Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w92 5/15 uku. 3
  • Je! Kweli Biblia Ni Zawadi Kutoka kwa Mungu?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je! Kweli Biblia Ni Zawadi Kutoka kwa Mungu?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1992
  • Habari Zinazolingana
  • Je! Kitabu Hiki Kinaweza Kukusaidia Ufanikiwe?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1981
  • Hifadhi ya Nyaraka za Siri Yafunguliwa
    Amkeni!—1998
  • Yehova Huwalinda Watu Wake
    Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2020
  • Maarifa Ni Mengi Lakini Mabadiliko Ni Machache
    Amkeni!—2002
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1992
w92 5/15 uku. 3

Je! Kweli Biblia Ni Zawadi Kutoka kwa Mungu?

“NAAMINI kwamba Biblia ndiyo zawadi bora zaidi ambayo Mungu amepata kumpa mwanadamu kwa wakati wowote.” Taarifa hiyo ilitolewa na Abraham Lincoln, rais wa 16 wa United States.a Si yeye peke yake anayeonyesha uthamini wake kwa ajili ya kitabu hicho cha zamani.

Waziri wa serikali Mwingereza wa karne ya 19 William E. Gladstone alitaarifu hivi: “Biblia inadhihirishwa kuwa na Mwanzo wa Kipekee, nayo hutengwa kwa mbali na vitabu vingine.” Kwa kupatana na mawazo hayo, waziri wa serikali Mwamerika wa karne ya 18 Patrick Henry alisema hivi: “Biblia ina thamani kubwa kuliko vitabu vingine vyote ambavyo vimepata kuchapishwa wakati wowote.” Kwa wazi, akivutiwa na Maandiko Maliki Mfaransa Napoléon Bonaparte alieleza hivi: ‘Biblia si kitabu cha kawaida tu, bali ni Kitu Chenye Uhai, chenye uwezo wa kushinda wote wanaokipinga.’

Kwa wengine, Biblia imekuwa chanzo cha msaada na faraja. Robert E. Lee aliyekuwa jemadari wa Mwungano wa Majimbo ya Amerika alitaarifu hivi: “Biblia haijashindwa kamwe kunipa mwangaza na imara katika matatizo na taabu zangu.” Na kwa sababu ya uthamini wake kwa kitabu hicho, rais wa U.S. John Quincy Adams alisema hivi: “Kwa muda wa miaka mingi nimefanya kusoma Biblia yote kila mwaka kuwa zoea langu.”

Ikiwa yule Aliye Juu Zaidi ameipa ainabinadamu Biblia, kwapasa kuwa ushuhuda wa kwamba imepuliziwa roho kimungu. Yapasa kuwa bora zaidi ya kitabu kingine chochote. Na ili Biblia iwe chanzo cha kweli cha imara na maagizo, ingepasa kutegemeka kabisa. Kwa hiyo basi, swali moja labaki, Je! kweli Biblia ni zawadi kutoka kwa Mungu? Acheni sasa tutafute jibu la swali hilo.

[Maelezo ya Chini]

a Bila shaka, kuna zawadi bora zaidi—Yesu Kristo.—Yohana 3:16.

[Picha katika ukurasa wa 3]

William E. Gladstone

[Hisani]

U.S. National Archives photo

Abraham Lincoln

[Hisani]

U.S. National Archives photo

Patrick Henry

[Hisani]

Harper’s U.S. History

Napoléon Bonaparte

[Hisani]

Drawn by E. Ronjat

John Quincy Adams

[Hisani]

Harper’s U.S. History

Robert E. Lee

[Hisani]

U.S. National Archives photo

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki