Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w90 4/1 uku. 31
  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
  • Habari Zinazolingana
  • Tauni za Yehova juu ya Jumuiya ya Wakristo
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
  • Saa ya Hukumu ya Mungu Imewasili
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1989
  • Mambo Makuu Katika Kitabu cha Ufunuo—I
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2009
  • Siri Takatifu ya Mungu—Upeo Wayo Wenye Utukufu!
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
w90 4/1 uku. 31

Maswali Kutoka kwa Wasomaji

◼ Mipulizo ya kimalaika ya tarumbeta saba za Ufunuo ilianza kuvuma wakati gani?

Katika Ufunuo sura 8, 9, na 11, twasoma juu ya malaika saba waliopuliza tarumbeta saba, wakitangaza ujumbe wa tauni za kadiri kubwa juu ya visehemu vya ainabinadamu. Hizi zawakilisha mipigo ya mbiu ya hukumu za Yehova ambayo imetangazwa na watu wa Yehova katika wakati wote wa mwisho kuanzia sana-sana na mkusanyiko wa Cedar Point wa 1922,—Ona Revelation—lts Grand Climax At Hand, sura ya 21 hadi ya 23 na sura ya 26.

Mipulizo ya kwanza minne hufichua hali ya kiroho ambayo imekufa ya kisehemu cha Jumuiya ya Wakristo cha “dunia” na “bahari,” na pia hali ya kuanguka kwa makasisi na giza la kiroho la Jumuiya ya Wakristo.—Ufunuo 8:7-12, NW.

Historia huonyesha kwamba kufichua peupe mambo haya ya uhakika kulianza hasa kabla ya 1922. Kwa kielelezo, hotuba “Mamilioni Wanaoishi Sasa Huenda Wasife Kamwe,” iliyotolewa mara ya kwanza katika 1918 na kuchapishwa kwa namna ya kijitabu katika 1920, ilisimulia juu ya kushindwa kwa Jumuiya ya Wakristo na juu ya mwisho unaokaribia wa ulimwengu huu. The Golden Age la Septemba 29,1920, lilifichua wazi Jumuiya ya Wakristo kuwa mwasherati, mhadaaji mwenye kusema uwongo, na mwongozi mbaya wa watu.

Basi, kwa nini kitabu Revelation Climax kinasema kwamba kwenye mkusanyiko wa Cedar Point katika 1922 ndipo tu tarumbeta nne hizi zilianza kupulizwa? Kwa sababu wakati huo ndipo wito ulipotolewa kwamba “tangazeni, tangazeni, tangazeni Mfalme na Ufalme,” ukitoa motisha kubwa kwenye utendaji wa kuhubiri. Toleo la Novemba 1, 1922 la Mnara wa Mlinzi (Kiingereza), lasema hivi: “Marafiki walichukua kwamba wazo kuu la mkusanyiko lilikuwa kwamba pendeleo halisi na wajibu wa waliotakaswa walio duniani sasa ni kutangaza kuwapo kwa Bwana, Mfalme wa wafalme, na kwamba ufalme upo hapa, na kwamba hili ndilo jambo la maana zaidi kwao kufanya.”

Yapasa pia iangaliwe kwamba ingawa hizi jumbe zote nne za hukumu zimetangazwa na Mashahidi wa Yehova tangu 1922, kila mmoja ulipokea motisha nyingine pia kutokana na kukubaliwa kwa maazimio manne kwenye mikusanyiko iliyofanywa kati ya 1922 na 1925. Makumi ya mamilioni ya nakala za maazimio haya ziligawanywa baada ya hapo kwa namna iliyopigwa chapa, zikifichua sana ufu wa kiroho wa Jumuiya ya Wakristo.—Ona kitabu Revelation Climax, ukurasa 133, fungu la 15.

Mipulizo ya tarumbeta tatu za mwisho yahusisha “ole.” (Ufunuo 8:13) Ni ‘tofauti na mipulizo ya tarumbeta nne za kwanza katika maana ya kwamba zahusiana na matukio hususa. Mpulizo wa tarumbeta ya tano wahusiana na kuachiliwa kwa watu wa Mungu kutoka katika “abiso” katika 1919. Ya sita yahusu “jeshi la wapanda farasi” na kampeni kubwa sana ya kuhubiri kimataifa iliyoanza katika 1922. Ya saba yakatamana na kuzaliwa kwa Ufalme wa Mungu katika 1914.—Ufunuo 9:1-19; 11:15-19, NW.

Kila moja la matukio haya lilimletea ole Shetani na ulimwengu wake. Kuachiliwa kwa wapakwa-mafuta katika 1919 kutoka katika abiso ya kutotenda kuliuma makasisi wa Jumuiya ya Wakristo na kuonyesha kukataliwa kwayo kabisa na Yehova. Kuanzia 1922 hadi leo, hilo jeshi kubwa sana la wapanda farasi limeua Jumuiya ya Wakristo, kwa uneni wa kitamathali, likifichua hali yake iliyokufa na kuonya juu ya uharibifu wake unaokuja. Na baada ya kuzaliwa kwa Ufalme katika 1914, Shetani alitupwa nje ya mbingu, akichochea matata yenye uharibifu miongoni mwa ainabinadamu. Karibuni UfaIme utaondoa jamii ya kibinadamu yenye kuonekana kana kwamba ina uthabiti ambayo Shetani amejenga (dunia), na ufutilie mbali ainabinadamu yenye uasi (bahari) kwenye Har-Magedoni.—Ufunuo 11:17-12:12; 21:1, NW.

Kwenye mkusanyiko wa Cedar Point katika 1922, “ole” zote tatu zilipata kuonekana wazi kwa ulimwengu kwa ujumla. Kampeni ya kuhubiri iliyoanzishwa wakati huo ilionyesha wazi kwamba “nzige” walikuwa wametoka katika “abiso” na kwamba shambulizi la “jeshi la wapanda farasi” lilikuwa likiendelea. Na wito wenye kuchochea wa kutangaza Mfalme na Ufalme ulipatana kikamili na mpulizo wa tarumbeta ya saba. Toleo la Machi 1, 1925 la Mnara wa Mlinzi (Kiingereza) lilieleza kwamba matukio katika 1914, 1919, na 1922 yalitabiriwa katika Ufunuo sura ya 12. Huu ulikuwa uelewevu wa kina kirefu zaidi wa kuzaliwa kwa Ufalme, nao ulitangazwa kwa uaminifu na Mashahidi wa Yehova. Kwa kuongezea, kutangazwa kwa habari hizi zenye kuleta tauni kulipokea motisha kubwa kutokana na kukubaliwa halafu kugawanywa kwa maazimio yenye nguvu nyingi wakati wa mikusanyiko iliyofanywa kuanzia 1926 hadi 1928.—Ona Revelation—lts Grand Climax At Hand, kurasa 147, 149, 172.

Hivyo, kupulizwa kwa tarumbeta saba kulianza katika 1922 na kukaendelea sana katika miaka ya 1920. Tangu wakati huo, watu wa Yehova wameshirikiana bila hofu na malaika katika kuambia ainabinadamu yote kwamba Jumuiya ya Wakristo imekufa kiroho, makasisi wayo ni viongozi walioanguka, na karibuni hiyo na sehemu nyingine yote ya ulimwengu huu wa kishetani itaharibiwa.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki