Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w91 12/15 kur. 3-4
  • Krismasi—Kwa Nini Inapendwa Sana Katika Japani?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Krismasi—Kwa Nini Inapendwa Sana Katika Japani?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1991
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Krismasi Ni Mwadhimisho wa Nani?
  • Je! Ni Lazima Wewe Usherehekee Krismasi?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
  • Ni Nini Kilichoipata Krismasi ya Kidesturi?
    Amkeni!—1993
  • Krismasi—Mbona Husherehekewa Hata Mashariki?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1999
  • Mapokeo ya Krismasi—Yana Mianzo Gani?
    Amkeni!—1990
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1991
w91 12/15 kur. 3-4

Krismasi—Kwa Nini Inapendwa Sana Katika Japani?

IMANI katika Baba Krismasi imo sana miongoni mwa watoto katika nchi ya Japani ya Kibuddha-Kishinto. Katika 1989, watoto Wajapani waliandika barua 160,000 kwa Ulimwengu wa Santa (Baba Krismasi) katika Swedeni. Hakuna nchi nyingine iliyopeleka nyingi kuliko hizo. Waliandika barua hizo wakitumaini kutosheleza tamaa ya mioyo yao, iwe ni “Kompyuta ya Michoro” ya kuchezea ya yeni 18,000 (dola 110 za U.S.) au ni video ndogo yenye kuchukulika kwa urahisi ya yeni 12,500 (dola 80 za U.S.).

Kwa wasichana wachanga Wajapani, kufanya urafiki wa mafahamiano pamoja na mvulana Jioni Tangulizi ya Krismasi huwa na maana ya pekee. “Kulingana na utafiti wa wanawake vijana,” yasema Mainichi Daily News, “asilimia 38 walisema kwamba walikuwa wamefanya mipango kwa ajili ya Jioni Tangulizi ya Krismasi mwezi mmoja kimbele.” Wanaume vijana huwa na makusudio ya kisiri ya kutaka kuwa pamoja na rafiki-wasichana wao Jioni Tangulizi ya Krismasi. “Wazo zuri ni kusali pamoja kwa ukimya na rafiki-msichana wako,” likadokeza gazeti la wanaume vijana. “Fanya hivyo katika mahali fulani pa ki-siku-hizi. Uhusiano wenu utakuwa wa ukaribu zaidi upesi.”

Waume Wajapani hutumaini pia kupata nguvu fulani ya kimzungu kwa desturi yao ya Krismasi ya kununua “keki yenye mapambo” wanaporudi nyumbani kutoka kazini. Kuigiza sehemu ya Baba Krismasi (mwenye kuja na zawadi) hudhaniwa kwamba kutalipia kutotunza kwao familia kwa wakati ule mwingine wote wa mwaka.

Kwa kweli, Krismasi imetia mizizi yayo miongoni mwa Wajapani wasio Wakristo. Kwa hakika, asilimia 78 wa wale waliohojiwa katika utafiti wa kikundi cha maduka walisema kwamba wao hufanya jambo la pekee kwa ajili ya Krismasi. Uwiano huo ni mkubwa sana katika nchi ambapo asilimia 1 tu ya wakaaji hudai kuwa na imani katika Ukristo. Ingawa wao hudai kuwa Wabuddha au Washinto, wanastarehe sana kuonea shangwe sikukuu ya “Kikristo.” Katika kalenda yayo, pamoja na sikukuu nyinginezo za Kijapani, Sehemu Maalumu ya Shinto Ise inayojulikana sana huorodhesha Desemba 25 kuwa “siku ya kuzaliwa kwa Kristo.” Hata hivyo, mandhari za wasio Wakristo wakisherehekea sana wakati wa Krismasi, hutokeza swali hili:

Krismasi Ni Mwadhimisho wa Nani?

Webster’s Ninth New Collegiate Dictionary hufafanua Krismasi kuwa “karamu ya Kikristo ya Desemba 25 . . . inayoadhimisha kuzaliwa kwa Kristo.” Imeonwa kuwa wakati wa “Wakristo” wa “kujiunganisha katika hisia zao za shangwe siku ya kuzaliwa kwa Kristo.”

Wale wanaoadhimisha Krismasi kuwa sikukuu ya kidini peke yake huenda wakaona wale wanaoifanya siku hiyo kuwa ya kilimwengu kwa kusherehekea na kwa kutoa zawadi, kuwa wenye kuudhi na hata wenye ukufuru. “Katika Japani ubiashara wetu mkubwa sana hukata shauri kwamba: hakuna Kristo,” akaandika Mwamerika anayeishi Japani. “Kwa mtu wa Magharibi,” akaandika mwingine kuhusu Krismasi ya Kijapani, “kitu kinachokosekana si bata mzinga [ambaye kwa kawaida hapatikani katika masoko ya Kijapani], bali ni ile sehemu iliyo ya maana zaidi, roho ya Krismasi.”

Roho ya Krismasi ni nini basi? Je! ni ile hali ya kuwa na mahubiri ya kanisani pamoja na nyimbo za kusifu, mti holi na mishumaa, ambayo kwa wengi hutumiwa kwa ziara yao ya kwenda kanisani mara moja tu kila mwaka? Au ni ule upendo, hali ya uchangamfu, na kule kutoa zawadi kunakochochea wengi kuwa wakarimu? Je! ni ule utulivu unaoenea vitani wakati askari-jeshi wanapokuwa wakiadhimisha siku chache za “amani duniani”?

Kwa kushangaza, roho ya Krismasi hushindwa mara nyingi kuleta amani hata nyumbani. Kulingana na utafiti wa 1987 huko Uingereza, ilikadiriwa kwamba ‘mizozo ya nyumbani’ ingetokea katika asilimia 70 ya nyumba za Waingereza wakati wa Krismasi mwaka huo. Kupigania pesa kungekuwa kisababishi kikuu. Kunywa kupita kiasi na mtu kukosa kutimiza daraka lake katika familia husababisha mapigano pia.

“Mimi naona kama tunakosa kuelewa jambo fulani kuhusu maana ya kweli ya Krismasi,” akaandika mtu wa Magharibi anayeishi Japani aliyetembelea nchi yake wakati wa majira ya Krismasi ya hivi karibuni. “Kila Des. 25, mimi huhisi tamaa ileile ya kurudia ile Krismasi ya kale ya mtindo wa zamani—sherehe ya kipagani iliyoadhimisha kipupwe cha kikomo cha jua kwa kuabudu miti na kufanya karamu za ukosefu wa adili. Tungali tuna alama za kipagani—mmea misotoo, mti holi, misunobari na kadhalika—lakini kwa njia fulani yaonekana Krismasi haijapata kamwe kuwa sawa na ilivyokuwa tangu iliponyakuliwa na Wakristo na kugeuzwa kuwa sikukuu ya kidini.”

Pasipo shaka, Krismasi ni sikukuu ya kipagani. Wakristo wa mapema hawakuiadhimisha “kwa sababu waliona kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa mtu yeyote kuwa desturi ya kipagani,” chasema The World Book Encyclopedia. Sikukuu za kipagani za Saturnalia na Mwaka Mpya ndizo chanzo cha kule kusherehekea na kubadilishana zawadi.

Ikiwa Krismasi ni ya kipagani kwa asili, ni lazima Wakristo wa kweli waulize swali hili, Je! Krismasi ni ya Wakristo? Ebu tuone yale Biblia husema kuhusu mwadhimisho wa siku ya kuzaliwa kwa Kristo.

[Sanduku katika ukurasa wa 4]

Mwanzo wa Mwadhimisho wa Krismasi

Ingawa maelezo madogo-madogo yaliyo halisi yamepotea kwa sababu ya muda mwingi kupita, madokezo huonyesha kwamba kufikia 336 W.K., namna fulani ya Krismasi ilikuwa ikiadhimishwa na kanisa la Roma. “Tarehe ya Krismasi iliwekwa Desemba 25 makusudi,” yaeleza The New Encyclopœdia Britannica, “ili ile sikukuu kubwa ya mungu wa jua ikose kuwa ya maana.” Hiyo ilikuwa wakati wapagani walipojitoa katika karamu za ukosefu wa adili wakati wa sikukuu za Saturnalia ya Kiroma na pia katika karamu ya Waselti na Wajerumani ya wakati wa kituo cha jua cha mbali zaidi majira ya kipupwe. The New Caxton Encyclopedia husema kwamba “kanisa lilitwaa nafasi hiyo kuzifanya sikukuu hizo kuwa za Kikristo.”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki