Kuongolewa kwa Konstantino—Kuwa Nini?
LILE dai la kwamba mmaliki Mroma Konstantino aliongolewa limewapendeza wanafunzi wa dini kwa muda mrefu. Kulingana na usimulizi wake mwenyewe, katika jioni yenye kutangulia pigano moja katika 312 W.K., ambalo yeye alishinda, Konstantino mpagani aliona njozi ya msalaba wenye shime hii: “Kwa [ishara] hii shinda.” ‘Aliongolewa’ muda mfupi baada ya hapo (katika 313 W.K.) na akakomesha mnyanyaso wa Wakristo katika milki ya Kiroma. Konstantino alitia moyo kwamba namna ya Ukristo uliokuwapo wakati huo uwe dini ya Serikali, na hata akajiingiza katika magomvi ya ndani kanisani. Hata hivyo, alifanya vitendo vilivyotia shaka juu ya ukweli wa kuongolewa kwake na hakubatizwa mpaka muda mfupi tu kabla ya kifo chake miaka 24 baadaye.
Katika makala moja katika Bible Review, Stanley A. Hudson ambaye ni mwanafunzi mwenye kusomea asili ya sarafu mbalimbali na shahada ya theolojia, alifunua jinsi sarafu zilizoundwa wakati wa utawala wa Konstantino zasaidia kutoa habari fulani za kusisimua kuhusu jambo hili. Hadi wakati wa Konstantino, ilikuwa kawaida ya sarafu za Kiroma kuonyesha miungu maarufu ya Kiroma. Lakini Hudson aliripoti kwamba baada ya kuongolewa kwa Konstantino, maneno ya kipagani yalizidizidi kutoonyeshwa—isipokuwa kisa kimoja. Sarafu zenye kuonyesha Sol, yule mungu jua—mwenye kupendelewa zaidi na Konstantino hapo kwanza—ziliundwa kwa wingi sana. Kwa nini?
Hudson alidokeza mawezekano mawili. Kwanza, huenda ikawa kuongolewa kwa Konstantino kulitukia kidato kwa kidato—ajapokuwa aliona njozi yake ya kutazamisha. Au huenda ikawa Konstantino kwa kweli alivurugika kudhania Sol ni Yesu. Ni jambo la kawaida hata leo kuchanganya imani za namna tofauti-tofauti. Kwa kielelezo, katika Amerika ya Kilatini, miungu ya kike Pacha-Mama na Tonantzin iliyokuwako kabla ya wakati wa Columbus ingali yaabudiwa kwa kisingizio cha kwamba mwenye kuabudiwa ni Bikira Mariamu. Kwa njia iyo hiyo, huenda Konstantino akawa aliabudu Sol kwa kisingizio cha kuabudu Yesu.
Uchanganyi huo wa imani ungeeleza kwa nini Desemba 25, ‘ile siku ya kuzaliwa kwa jua lisiloshindika,’ ilichaguliwa kuwa siku ya kukumbuka uzaliwa wa Yesu. Ungetusaidia pia tuone kwa nini juu ya sarafu iliyoundwa ili kukumbuka kifo cha Konstantino pana maandishi yasemayo “DV Constantinus” (“Konstantino wa Kimungu”). Hii yaonyesha kwamba, ajapoongolewa na kubatizwa hatimaye, Konstantino alionwa kuwa mungu baada ya kifo chake, sawasawa na wamaliki wapagani waliomtangulia.
Hisani ya Picha katika ukurasa wa 7]
The Metropolitan Museum of Art. Bequest of Mrs. F. F. Thompson, 1926 (26.229)