichapo cha Charles Dickens A Christmas Carol, ambacho ni hadithi ya kuongolewa kimaskini kwa Scrooge ili afuate roho ya Krismasi, kilichochea huruma ya kuwafadhili maskini. Hali ovyo na magumu ya kiuchumi ya kuishi katika miji iliyojaa lile Vuvumko la Viwanda zilichochea watu wa enzi ya Victoria waanzishe krusedi ya maadili ambayo, katika kipindi cha baadaye cha enzi ya Edward, ilirekebishwa ili iwatendee fadhili maskini “wenye kustahika” tu.

Mwandikaji mmoja katika Catholic Herald cha Uingereza aonelea hivi: “Kidato kwa kidato, utajiri wa ujumla ulipoongezeka, mengi ya mambo yasiyofaa ya Krismasi yenye kufanywa na watu wa tabaka la katikati yameenea kote. Badala ya usahili wa mambo na ukarimu kumekuwako ushindani na kujitanguliza mbele ya wengine. Badala ya ule msherehekeo wa kinyumbani ambao wakati mmoja ulikuwa mfurahio halisi kumekuwa na shamrashamra potovu za kula kupindukia. Familia hulazimishwa na pokeo hili jipya zitumie siku kadhaa zikiwa pamoja, zipende zisipende, huku zikicheza michezo ambayo baadhi yazo huidharau, zikitazama televisheni ambayo baadhi yazo huichukia, zikiacha kuwasiliana na majirani na watu wa nje wakati mmoja huo ambapo ndipo nia njema na urafiki wa ujumla hupasa kuonyeshwa sana.

“Na mtu akisema hivyo, mtu akithubutu kuchambua ule ubiashara ama zile desturi za kijamii tu zinazohusika, yeye huitwa maskini hohehahe. Kwa maoni yangu Krismasi imekuwa na kasoro mbaya sana katika miaka ya majuzi.”

Kama wewe unakubaliana au hukubaliani na mkadirio huo, ni jambo gani liwezalo kutukia katika ujirani wako wakati wa Krismasi?

Krismasi—Wakati wa Balaa

Je! wewe waona kwamba watu fulani hutumia pindi hii kwa kula na kunywa kupindukia? Je! tabia ya ulevi na makelele huvuruga amani ya jumuiya yenu? Ingawa watu wengi wenye mioyo myeupe huonyesha fadhili na ufikirio wa kutokeza wakati wa Krismasi, jitihada zao hazizuii uharibifu wa mahusiano ya kifamilia ambao hutukia sana kwenye msimu huo.

Basi wewe ungeweza kuuliza hivi, ‘Kwa nini Krismasi hutokeza hali hizo za kupita kiasi za mwenendo mbaya?’ Kwa msingi, ni kwa sababu si ya Kikristo, ni ya kipagani. Je! waweza kuwazia Kristo akipendezwa na jambo hilo? Sivyo kamwe. Kwa kweli, kwa kutumia maneno ya wazi, Biblia husababu hivi: “Pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza? Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari [Shetani]?”—2 Wakorintho 6:14, 15.

Maoni Tofauti

Wakati wa msimu huu wa Krismasi, wewe waweza kupata ziara kutoka kwa mmoja wa Mashahidi wa Yehova. Utaona kwamba wao hawajiungi katika miadhimisho ya Krismasi. Labda wewe wahangaikia watoto wao, ukidhani kwamba wao, zaidi ya watu wengine wote, ndio huukosa ufurahio wa misherehekeo hiyo. Lakini katika hoji moja lililofanywa katika Southern Evening Echo la Southampton (Uingereza), baba mmoja Shahidi mwenye watoto wawili alitoa uhakikishio huu: “‘Kwa kweli wao hawahisi wanakosa ufurahio, mimi nawahakikishia’ asema John. ‘Mashahidi wa Yehova wana bidii sana katika kukuza maisha ya familia yenye furaha. Kwa hiyo zaidi ya kuwapa watoto wetu zawadi nyingi muda wote mwakani, sisi huwapa kitu chenye thamani zaidi [, yaani,] wakati na upendo wetu.’”

Kwa uhakika, upendo na upendezi huo halisi huchangia sana maisha ya familia yenye furaha. Kwa hiyo badala ya kufuata mapokeo ya Krismasi yaliyo na mwanzo wa kipagani, je! haingekuwa vizuri zaidi kila mtu akimheshimu Yesu kwa kuonyesha roho ya kweli iliyo kama ya Kristo kwa watu wa ukoo, rafiki, na watu tuwajuao, ndiyo, na kwa watu tusiowajua pia, muda wote mwakani?

[Sanduku/Picha katika ukurasa wa 23]

BABA KRISMASI, AITWAYE PIA SANTA CLAUS

Baba Krismasi imeelezwa kuwa “ndiyo hadithi yenye mafanikio zaidi katika utangazaji tangu Yesu Kristo.” Lakini yeye alikuwa nani? Kulingana na The Customs and Ceremonies of Britain, yeye amekuwa “ajulikana kuwa mtu asiyefahamika wazi mwenye kufananisha msimu [wa Krismasi] tangu angalau karne ya 15 . . . naye huonekana katika mchoro wa kuchongelea mtini wa 1653 katika vazi lake ambalo laonekana kama la ki-siku-hizi: lakini zile ziara za ‘Santa’ za Jioni-Tangulizi ya Krismasi, tabia yake ya kuteremka katika mabomba ya kutolea moshi nyumbani ili ajaze zawadi katika soksi ndefu (au, hata zaidi, katika vitambaa vya mito ya kulalia) na kigari chake chenye kukokotwa na kulungu, yote hayo yalianza kwenye asili ya mapokeo mbalimbali, USA. Tabia yake huko ilichanganywa na hekaya za Ulaya juu ya Mtakatifu Nicholas wa Myra (aliyeokoa wanawali watatu kutoka kwenye umalaya kwa kunyemelea wakati wa usiku-kati na kutoa zawadi ya pesa za mahari, na akiwa Sinte Klaas akajaza zawadi katika viatu vya watoto Waholanzi-Waamerika katika Desemba 6, siku ya msherehekeo wake); yule Krisskringle Mjeremani-Mwamerika (aliyethawabisha watoto wema na kuwaadhibu wabaya); na ngano za Kiskandinavia au za Kirusi juu ya wachawi-waume wenye kukaa katika Ncha ya Kaskazini. . . . Santa huyu Mwamerika aliye kwa namna ya watu wengi alivuka tena Bahari Kuu Atlantiki kwa unyamavu katika miaka ya 1870: ambaye tangu wakati huo amezidi kukaza fikira kwenye vitu vya kimwili tu kwenye ‘Krismasi ya watoto,’ yaonekana bila kuharibiwa sifa na wanabiashara wenye kuiga-iga umbo lake.”

[Sanduku/Picha katika ukurasa wa 24]

MIMEA YA KRISMASI ILIYO NA UBICHI DAIMA

Mimea itumiwayo kwa wingi zaidi miongoni mwa mapambo ya Krismasi ni holly, ivy, na mistletoe, ambayo huelezwa kuwa “mimea ya ajabu inayozaa matunda katika msimu usio wa uhai.” Lakini kwa nini itumiwe hasa mimea hiyo yenye ubichi daima? Ingawa watu fulani huamini kwamba vijitunda vyekundu vya holly huwakilisha damu ya Kristo na majani yao yenye kuchoma-choma hufananisha “taji la miiba” ambayo askari za Pontio Pilato waliweka juu ya kichwa cha Yesu kwa kumdhihaki, wapagani waliona majani maangavu na vijitunda vyenye kung’aa vya holly kuwa ni kifananishi cha kiume cha uhai wa milele. (Mathayo 27:29) Waliuona ivy kuwa kifananishi cha kike cha uhai wa kutokufa. Holly na ivy pamoja ikawa ndicho kifananishi chao cha nguvu za uzazi. Kushirikishwa kwa mistletoe na hali za upagani kungali imara sana hivi kwamba kitabu The Customs and Ceremonies of Britain hutaarifu hivi: “Hakuna mpambaji yeyote wa kanisa atakayevumilia jambo hilo—isipokuwa huko York Minster.” Ujulikanao zaidi kati ya mimea yote yenye ubichi daima ni mti wa Krismasi, ambao umekaziwa kwa muda mrefu katika mapokeo ya Kijeremani na kufanywa maarufu katika Uingereza na mume wa Malkia Victoria, Mwana-Mfalme Albert, na ambao ulikuja kuwa ndicho kitu cha kukaziwa fikira wakati wa familia kuadhimisha Krismasi. Tangu 1947, Oslo, mji mkuu wa Norowei, umepeleka zawadi ya mti wa Krismasi ili ukawe wonyesho katika Kiwanja cha Umma cha Trafalgar katika London.

[Picha katika ukurasa wa 25]

Mti wa Krismasi unaotolewa kila mwaka na Norowei kuwa zawadi kwa Uingereza

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki