Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w90 12/15 kur. 3-4
  • Bethlehemu—Je! Ni Kifananisho cha Umoja na Upendo wa Kikristo?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Bethlehemu—Je! Ni Kifananisho cha Umoja na Upendo wa Kikristo?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
  • Habari Zinazolingana
  • Ukweli Ni Nini Juu ya Bethlehemu na Krismasi?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
  • Je, Krismasi Imempoteza Kristo?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1998
  • Desturi za Krismasi-Je, Ni za Kikristo?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2000
  • Kuzaliwa kwa Yesu—Masimulizi Halisi
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1998
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
w90 12/15 kur. 3-4

Bethlehemu—Je! Ni Kifananisho cha Umoja na Upendo wa Kikristo?

“BETHLEHEMU . . . ni uthibitisho wa upendo usioisha, ni somo la unyenyekevu.”—Maria Teresa Petrozzi, mtungaji wa kike wa kitabu Bethlehem.

Je! Bethlehemu inamaanisha kitu kama hicho kwako? Labda ndivyo, kwa kuwa mamia ya mamilioni ya watu wenye moyo mweupe wanaopenda amani ulimwenguni pote wanatazama kwa kicho kingi kuelekea Bethlehemu, hasa wakati wa Krismasi. Wanafahamu kwamba jiji dogo hili la Mashariki ya Kati ndipo alipozaliwa “Mwana-Mfalme wa Amani,” Yesu Kristo. Kwa karne nyingi wasafiri wamemiminika hapa kutembelea pamoja pa mahali patakatifu zaidi pa Jumuiya ya Wakristo, na labda kupaheshimu kwa ibada. Hapo ndipo Pango la Uzaliwa, mahali pa kimapokeo pa uzaliwa wa Yesu Kristo. Ni katika lile jengo kubwa, la kihistoria linaloitwa Kanisa la Uzaliwa.—Isaya 9:6, NW; Mathayo 2:1.

Hata hivyo, kwa uhalisi, je! sehemu hizo takatifu za kimapokeo zimetumika kuwa mahali pakuu pa umoja, upendo, na unyenyekevu wa Kikristo? Wewe unakata shauri gani kwa mambo yanayofuata?

Mwandikaji Mkatoliki Maria Teresa Petrozzi anaeleza hivi katika Bethlehem: “Kuanzia karne ya 16, [Bethlehemu] paliteseka kutokana na mapambano makali ya umwagaji damu kati ya Walatini [Wakatoliki Waroma] na Wagiriki [waamini wa Orthodoksi ya Kigiriki] kwa kupigania uongozi katika lile kanisa la Uzaliwa.” Haya ‘mapambano ya umwagaji damu’ kwa ajili ya kupata uongozi mara nyingi yalihusiana na ile nyota ya fedha katika lile Pango la Uzaliwa, ambalo liko chini ya ardhi, chini ya Kanisa la Uzaliwa. Nyota hii inasemwa kuwa inatia alama mahali halisi pa uzaliwa wa Kristo. R. W. Hamilton anaripoti hivi katika kitabu chake The Church of the Nativity, Bethlehem: “Inajulikana vema kwamba mawili ya masuala yaliyokuwa katika ubishi kati ya Ufaransa na Urusi ambao uliongoza kwenye ile vita ya Krimea yalihusu madai ya ushindani juu ya kumiliki funguo za milango mikubwa ya basilika na chumba kilicho chini ya kanisa [Pango la Uzaliwa], na kuhusu wizi wa kifumbo uliotukia usiku mmoja katika 1847 wa ile nyota ya fedha yenye mwandiko wa Kilatini ulioingizwa katika zege moja la marimari chini ya madhabahu ya ule Uzaliwa.”

Kutokana na mahitilafiano yenye kuendelea kati ya madhehebu mbalimbali muda wa karne zote kuhusu haki za kuwa katika mahali hapa mbalimbali, “haki za kila madhehebu sasa zinaagizwa zifuatwe kwa uangalifu. Kwa mfano, kati ya zile taa 53 zilizo katika lile pango, Wafrancisca wanaruhusiwa 19. Madhabahu ya Uzaliwa ni mali ya Wagiriki, na Walatini hawaruhusiwi kufanya ibada zao hapo.”—Historical Sites in Israel.

Wakati wa Krismasi, ikiwa hali ya kisiasa inaruhusu, kila mmoja wa mitaa ya kidini iliyopo ya Jumuiya ya Wakristo unafanya Misa yao wenyewe ya Krismasi na kuwa na msafara kupitia Bethlehemu. Katika Desemba 24 na 25, Walatini wanakuwa na msafara na Misa ya usiku-kati katika Kanisa la Mtakatifu Catherine, kando ya Kanisa la Uzaliwa, ambalo sasa linashirikiwa na makanisa ya Orthodoksi ya Ugiriki na ya Armenia. Katika Januari 6, makanisa ya Orthodoksi ya Ugiriki, ya Siria, na ya Kikopti yanaadhimisha Misa zao za Krismasi. Katika Januari 18, Misa ya Krismasi ya Orthodoksi ya Armenia inafanywa, kukiwa na msafara katika Januari 19.

Je! yaliyotangulia yanadokeza kwamba sehemu takatifu za kimapokeo za Bethlehemu ni ‘uthibitisho wa upendo usioisha, somo la unyenyekevu’? Kwa kuongezea, je! zinaonyesha ukweli juu ya hali za uzaliwa wa Yesu? Kwa mfano, yeye alizaliwa wakati gani? Je! kwa kweli alizaliwa katika lile ambalo sasa ni Pango la Uzaliwa? Na je! wewe au mtu mwingine yeyote mnapaswa kupaheshimu kwa ibada mahali pa kuzaliwa kwake?

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 3]

Pictorial Archive (Near Eastern History) Est.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki