Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w94 12/15 kur. 2-4
  • Krismasi Inamaanisha Nini Kwako?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Krismasi Inamaanisha Nini Kwako?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1994
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • “Wakati wa Biashara”
  • Je! Ni Lazima Wewe Usherehekee Krismasi?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
  • Ni Nini Kilichoipata Krismasi ya Kidesturi?
    Amkeni!—1993
  • Krismasi—Kwa Nini Inapendwa Sana Katika Japani?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1991
  • Krismasi (Noёl) Ilianza Zamani Sana
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1979
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1994
w94 12/15 kur. 2-4

Krismasi Inamaanisha Nini Kwako?

Wewe ungejibuje? Krismasi ni (1) wakati wa kuwa pamoja na familia yako; (2) wakati wa karamu; (3) wakati wa mambo ya kidini; (4) wakati wa mkazo; (5) wakati wa majonzi; (6) wakati wa matangazo ya kibiashara yenye kutokeza sana.

INGAWA yaonekana kuwa ajabu, kati ya watu zaidi ya 1,000 walioombwa maoni katika Uingereza, ni asilimia 6 tu waliofikiria Krismasi kuwa sherehe ya kidini hasa. Kwa kutofautisha, asilimia 48 walifikiria Krismasi kuwa hasa wakati wa kuwa na familia zao. Kwa kweli, wengi wasisitiza kwamba ni wakati wa pekee kwa watoto. Akionyesha hali ya kawaida msichana mmoja wa miaka 11, alipoulizwa alichopenda sana kuhusu Krismasi, alijibu hivi: “Ule msisimuko, hisi ya furaha, [na] kupeana zawadi.” The Making of the Modern Christmas chakubali kwamba “mikazo mingi ya . . . Krismasi ya ‘kidesturi’ bila shaka inatiliwa nyumbani, familia na hasa watoto.”

Lakini hasa ni katika Jumuiya ya Wakristo ya magharibi ambapo Krismasi inakuwa jambo la familia, wakati watu wa ukoo wakusanyikapo kupeana zawadi. Katika nchi ambapo Kanisa la Orthodoksi la Mashariki linatawala, watu hutilia Ista mkazo zaidi; na bado wakati wa Krismasi huwa kipindi cha mapumziko.

“Wakati wa Biashara”

Krismasi “imekuwa njia ya . . . biashara yenye kutokeza sana,” chasema The New Encyclopædia Britannica. Huenda hakuna mahali pengine jambo hili ni kweli kuliko ilivyo katika Japani.

“Wajapani wameacha kufanya unafiki wowote juu ya dini na wamebadili Krismasi kuwa wakati wa biashara,” laripoti Daily Record la Washington. Krismasi katika Japani, laongeza, “ni sherehe kuu inayokazia sana biashara na isiyokazia sana mambo ya kidini.”

Hata katika nchi ziitwazo za Kikristo, ni vigumu kutambua hiyo “hali ya kidini.” Miaka 40 iliyopita, kijitabu kipingacho Krismasi kiliomboleza: “Krismasi huendelezwa na ulimwengu wa biashara. Ndicho kipindi cha kufanyiza pesa zaidi katika mwaka. Wafanya biashara wanaodai kuwa Wakristo hutazamia majira ya Krismasi, si kwa ajili ya Kristo, bali kwa ajili ya kupata faida ya kifedha.” Maneno hayo ni ya kweli jinsi gani leo! Katika nchi nyingi, si mara nyingi tufikapo robo ya mwisho ya mwaka kabla hatujakumbushwa ni siku ngapi zinazobaki za kununua zawadi za Krismasi inayokuja. Biashara huongezeka zaidi mwaka unapokwisha, robo ya uuzaji ya mwaka mzima ikitokea wakati wa Krismasi.

Krismasi iwe inamaanisha nini kwako, huenda unajiuliza jinsi ilivyoanza. Je, kweli Biblia inaunga mkono kutoa zawadi wakati wa Krismasi? Je, kweli sherehe za Krismasi za kisasa ni za kikristo? Acha tuone.

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 2]

Cover: Thomas Nast/Dover Publications, Inc., 1978

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki