Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g93 12/22 kur. 16-19
  • Ni Nini Kilichoipata Krismasi ya Kidesturi?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ni Nini Kilichoipata Krismasi ya Kidesturi?
  • Amkeni!—1993
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Mambo Halisi ya Karne ya 19
  • Dickens na Krismasi
  • Krismasi Yafanywa Kuwa Biashara
  • Vyanzo vya Krismasi
  • Vipi Juu ya Desturi za Krismasi?
  • Mashaka Mengi
  • Jambo la Kufanywa Kuihusu
  • Je! Ni Lazima Wewe Usherehekee Krismasi?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
  • Mapokeo ya Krismasi—Yana Mianzo Gani?
    Amkeni!—1990
  • Krismasi—Kwa Nini Inapendwa Sana Katika Japani?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1991
  • Krismasi Inamaanisha Nini Kwako?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1994
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1993
g93 12/22 kur. 16-19

Ni Nini Kilichoipata Krismasi ya Kidesturi?

“Krismasi ilikuwa pindi yenye kufurahisha kwetu sisi watoto,” asema Rita, akikumbuka huko nyuma miaka ya 1930. “Kila mtu alienda kanisani, ambamo tuliimba nyimbo tulizopenda sana. Tulipokuja nyumbani mama alipika batamzinga, na tulikula pudini na krimu ya Krismasi. Tuliamini kwa moyo kwamba ilikuwa siku ya kuzaliwa kwa Yesu, siku yake. Lakini mambo yamebadilika. Jambo tu ambalo watoto wanaonekana wakifikiria juu yalo sasa ni Baba Krismasi akija kuleta zawadi.”[1]

Na mleta habari za Amkeni! katika Uingereza

KWA muda wa miaka ambayo imepita, kusherehekea Krismasi kumebadilika katika njia nyingi—na si katika nyakati za karibuni tu. Hata katika 1836, mtungaji-vitabu Mwingereza Charles Dickens alisema: “Kuna watu ambao watakuambia kwamba Krismasi kwao si kama vile ilivyokuwa zamani.”[6]

Pengine, inashangaza wengine kwamba Kri-smasi haijawa sikuzote tukio lenye kupendwa sana. Katika karne ya 19, Dickens alipoandika, kupendwa kwa Krismasi kulikuwa kumepungua. Magazeti mengi ya Uingereza hayakuchapisha habari juu ya Krismasi wakati wa mwanzo-mwanzo wa hiyo karne.[7]

Dickens na mwenzake mwenye umri mkubwa zaidi Mwamerika, Washington Irving, walijitajidi kuitukuza Krismasi.[8] Kwa nini? Dickens hakutaka kurudisha mapokeo ya zamani bali pia, kujulisha wasomaji wake juu ya mambo halisi ya maisha kwa watu maskini na hivyo kufanya hali yao iwe bora zaidi.[9]

Mambo Halisi ya Karne ya 19

Ijapokuwa mageuzi makuu ya viwanda yalileta usitawi kwa wengine, pia yalisababisha mitaa ya hali ya chini, uchafu, na kazi yenye jasho.[10][13] “Kila mji mkubwa una mtaa mmoja au zaidi wa hali ya chini,” akaandika Friedrich Engels katika 1844, “ambapo wale wafanyao kazi ngumu wasongamana pamoja . . . , wakiwa mbali na tabaka la watu wa maisha ya hali ya juu.”[14]

Sheria ya Viwanda ya Uingereza ya 1825, iliyohusu viwanda vya nguo pekee, ilisema kwamba hakuna mtu anayepaswa kufanya kazi katika kiwanda cha pamba kwa zaidi ya muda wa saa 12 katikati ya juma au kwa saa 9 siku ya Jumamosi.[15] Katika 1846, mwanahistoria Thomas Macaulay alilaumu kazi ngumu zaidi kama hiyo kuwa “yazuia ukuzi wa akili, bila kuandaa wakati wa kutumia akili vizuri, na kukosa wakati wa maendeleo ya kiakili.”[16]

Kurudishwa kwa sherehe za Krismasi kulitukia katikati ya matatizo ya kijamii na kiadili ya karne ya 19.

Dickens na Krismasi

Charles Dickens aliongoza katika kufanya jamii ifikirie matatizo ya watu maskini.[19] Katika kitabu chake cha kale A Christmas Carol, kilichochapishwa katika 1843, Dickens alitumia ujuzi wake kwa ustadi juu ya desturi za Krismasi ili kutimiza kusudi lake.[21]

A Christmas Carol kilifanikiwa mara hiyo, na maelfu ya nakala zikauzwa. Mwaka uliofuata, majumba tisa ya michezo ya kuigiza ya London yalionyesha michezo ya kuigiza ya hadithi hiyo.[23] Katika usiku wa kuamkia Krismasi wa 1867, Dickens alikisoma katika United States huko Boston, Massachusetts. Bw. Fairbanks, mwenye kiwanda kimoja aliyetoka Vermont, naye akasema hivi kwa mke wake: “Baada ya kusikiliza usomaji wa Bw. Dickens wa A Christmas Carol usiku huu nahisi napaswa kuacha desturi ambayo tumekuwa tukishikilia hata sasa ya kuendelea na kazi katika kiwanda Siku ya Krismasi.” Alifanya kulingana na ahadi yake. Mwaka uliofuata aliongeza ile desturi ya kupeana batamzinga wakati wa Krismasi.[24]

Krismasi Yafanywa Kuwa Biashara

Misaada ilikuja kuenea katika kipindi cha Krismasi, kutia na utendaji wa mashirika ya kugawanya makaa-mawe kwa wajane maskini na vilevile wenye kumiliki mashamba wakitoa zawadi za pesa na chakula.[26] Kwa maneno, upesi Krismasi ikaja kuwa, fursa ya matabaka yote ya watu kukutana kwa ushirika wa kijamii. Kuruhusu migawanyiko kati ya matajiri na maskini kusionekane wakati huu wa mwaka kulifanya matajiri wengi wasihisi kuwa na hatia.[27]

Sherehe nyingi za kidesturi zilianzishwa tena au zikaundwa. Kwa mfano, kadi za kwanza za Krismasi zilitokea katika 1843, na gharama ya uchapaji ilipokuwa rahisi, mauzo ya kadi yakasitawi.[28] Miti ya Krismasi, iliyokuwa desturi ya kale sana, pia ilizidi kupendwa baada ya Prince Albert, mume wa Malkia Victoria, kuanzisha njia ya Kijerumani ya upambaji wa miti ya Krismasi, akiitia zari, madoido, na mishumaa.[29]

Kuendeleza Krismasi kibiashara kulianza kuenea. Leo, zaidi tu ya karne baadaye, Krismasi imekuwa ya kibiashara sana hivi kwamba umma unaipinga. Jambo hilo latokeza swali hili: Krismasi ilikuwaje mwanzoni?

Vyanzo vya Krismasi

Likitoa habari ya historia, gazeti The Chicago Tribune Desemba uliopita tu liliandika hivi kwenye ukurasa walo wa mbele: “Kwa kushangaza, sikukuu ambayo sasa Wakristo wanalalamika juu yayo kwamba inachukuliwa na biashara ina dalili za sherehe za kipagani ambazo zilichukuliwa na Ukristo.

“Adhimisho la kwanza la Krismasi lililoripotiwa likiwa kuzaliwa kwa Yesu Kristo lilikuwa zaidi ya miaka 300 iliyopita baada ya tukio hilo. Katika Karne ya 4, Ukristo ukaja kuwa dini rasmi ya Milki ya Roma, na, wanachuo waamini, Wakristo waliiweka Des. 25 kuwa tarehe ya kuzaliwa kwa Yesu ili ipatane na sherehe ya wasio-Wakristo iliyokuwako.

“‘Badala ya kupigana dhidi ya sikukuu za kipagani, waliamua kushiriki nao na kuzibadilisha,’ akasema profesa Russell Belk wa Chuo Kikuu cha Utah . . . ‘Sikukuu za kipagani zilizobadilishwa na Ukristo zilikuwa sherehe za Kiroma za Saturnalia—ambazo zilikuwa sherehe za kufurahia za kupeana zawadi—na baadaye sherehe za Yule (gogo la Krismasi) katikati ya kipupwe,’ akasema Belk.

“Krismasi imezidi na ikapungua kupendwa kwa karne nyingi. Ilipigwa marufuku na Wapuriti kwa muda katika Uingereza na Amerika ambao walipinga upuzi uliohusika nayo. Lakini kuelekea katikati ya 1800, Belk alisema, ‘Krismasi ilikuwa matatani, ikipungua kupendwa.’ Alisema kwamba viongozi wa kidini walifurahia kuona biashara ikihusika, kwa njia ya kupeana zawadi na Baba Krismasi, katika kuianzisha tena sikukuu hiyo.

“Kurudishwa huko, akasema Belk, kuliletwa sana na mtungaji-vitabu Mwingereza Charles Dickens, ambaye kitabu chake ‘A Christmas Carol’ cha 1843 kilionyesha mwanamume bahili aliyekuja kuwa mpaji mkarimu.”[42]

Vipi Juu ya Desturi za Krismasi?

Dickens asemekana kuwa “alifurahia desturi zote na mambo yote yaliyohusiana na Krisma-si.”[20] Lakini desturi hizi na mambo hayo yalitoka wapi?

Likiandaa muono-ndani wenye kupendeza juu ya jambo hili, New York Newsday la Desemba 22, 1992, lilimnukuu John Mosley, aliyeandika kitabu The Christmas Star: “‘Viongozi wa kanisa wa zamani hawakusherehekea Krismasi katika Desemba hasa kusherehekea kuzaliwa kwa Kristo,’ [Mosley] akasema. ‘Ilikuwa njia yao ya kushughulika na kikomo cha kipupwe,’ badiliko la kipupwe, wakati jua linapofika kusini na kuelekea kaskazini tena, likileta mwangaza mpya.

“Uthibitisho wa hilo waonekana katika ishara za Krismasi, akasema Mosley. Ulio dhahiri zaidi ni ule utumiaji wa mimea ya chani-kiwiti, inayofananisha maisha katika wakati wa giza na baridi. ‘Mmea ulio chani-kiwiti zaidi ni mti wa Krismasi,’ akasema. ‘Na Wazungu wa kaskazini walisherehekea kikomo cha kipupwe porini; waliabudu miti. Kwa hiyo mti wa krismasi ni urejezo wa ibada ya mti katika nyakati za kale.’

“Mosley asema pia, ‘Ni nini mnachoweka kwenye miti? Miangaza. Mwangaza hukumbusha Jua na kufananisha Jua. Ni kwa ajili ya kuzaliwa upya kwa Jua na kurudi kwa nuru baada ya kikomo cha kipupwe. Mambo makuu yanayohusika katika kikomo cha kipupwe ni mwangaza na mimea ya chani-kiwiti.

“Des. 25, akaongezea, ‘pia ilikuwa tarehe ya zamani ya kikomo cha kipupwe, na mambo mengi tunayofanya sasa, na ambayo twafikiri kwamba ni desturi za kisasa za Krismasi, kwa kweli ni dalili za chanzo cha sherehe za kipupwe.”[43]

Muziki pia huwa katika sherehe za Krismasi. Hivyo, haishangazi kwamba sherehe za Kiroma za Saturnalia zilitukuzwa kwa karamu na ufurahishaji wazo, kutia na kucheza dansi na kuimba. Kwamba Krismasi ya kisasa ilichukua nyingi ya desturi zayo kutoka Saturnalia ya kale, wanachuo hawapingi tena.[30]

Mashaka Mengi

Askofu mkuu wa Uingereza wa Canterbury, Dakt. George Carey, alilalamika juu ya ile “Krismasi ya Victoriana, Krismasi ya Charles Dickens.” Sababu ilikuwa nini? “Nina wasiwasi ikiwa watoto wetu wataathiriwa na ubiashara,” akasema.[36]

Kulingana na gazeti The Scotsman, askofu Mwanglikana David Jenkins aamini kwamba biashara ya Krismasi inafadhaisha watu sana. “Twaabudu pupa na Krismasi yawa karamu ya pupa na upuzi,” alisema, akiongezea: “Watu wa kawaida hufanywa maskini na kadi zao za mkopo. . . . Kuna uthibitisho unaoongezeka kwamba baada ya Krismasi watu hukata tamaa na kuwa na magombano ya familia. Krismasi huongeza matatizo kuliko inavyoleta manufaa.”[37]

The Church Times la Uingereza kwa kufaa lilijumlisha tatizo la Krismasi hivi kwa ufupi: “Twahitaji kuwekwa huru kutokana na desturi za kupita kiasi za ulevi za bacchanalia (desturi za ibada ya Bacchus) ambazo tumeruhusu zisitawi!”[38]

Jambo la Kufanywa Kuihusu

Unaweza kutambua Krismasi kwa jinsi ilivyo, sherehe ya kipagani inayoandamana kibandia na siku ya kuzaliwa kwa Yesu, na haihusiani kamwe nayo. Ndivyo alivyofanya Rita, mwanamke aliyetajwa mwanzoni. Alikuja kuwa mmoja wa Mashahidi wa Yehova, na sasa ameunganika na washiriki Mashahidi wenzake zaidi ya 4,500,000, wanaoepuka Krismasi kabisa kabisa.

Hata hivyo, si rahisi sikuzote kuchukua msimamo ambao hutofautiana na ule wa wengi. (Linganisha Mathayo 7:13, 14.) The Church Times lilijulisha hivi: “Humbidi mwanamume, mwanamke, au familia kuwa hodari kuchagua kutoshiriki kamwe katika sherehe inayobidishwa zaidi kwetu na marika wetu.”[40]

Wengi ambao wamefanya uamuzi wa “kutoshiriki” wakubali. Lakini pia wanajua kwamba upendo wenye kina wa kweli umewapa kichocheo na nguvu ya kuchukua na kusitawisha msimamo huo. Inawezekana kwako pia—ikiwa hiyo ni tamaa yako.

[Sanduku katika ukurasa wa 17]

Je! ulipata kujua mambo haya ya hakika?

* Yesu hakuzaliwa katika Desemba 25.

* Wachungaji katika Israeli walilinda kondoo zao mazizini katikati ya kipupwe, wala si kondeni usiku.

* Wale ‘wanaume wenye hekima’ kwa kweli walikuwa wafanya mizungu, wanajimu, na walimtembelea Yesu alipokuwa mtoto mdogo, si kitoto kichanga.

* Hakuna mahali popote katika Biblia pasemapo kwamba Wakristo wapaswa kusherehekea kuzaliwa kwa Yesu. Lakini kuna amri ya moja kwa moja ya kuadhimisha kifo chake.

[Sanduku katika ukurasa wa 18]

Sababu Inayofanya Mashahidi Wasiisherehekee

The Witness, gazeti rasmi la Roma ya Katoliki la dayosisi ya Dubuque, Iowa, U.S.A., lilitoa swali lifuatalo katika toleo lalo “Sehemu ya Maswali.”

“Mke wangu ameuliza watoto wangu 10 wasaidie kusherehekea siku ya kuzaliwa kwangu ya mwaka wangu wa 80.

“Hata hivyo, wawili kati ya watoto hao ni Mashahidi wa Yehova nao walisema hawasherehekei siku za kuzaliwa kwa sababu wanaishi maisha yao wakifuata kwa ukaribu mfano ambao Yesu alituachia na kulingana na Biblia.

“Walisema kwamba wala Yesu wala Wakristo wowote wa mapema hawakusherehekea sikukuu. Ilikuwa desturi ya kipagani ambayo Wakristo hawakupaswa kuisherehekea. Ilionwa kuwa desturi ya kipagani wakati wa Kristo nayo yapaswa kuonwa vivyo hivyo leo.”

Kasisi John Dietzen alijibu swali hilo: “Najua inaweza kuwaumiza moyoni, lakini habari mnayotoa ni sahihi. Miongoni mwa tofauti za itikadi na mazoea kati ya Mashahidi wa Yehova na madhehebu mengine ya Kikristo ni hii.

“Wakishikilia itikadi hii, washiriki wao hata hawasherehekei Krismasi, kwa sababu siku hiyo ni ya kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa Yesu na pia kwa sababu tarehe ya Krismasi iliwekwa, kwa wazi katika karne ya nne katika siku ya kikomo cha kipupwe (kulingana na kalenda ya zamani ya Julian), ambayo wakati huo ilikuwa karamu kubwa ya kipagani.”[45]

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 16]

Baba Krismasi: Thomas Nast/Dover Publications, Inc. 1978

Mti na soksi ndefu: Old-Fashioned Christmas Illustrations/Dover Publications, Inc.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki