Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w90 7/1 kur. 5-6
  • Kuiokoa Dunia Isiangamizwe

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuiokoa Dunia Isiangamizwe
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Kuiangamiza Dunia
  • Dunia Iliyookolewa Isiangamizwe
  • Kutoa Onyo la Kimungu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1981
  • Je, Mwisho Umekaribia?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2015
  • Binadamu Anaifanya Dunia Nini?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
  • Kuokolewa kwa Dunia Kwakaribia Sana
    Amkeni!—1993
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
w90 7/1 kur. 5-6

Kuiokoa Dunia Isiangamizwe

WAKATI mmoja zamani katika historia ya kibinadamu, Mungu aliiokoa dunia isiangamizwe na wanadamu. Alifanya hivyo kwa njia ya gharika ya tufe lote katika siku za Noa. Hatuna maandishi ya kuonyesha kwamba wanadamu walikuwa wakiharibu mazingira halisi huko nyuma. Lakini dunia ilikuwa ikiangamizwa kwa njia nyingine kwa kadiri ambayo Mungu alihisi uhitaji wa kutenda kwa ukali kabisa.

Biblia huripoti hivi: “Dunia ikaja kuangamizwa machoni pa Mungu wa kweli na dunia ikaja kujazwa jeuri. Kwa hiyo Mungu akaiona dunia na, tazama! ilikuwa imeangamizwa, kwa sababu mnofu wote ulikuwa umeangamiza njia yao duniani.” (Mwanzo 6:4, 11, 12, NW) Ndiyo, katika siku ya Noa Mungu aliiona dunia kuwa imeangamizwa kwa sababu ya jeuri na uovu wa ainabinadamu.

Vivyo hivyo, Israeli wa kale walipoanza kutwaa umiliki wa Bara la Ahadi, Mungu alionya hivi: “Hamtaitia unajisi nchi ambayo mwaiketi; kwa kuwa damu huitia nchi unajisi . . . Kwa hiyo msiitie unajisi nchi.” (Hesabu 35:33, 34) Hivyo, Kaanani iliangamizwa kwa sababu ya hatia ya damu ya wakaaji wayo. Kielelezo kibaya sana cha jambo hilo kilikuwa zoea lao la kudhabihu watoto wachanga kwa miungu yao.

Pia Wakanaani walikuwa wakosefu wabaya sana wa adili, na hilo pia liliathiri maoni ya Mungu juu ya bara hilo. Aliwaonya Israeli hivi: “Msijijitie unajisi katika mambo hayo [mazoea ya kukosa adili] hata mojawapo; kwa maana hizo taifa nitakazozitoa mbele zenu zimekuwa najisi kwa mambo hayo yote; na hiyo nchi imekuwa najisi; . . . na hiyo nchi yatapika [itatapika, NW] wenyeji wake na kuwatoa.” (Walawi 18:24, 25) Ukosefu wa adili na umwagaji wa damu uliangamiza Kanaani kwa kadiri ambayo Mungu aliyaharibu mataifa ya Kikanaani.

Kuiangamiza Dunia

Namna gani leo? Je! sisi pia hatuishi katika enzi ya jeuri, umwagaji wa damu, na ukosefu wa adili usiozuiliwa? Hata binadamu afanye nini kujaribu kurekebisha hasara ambayo amefanyia dunia halisi, yeye hawezi kamwe kuwarudishia uhai watu wanaokadiriwa kuwa milioni mia moja ambao wamekufa katika vita vyake katika karne hii; wala hawezi kurudisha mamilioni waliouawa na wahalifu au mihanga wengi hohehahe ambao huuawa na njaa. Kwa uhakika, hawezi kurudisha vile vitoto visivyozaliwa vinavyokadiriwa kuwa milioni 40 hadi 60 ambavyo uhai wavyo hukomeshwa kwa kutolewa mimba kila mwaka. Je! sisi twaweza kutia shaka kwamba machoni pa Mungu dunia inaangamizwa na mambo ya jinsi hiyo—sembuse na ukosefu wa adili ambao umeenea sana leo?

Kufikiri kuzuri kwatuambia kwamba ni lazima Mungu atende karibuni ili kuiokoa dunia na utendaji wa binadamu wa kuiangamiza, na unabii wa Biblia wahakikisha jambo hilo. Lakini yeye atafanya nini? Biblia husema kwamba ‘atawaangamiza wale wanaoangamiza dunia.’ (Ufunuo 11:18, HNWW; linganisha Mathayo 24:3-14.) Kama vile mwenye kupangisha nyumba humtupa nje mpa-ngaji mharibifu, ndivyo Mungu ‘atakavyowatupa nje’ wale wanaoangamiza uumbaji wake mzuri, dunia.

Biblia hutaarifu hivi: “Bali waovu watatengwa na nchi, nao wafanyao hila watang’olewa.” (Mithali 2:22) Kitendo hicho cha kimungu kinachokuja huitwa na Biblia Har–Magedoni. (Ufunuo 16:16) Yesu pia alikiita “dhiki kubwa, ambayo haijatokea namna yake tangu mwanzo wa ulimwengu hata sasa, wala haitakuwapo kamwe.” (Mathayo 24:21) Itakuwa kubwa hata kuliko Gharika.

Je! huu ni utatuzi wa kupita kiasi au usio haki? Sivyo, Mungu, akiwa ndiye Muumba wa dunia, ana haki ya kuamua ni nani ataikaa. Pia yeye ana haki ya kumchukua binadamu kuwa mwenye daraka kwa vitendo vyake. Zaidi ya hilo, Mungu akiruhusu binadamu aendeleze mwendo wake bila kuangaliwa, dunia itaangamizwa kwa kila mtu, na uhai utakuwa usiowezekana. Kwa upande mwingine, kwa “kuwaangamiza wale wanaoangamiza dunia,” Mungu ahifadhi urithi wetu wa kidunia kwa wenye kuthamini. Biblia huahidi hivi: “Maana wanyofu watakaa katika nchi, na wakamilifu [wasio na lawama, NW] watadumu ndani yake.”—Mithali 2:21.

Kwa msaada wa Mungu, mamilioni wamepata imara ya kujionyesha kuwa wasio na lawama kwa sababu wao wataka kubakizwa ili waonee shangwe uumbaji wa Mungu. Pia wao hufuata viwango vya juu vya maadili vya Mungu na huepuka jeuri na hatia ya damu hata kwa njia isiyo ya moja kwa moja. Hivyo, wao si waangamizi wa dunia katika njia hiyo yenye umaana.

Dunia Iliyookolewa Isiangamizwe

Sasa watu hao wana tazamio lenye shangwe la kuiona dunia ikigeuzwa kutoka hali yayo ya sasa ya kuangamizwa iwe paradiso yenye afya. Naam, hata miili yao itasafishwa sana, itakaswe yale matokeo ya uangamivu wa dhambi. Kitabu cha mwisho cha Biblia huonyesha uandalizi wa Mungu wa kufanya yote haya yawezekane kuwa kama “mto wa maji ya uhai” ya ufananisho. Kila upande wa mto huu, “kulikuwa na miti ya uhai ikifanyiza mazao kumi na mawili ya tunda, ikitoa matunda yayo kila mwezi. Na majani ya miti yalikuwa kwa ajili ya kuponeshwa kwa mataifa.”—Ufunuo 22:1, 2, NW.

Njozi hiyo yenye uvuvio ni uhakikisho kamili kwamba Mungu ataiokoa dunia na ainabinadamu iliyomo isiangamizwe. Unabii mwingine mbalimbali hutoa mwono wa mapema wa dunia hiyo iliyorudishiwa hali nzuri. Kwa kielelezo, fikiria mwono wa mapema wa Isaya ambao umeelezwa kishairi: “Nyika na mahali palipo ukiwa patafurahi; jangwa litashangilia na kuchanua maua kama waridi. Litachanua maua mengi, na kufurahi, naam, kwa shangwe na kuimba.” (Isaya 35:1, 2) Wakati huo hakutakuwa na bahari zilizochafuliwa, udongo wa juu ulioangamizwa, wala halianga yenye sumu.

La maana zaidi, dunia haitaangamizwa na jeuri, umwagaji wa damu, wala ukosefu wa adili. Ni wale tu wenye kustahi Mungu, viwango vyake, na uumbaji wake watakaokuwapo. (Ufunuo 21:7, 8) Sasa sikiliza matokeo matukufu ya mambo yote hayo: “[Mungu] atapangusa kabisa machozi kutoka macho yao, na kifo hakitakuwapo tena, wala hakutakuwapo kuomboleza wala kuguta wala umivu tena. Vitu vya kwanza vimepitilia mbali. . . . ‘Tazama! mimi ninafanya vitu vyote kuwa vipya.’”—Ufunuo 21:4, 5, NW.

Lo, ni tokeo lenye kufurahisha kama nini! Sisi twaterema kama nini kwamba karibuni Mungu ‘atawaangamiza wale wanaoangamiza dunia’! Na ahadi hizi zenye uvuvio zatusukuma kama nini tutake kutumikia Mungu ambaye ataiokoa dunia isiangamizwe na kuifanya iwe makao ya kiparadiso kwa ainabinadamu yenye moyo ufaao!

[Blabu katika ukurasa wa 6]

Biblia husema kwamba Mungu ‘atawaangamiza wale wanaoangamiza dunia.’ —Ufunuo 11:18, HNWW

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki