Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w91 6/15 kur. 27-30
  • Kuchunguza Nyuso za Johari ya Mungu Isiyohesabika Bei Biblia!

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuchunguza Nyuso za Johari ya Mungu Isiyohesabika Bei Biblia!
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1991
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Maandiko ya Kiebrania
  • Maandiko ya Kigiriki ya Kikristo
  • Jinsi ya Kutafuta Maandiko Katika Biblia Yako
    Habari Zaidi
  • Funzo Namba 3—Kupima Matukio Katika Mkondo wa Wakati
    “Kila Andiko, Lenye Pumzi ya Mungu, Lafaa”
  • “Kila Andiko, Lenye Pumzi ya Mungu, Lafaa”
    “Kila Andiko, Lenye Pumzi ya Mungu, Lafaa”
  • Mfululizo wa Matukio
    Biblia—Ina Ujumbe Gani?
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1991
w91 6/15 kur. 27-30

Kuchunguza Nyuso za Johari ya Mungu Isiyohesabika Bei Biblia!

KATIKA 1867 mkulima mmoja wa Afrika Kusini jina lake Schalk van Niekerk alikuwa akitazama watoto wakichezea mawe fulani. Jiwe moja hasa lililo jangavu na maridadi lilivuta macho yake. “Waweza kulichukua, ukipenda,” akasema mama ya watoto hao. Ingawa hivyo, Van Niekerk alipeleka jiwe hilo kwa mtaalamu wa madini likachunguzwe. Kumbe watoto hao hawakung’amua kwamba walikuwa wakichezea almasi kubwa yenye thamani ya pauni 500!

Je! yawezekana kwamba wewe pia una johari isiyohesabika bei bila kung’amua hivyo? Kwa kielelezo, watu wengi wana Biblia, kwa maana hicho ni kitabu chenye kuuzwa kupita vyote vya wakati wowote, kipatikanacho kikiwa kizima au kwa sehemu katika lugha zaidi ya 1,900. Hata hivyo, watu walio wengi hawajaisoma Biblia na hivyo wao wajua kiasi kidogo cha yaliyomo.

Biblia hudai kuwa ‘ina pumzi ya Mungu’ na kwa hiyo ni Neno la Mungu. (2 Timotheo 3:16; linganisha 1 Wathesalonike 2:13.) Hiyo ndiyo mali iliyo ya thamani kubwa zaidi ya ainabinadamu. Kwa njia ya hiyo, sisi hujifunza jinsi ya kupata yaliyo bora zaidi sasa maishani na, la maana zaidi, jinsi ya kupata uhai wa milele! (Yohana 17:3, 17) Je! kitu chochote kingeweza kuwa chenye thamani kuliko hicho?

Hata hivyo, ili kuthamini johari hiyo na nyuso zayo zote, ni lazima mtu afahamiane nayo. Kwa kutupa jicho mara ya kwanza, huenda hilo likaonekana kuwa jambo gumu sana. Ingawaje, Biblia ni mkusanyo wa vitabu tofauti 66. Vitabu hivyo vina nini? Je! kuna sababu fulani ya mpangilio ambao vyaonekana vikiwa nao? Ikiwa ndivyo, mtu aweza kupataje vifungu vya pekee katika Biblia?

Kuzoelea Biblia ni jitihada. Lakini kama vile johari halisi, Biblia ina umbo la pande mbalimbali zenye upatano na utaratibu. Twaweza kuona hilo tukifikiria kifupi yaliyomo.

Maandiko ya Kiebrania

—Yenye Kuelekeza kwa Kristo

Kwa ujumla Biblia hugawanywa katika “Agano la Kale” na “Agano Jipya.” Ingawa hivyo, hayo ni majina yasiyofaa yenye kutoa wazo la kwamba “Agano la Kale” limekuwa kuukuu na lina thamani kidogo. Jina lifaalo zaidi kwa sehemu hiyo ya Andiko lingekuwa Maandiko ya Kiebrania, kwa kuwa sehemu hiyo iliandikwa hapo kwanza sana-sana katika lugha ya Kiebrania. “Agano Jipya” liliandikwa katika Kigiriki katika karne ya kwanza W.K.; hivyo, kwa kufaa zaidi huitwa Maandiko ya Kigiriki ya Kikristo.

Kitabu cha kwanza cha Biblia, Mwanzo, huanzia enzi nyingi za wakati uliopita ambapo Mungu aliumba mbingu na dunia na baadaye akaanza kutayarisha dunia ili ikaliwe na wanadamu. Mume na mke wa kwanza wawili wa kibinadamu waliumbwa wakamilifu; hata hivyo, walichagua mwendo wa dhambi, kukiwa na matokeo yenye msiba kwa wazao wao. Hata hivyo, kama vile johari yenye kuonwa katika nuru hafifu, Biblia huandaa king’ao cha tumaini kwa ajili ya ainabinadamu iliyoanguka dhambini: “mbegu” ambayo hatimaye itaondoa matokeo ya dhambi na kifo. (Mwanzo 3:15, NW) Mbegu huyo atakuwa nani? Mwanzo waanza kufuatisha ukoo wa Mbegu huyo mwenye kuja, ukikaza fikira juu ya maisha za watu fulani wa mababu waaminifu wa Mbegu huyo, kama vile Abrahamu, Isaka, na Yakobo.

Ndipo Kutoka hueleza kuzaliwa kwa Musa. Kwa njia nyingi maisha ya Musa hutangulia kuwa kivuli cha yale ya Mbegu huyo mwenye kuja. Baada ya mapigo kumi, Israeli wafanya Mwondoko mkubwa kutoka Misri na kusimamishwa imara wakiwa taifa chaguliwa la Mungu kwenye Mlima Sinai. Mambo ya Walawi, kama jina hilo lionyeshavyo, chatokeza virekebi vya Mungu kwa ukuhani wa Kilawi katika Israeli. Hesabu chaeleza juu ya pindi ambapo Waisraeli walihesabiwa (kwa uhesabu wa idadi ya watu) na juu ya matukio ya wakati wa safari ya Israeli jangwani. Na sasa, wakiwa tayari kuingia Bara Lililoahidiwa, Israeli wapokea mahimizo ya mwisho ya Musa. Hiyo ndiyo habari ya Kumbukumbu la Torati. Akielekeza kwenye Mbegu inayokuja, Musa ahimiza taifa lisikilize ‘nabii ambaye Mungu ataondokesha.’—Kumbukumbu 18:15.

Vile vitabu vya kihistoria vyafuata. Sana-sana hivyo vimo katika mpangilio wenye kufuatana kimatukio. Yoshua hueleza kushindwa na kugawanywa kwa Bara Lililoahidiwa. Waamuzi husimulia matukio ya kutazamisha ya miaka iliyofuata wakati ambapo Israeli wasimamiwa na mfululizo wa waamuzi. Ruthu chaeleza juu ya mwanamke mmoja mwenye kuhofu Mungu, aishiye wakati wa kipindi cha Waamuzi na ambaye ana pendeleo la kuwa nyanya wa zamani wa Yesu Kristo.

Hata hivyo, kipindi cha kutawalwa na waamuzi chafikia mwisho. Samweli ya Kwanza yaeleza juu ya utawala wenye msiba wa mfalme wa kwanza wa Israeli, Sauli, kama uonwavyo kupitia macho ya nabii Samweli. Samweli ya Pili yaeleza juu ya utawala wenye mafanikio wa Daudi, mwandamizi wa Sauli. Wafalme ya Kwanza na ya Pili ndipo zatuchukua kutoka utawala mtukufu wa Sulemani hadi uhamisho wa Kibabuloni wenye kuhuzunisha wa taifa la Kiisraeli katika 607 K.W.K. Mambo ya Nyakati ya Kwanza na ya Pili zarudia kusimulia historia hiyo kama ionwavyo kwa maoni ya taifa lililorudishwa kutoka kwenye uhamisho huo. Mwisho, Ezra, Nehemia, na Esta vyaeleza jinsi Waisraeli warudishwavyo kwenye bara la kwao na kadiri fulani ya historia yao yenye kufuata.

Vile vitabu vya kishairi ndivyo vinavyofuata, vikiwa na baadhi ya ushairi mzuri zaidi uliopata kuandikwa. Ayubu chaandaa picha yenye kuchochea ya uaminifu wa kimaadili chini ya mateso na thawabu yao. Kitabu cha Zaburi kina nyimbo za sifa kwa Yehova na sala za kuomba rehema na msaada. Hizo zimefariji watumishi wa Mungu wasiohesabika. Kwa kuongezea, Zaburi kina unabii usiohesabika ambao hutuangazia zaidi sisi habari za kuja kwa Mesiya. Mithali na Mhubiri vyafunua nyuso za hekima ya kimungu kwa njia ya semi thabiti, hali Wimbo Ulio Bora ni ushairi wa mapenzi bora kabisa yenye maana ya kiunabii iliyo ya kina kirefu.

Vitabu 17 vinavyofuata—kuanzia Isaya hadi Malaki—sana-sana ni vya kiunabii. Vyote, isipokuwa Maombolezo, vina jina la mwandikaji. Mwingi wa unabii huu tayari umekuwa na matimizo ya ajabu. Pia waelekeza kwenye matukio ya kipeo katika siku yetu na wakati ujao ulio karibu.

Hivyo Maandiko ya Kiebrania yatokeza unamna-namna wa kushangaza katika muundo na mtindo. Hata hivyo, yote yana kichwa kimoja cha ujumla. Unabii wayo mbalimbali, maelezo ya koo mbalimbali za vizazi, na matukio ya kutazamisha wang’aa kwa hekima yenye kutumika na maana ya kiunabii.

Maandiko ya Kigiriki ya Kikristo

—Yule Mbegu Atokea

Miaka elfu nne imepita tangu anguko la mwanadamu ndani ya dhambi. Kwa ghafula kwatokea katika tamasha ya kidunia yule Mbegu aliyengojewa sana, yule Mesiya, Yesu! Maandiko ya Kigiriki ya Kikristo yaweka rekodi ya huduma ya mtu huyu mkuu katika historia ya kibinadamu katika vitabu tofauti vinne lakini vyenye kukamilishana, viitwayo Gospeli. Hivyo ni Mathayo, Marko, Luka, na Yohana.

Masimulizi manne hayo ya Gospeli ni yenye thamani kubwa kama nini kwa Wakristo! Yaeleza juu ya miujiza ya Yesu ya kushangaza sana, mifano yake ya maneno yenye maana, Mahubiri yake Mlimani, kielelezo chake cha unyenyekevu, huruma yake na utii kamili kwa Baba yake, upendo wake kwa “kondoo” zake, na mwisho kifo chake cha dhabihu na ufufuo mtukufu. Uchunguzi wa zile Gospeli hujenga ndani yetu upendo wa kina kirefu kwa Mwana wa Mungu. Juu ya yote, sisi huvutwa karibu na mmoja yule aliyetuma Kristo—Yehova Mungu. Masimulizi haya yastahili kusomwa tena na tena.

Matendo ya Mitume huanzia mahali ambapo zile Gospeli zaachia. Kitabu hicho chasimulia ile miaka ya mapema ya kundi la Kikristo kuanzia siku za Pentekoste hadi kufungwa gerezani kwa Paulo katika Roma katika 61 W.K. Katika kitabu hiki, twasoma juu ya mfia-imani wa kwanza Mkristo, uongofu wa Sauli, ambaye baadaye awa Paulo yule mtume, juu ya kuletwa ndani kwa waongofu wa kwanza Wasio Wayahudi, na safari za Paulo zenye kusisimua za kueneza evanjeli. Masimulizi hayo ni yenye kusisimua hata yenye kujenga imani.

Barua, au nyaraka 21, sasa zafuata. Za kwanza 14, zilizoandikwa na Paulo, zimepewa jina kufuatana na Wakristo au makundi yenye kuzipokea; zile nyingine zimepewa jina kufuatana na waandikaji—Yakobo, Petro, Yohana, na Yuda. Ni utajiri ulioje wa maonyo ya upole na kitia-moyo yaliyo katika barua hizo! Zazungumza juu ya fundisho na utimizo wa unabii mbalimbali. Zasaidia Wakristo wabaki wamejitenga na mazingira maovu ambamo wao hulazimika kuishi. Zakazia uhitaji wa kusitawisha upendo wa kidugu na sifa nyingine za kimungu. Zaweka kigezo cha utengenezo ufaao wa kundi, chini ya uongozi wa wanaume wazee kiroho.

Kama vile Maandiko ya Kiebrania yamalizikavyo kwa wazo la kiunabii, ndivyo na Maandiko ya Kigiriki. Ufunuo, ulioandikwa na mtume Yohana karibu na 96 W.K., waziunganisha pamoja nyuzi za unabii na kile kichwa kikuu cha Biblia—kutakaswa kwa jina la Yehova na Ufalme wake wa Kimesiya. Mfululizo wa njozi waonyesha kwa maneno ya wazi sana uharibifu wa vikosi vya kidini, kijeshi, na kisiasa vya mfumo mfisadi wa Shetani. Mahali pavyo pachukuliwa na jiji la Kristo la kiserikali, ambalo lageuza fikira zalo kwenye usimamizi wa mambo ya dunia. Chini ya utawala huo wa Ufalme, Mungu aahidi ‘kufuta kila chozi katika macho yao, na mauti haitakuwapo tena.’—Ufunuo 21:4.

Basi, je! kuna shaka lolote kwamba Biblia ni johari bora isiyo na ila, yenye kuangaza nuru ya kimungu? Ikiwa wewe hujaisoma yote, kwa nini usianze kufanya hivyo sasa? Utavutiwa na pande zayo mbalimbali zenye upatano, uangaziwe maarifa na mng’ao wayo, uguswe moyo na upendezi wayo, na kusisimuliwa na ujumbe wayo. Kweli kweli hiyo ni ‘kitolewacho kilicho kamili kutoka kwa Baba wa mianga.’—Yakobo 1:17.

[Chati katika ukurasa wa 28, 29]

JEDWALI YA VITABU VYA BIBLIA

Ikionyesha mwandikaji, mahali pa kuandikia, wakati wa kumaliza kuandika, na wakati uliohusishwa na matukio ya kitabu.

Majina ya waandikaji wa vitabu fulani na ya mahali ambapo viliandikiwa hayana uhakika. Tarehe nyingi ni za ukaribio tu, huku alama ya b. ikimaanisha “baada,” kbl. ikimaanisha “kabla,” na krb. ikimaanisha “karibu.”

Vitabu vya Maandiko ya Kiebrania (K.W.K.)

Kitabu; Mwa(Waa)ndikaji; Mahali Kilipoandikiwa; Uandikaji Ukamalizwa; Wakati Uliohusishwa

Mwanzo Musa Jangwa 1513 “Hapo mwanzo” hadi 1657

Kutoka Musa Jangwa 1512 1657-1512

Walawi Musa Jangwa 1512 mwezi 1 (1512)

Hesabu Musa Jangwa/

Nyanda za Moabu 1473 1512-1473

Kumbukumbu Musa Nyanda za Moabu 1473 miezi 2 (1473)

Yoshua Yoshua Kanaani krb. 1450 1473-krb. 1450

Waamuzi Samweli Israeli krb. 1100 krb. 1450-krb. 1120

Ruthu Samweli Israeli krb. 1090 miaka 11 ya utawala wa waamuzi

1 Samweli Samweli; Gadi; Nathani Israeli krb. 1078 krb. 1180-1078

2 Samweli Gadi; Nathani Israeli krb. 1040 krb. 1077-krb. 1040

1 Wafalme Yeremia Yerusalemu/Yuda 580 krb. 1040-911

2 Wafalme Yeremia Yerusalemu/Misri 580 krb. 920-580

1 Nyakati Ezra Yerusalemu (?) krb. 460 Baada ya 1 Nyakati 9:44, 1077-537

2 Nyakati Ezra Yerusalemu (?) krb. 460 1037-537

Ezra Ezra Yerusalemu krb. 460 537-krb. 467

Nehemia Nehemia Yerusalemu b. 443 456-b. 443

Esta Mordekai Shushani, Elamu krb. 475 493-krb. 475

Ayubu Musa Jangwa krb. 1473 Miaka zaidi ya 140 kati ya 1657 na 1473

Zaburi Daudi na wengine krb. 460

Mithali Sulemani; Aguri; Lemueli Yerusalemu krb. 717

Mhubiri Sulemani Yerusalemu kbl. 1000

Wimbo Ulio Bora Sulemani Yerusalemu krb. 1020

Isaya Isaya Yerusalemu b. 732 krb. 778-b. 732

Yeremia Yeremia Yuda/Misri 580 647-580

Maombolezo Yeremia Karibu na Yerusalemu 607

Ezekieli Ezekieli Babuloni krb. 591 613-krb. 591

Danieli Danieli Babuloni krb. 536 618-krb. 536

Hosea Hosea Samaria (Wilaya) b. 745 kbl. 804-b. 745

Yoeli Yoeli Yuda krb. 820(?)

Amosi Amosi Yuda krb. 804

Obadia Obadia krb. 607

Yona Yona krb. 844

Mika Mika Yuda kbl. 717 krb. 777-717

Nahumu Nahumu Yuda kbl. 632

Habakuki Habakuki Yuda krb. 628(?)

Sefania Sefania Yuda kbl. 648

Hagai Hagai Yerusalemu 520 Siku 112 (520)

Zekaria Zekaria Yerusalemu 518 520-518

Malaki Malaki Yerusalemu b. 443

Vitabu vya Maandiko ya Kigiriki ya Kikristo (W.K.)

Kitabu; Mwandikaji; Mahali Kilipoandikiwa ; Uandikaji Ukamalizwa; Wakati Uliohusishwa

Mathayo Mathayo Palestina krb. 41 2 K.W.K.-33 W.K.

Marko Marko Roma krb. 60-65 29-33 W.K.

Luka Luka Kaisaria krb. 56-58 3 K.W.K.-33 W.K.

Yohana Mtume Yohana Efeso, au karibu hapo krb. 98 Baada ya umalizio, 29-33 W.K.

Matendo Luka Roma krb. 61 33-krb. 61 W.K.

Warumi (Waroma) Paulo Korintho krb. 56

1 Wakorintho Paulo Efeso krb. 55

2 Wakorintho Paulo Makedonia krb. 55

Wagalatia Paulo Korintho au Antiokia ya Siria krb. 50-52

Waefeso Paulo Roma krb. 60-61

Wafilipi Paulo Roma krb. 60-61

Wakolosai Paulo Roma krb. 60-61

1 Wathesalonike Paulo Korintho krb. 50

2 Wathesalonike Paulo Korintho krb. 51

1 Timotheo Paulo Makedonia krb. 61-64

2 Timotheo Paulo Roma krb. 65

Tito Paulo Makedonia(?) krb. 61-64

Filemoni Paulo Roma krb. 60-61

Waebrania Paulo Roma krb. 61

Yakobo Yakobo (Ndugu ya Yesu) Yerusalemu kbl. 62

1 Petro Petro Babuloni krb. 62-64

2 Petro Petro Babuloni(?) krb. 64

1 Yohana Mtume Yohana Efeso, au karibu hapo krb. 98

2 Yohana Mtume Yohana Efeso, au karibu hapo krb. 98

3 Yohana Mtume Yohana Efeso, au karibu hapo krb. 98

Yuda Yuda (Ndugu ya Yesu) Palestina(?) krb. 65

Ufunuo Mtume Yohana Patmosi krb. 96

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki