Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w89 12/15 uku. 29
  • Muono-Ndani Juu ya Habari

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Muono-Ndani Juu ya Habari
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1989
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • “Si Sehemu ya Ulimwengu”
  • Je! Kuiba Si Dhambi?
  • Ubiashara wa Ibada ya Sanamu
  • Kwa Nini Kuiba Kwaongezeka?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1993
  • Je, Umaskini Ni Sababu Halali ya Kuiba?
    Amkeni!—1997
  • Kwa Nini Nisiibe?
    Amkeni!—1995
  • Dini Inawezaje Kupunguza Mikazo?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1983
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1989
w89 12/15 uku. 29

Muono-Ndani Juu ya Habari

“Si Sehemu ya Ulimwengu”

Wakati watu zaidi ya mia moja elfu waliposongamana katika Stediamu ya Olimpiki ya Berlin ya Magharibi kwa ajili ya kipindi cha mwisho cha Mkutano wa Kanisa Evanjeliko la Ujeremani, msimamizi wa kanisa Helmut Simon aliwahimiza wahusike katika siasa.

Simon aliorodhesha masuala kama utumizi ufaao wa asilimali, kuhifadhi mazingira, kuanzisha mfumo wa kiuchumi ulio wa haki, kumaliza mashindano ya kuunda silaha, na kuondoa ukosefu wa kazi ya kuajiriwa. Alihisi kwamba haya yangekuwa miongoni mwa matisho yasiyotatuliwa ya aina ya binadamu. Ili kuchochea wasikilizaji wake waone uharaka wa masuala haya, karatasi-habari ya Kijeremani Frankfurter Allgemeine Zeitung yaripoti kwamba “yeye alisema kwamba jambo bora zaidi ambalo lingeweza kuipata jumuiya katika Magharibi na Mashariki ni kuhusika kwayo katika siasa.” Simoni aliwatia moyo wahudhuriaji wote “kufikiria mhusiko huo kuwa wajibu na wauone mkutano wa kanisa kuwa haki za harakati ya Kiprotestanti ya wenyewe kwa wenyewe.”

Hata hivyo, je! Wakristo wa kweli waweza kwa kufaa kujihusisha katika harakati hizo za kisiasa? Je! Yesu hakusema kwamba wafuasi wake “si sehemu ya ulimwengu, kama vile [yeye hakuwa] sehemu ya ulimwengu”? (Yohana 17:16, NW) Yesu alifundisha wafuasi wake kusali Ufalme wa Mungu kuwa ndio tumaini halisi la pekee kwa aina ya binadamu. Kwa nini? Kwa sababu, kama vile nabii Danieli alivyotabiri zamani za kale, Ufalme wa Mungu ‘utavunja na kuharibu’ serikali hizi za kilimwengu zenye kukosa mafanikio, “nao utasimama milele na milele.”—Danieli 2:44.

Je! Kuiba Si Dhambi?

Je! kuiba ni dhambi? Si sikuzote, kulingana na Ivo Storniolo padri Mkatoliki. O Estado de S. Paulo, karatasi-habari moja ya Kibrazili, yanukuu Storniolo kuwa akitaarifu kwamba “Mungu hubariki na kuhalalisha uibaji wenye kufanywa na walio maskini.” Baadaye, yeye alisema alikuwa akirejezea “maskini wale tu ambao huiba ili waweze kuendelea kuwa hai.” Kwa maoni ya padri huyu, vijana wasiotii sheria ambao huiba hawapasi kuadhibiwa, kwa maana wao ‘wamenyang’anywa hapo kwanza na walio na nguvu.’ “Kwa maoni yake,” yasema O Estado, “akina marginais (watupwanje au watu waonwao kuwa hawafai kati ya jamii, ambao kwa ujumla ni maskini, wasioajiriwa kazi] wamo pia ‘miongoni mwa wachaguliwa wa Mungu.’”

Je! Biblia yaunga mkono njia hii ya kusababu mambo? Hata kidogo. Ingawa Yesu aliwatia moyo wafuasi wake wawaonyeshe wahitaji huruma, hakusema kamwe kwamba matatizo ya kijamii kama vile umaskini, yalikuwa kitetezi cha haki ya kuiba. Bali, kama vile mtume Paulo alivyoandika: “Mtu yeyote aliyekuwa mwizi ni lazima aache kuiba; badala ya hivyo apaswa ajitahidi sana mwenyewe kwenye kazi fulani ya ufuataji haki kwa mikono yake mwenyewe ili kwamba apate kuwa na kitu cha kushiriki pamoja na wale walio katika uhitaji.”—Waefeso 4:28, The New Jerusalem Bible.

Ubiashara wa Ibada ya Sanamu

Wonyesho wa kitaifa wa vitu na fanicha za kidini, uliofanywa kaskazini mwa Italia, uliruhusu kampuni 97 zionyeshe bidhaa zao. Miongoni mwa vitu vilivyoonyeshwa kilikuwamo kibanda cha maungamo chenye kufyonza mvumo wa sauti kikiwa pamoja na kichungi cha kuzuia viini, na kiti kilichoshindiliwa vitu vya kustarehesha. Pia mishumaa fulani iliyotakaswa isiyotoa harufu, ya aina ya “Papa John” pamoja na vihesabu-wakati vya muda wa saa 40; milio ya kengele za kanisa iliyorekodiwa kwa njia ya kompyuta; masanduku ya kuwekea sadaka yenye kinga imara yaliyo “kama makasha”; vidio za kuelimisha watoto (yaani, Biblia kulingana na Johnny); na mikoba ya ngozi bandia yenye vyombo vihitajiwavyo ili kufanya Misa ya peupe.

Mtindo wa kikasisi haukukosa kutiwa katika onyesho hilo. “Wabuni [wawili] wa mitindo ya kidini” waliieleza karatasi-habari ya Kiitalia La Stampa kwamba ‘zaidi ya yote, mapadri vijana wataka kuwa na sura mpya, nguo za sufi zenye kutakata zilizotiwa madoido ya mshono wa Kijeremani, zilizonyooka, zikiwa zinafanana, zisizo na rangi-rangi lakini zivutie. Nazo asante zimwendee Mungu, biashara yaendelea vizuri wee.’

Utalii wa kidini unafanyiza pia mapato ya biashara. “Kila mwaka kuna watu milioni 15 wenye kusafiri kwa sababu za kidini, na waendeshaji wa safari za utalii, walio au wasio wa kidini, hushindana ili wawapate watu hao,” yaripoti karatasi-habari ya Kiitalia La Repubblica. Ikitoa kielezi cha jambo hili, karatasi-habari ya Kiitalia Il Messaggero yasema kuhusu basilika ya “Mtakatifu” Anthony katika Padua kwamba “watu hutumbukiza mamilioni [ya pesa] si katika hoteli tu bali hasa katika masanduku ya pesa ya basilika kwa ajili ya picha takatifu na zawadi za kuwakumbuka watoaji.”

Si ajabu kwamba wakati Jumuiya ya Wakristo, pamoja na dini yote bandia, iharibiwapo, ‘wauza-bidhaa wasafiri wa dunia watatoa machozi na kuomboleza juu ya yeye.’ Kama vile Ufunuo 18:11, NW, uendeleavyo kusema: “Hakuna wa kununua tena bidhaa yao kamili.”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki