Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w92 7/1 kur. 24-25
  • Gerasa-Mahali Ambapo Wayahudi na Wagiriki Walikutana

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Gerasa-Mahali Ambapo Wayahudi na Wagiriki Walikutana
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1992
  • Habari Zinazolingana
  • Dekapoli
    Ufahamu wa Kina wa Maandiko
  • Njoo Uzuru Bahari ya Galilaya!
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1993
  • B10 Nchi ya Israeli Katika Siku za Yesu
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
  • Yordani Ambayo Huenda Ikawa Huijui
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1992
w92 7/1 kur. 24-25

Mandhari Kutoka Bara Lililoahidiwa

Gerasa-Mahali Ambapo Wayahudi na Wagiriki Walikutana

MTUME Paulo aliandika kwamba miongoni mwa mbegu ya kweli ya Abrahamu, “hakuna tena tofauti kati ya Myahudi na Mgiriki.” (Wagalatia 3:26-29, HNWW) Naam, malezi ya kitaifa au kitamaduni hayakuwa na maana kwa habari ya kupata kibali cha Mungu.

Maneno hayo huenda yakaonekana kufaa kwa Wakristo walioenea katika mkoa mmoja wa Roma, kama vile mkoa wa Galatia, ambapo palikuwa mchanganyiko wa Wayahudi, Wagiriki, Waroma, na wenyeji wa hapo. Lakini namna gani sehemu za Israeli yenyewe, kama vile Gileadi?

Eneo hilo liko mashariki mwa Yordani, kati ya Bahari ya Chumvi (Baharifu) na Bahari ya Galilaya. Karibu na katikati mwa nyanda hiyo ya juu yenye rutuba, Mto Yaboki huteremka kuelekea Yordani. Picha iliyo juu huonyesha baadhi ya magofu yenye kuvutia ya Gerasa, uitwao Jerash sasa, uliokuwa karibu na Yaboki ya juu.

Barabara ya kale ya biashara itokayo kaskazini hadi kusini iitwayo “barabara ya mfalme” ilipitia Gileadi. Walipoondoka Harani, Yakobo na familia yake yaonekana walisafiri kwenye barabara hii hadi Yaboki. Alishindana mweleka na malaika na kumkabili Esau karibu na mahali ambapo Gerasa ungejengwa. (Mwanzo 31:17-25, 45-47; 32:22-30; 33:1-17) Katika wakati wa baadaye, Waisraeli walihama kutoka kusini kwenye barabara ya mfalme walipoelekea Bara Lililoahidiwa. Makabila mawili na nusu yalikaa kaskazini na kusini mwa Yaboki kando ya barabara hiyo ya biashara.—Hesabu 20:17; Kumbukumbu la Torati 2:26, 27.

Je! Wagiriki walihusika na eneo hilo, na ikiwa ndivyo, kwa njia gani? Ndiyo, walihusika na eneo hilo wakati Aleksanda Mkuu aliposhinda eneo hilo. Kulingana na mapokeo, alijenga Gerasa kwa ajili ya wastadi wa jeshi lake. Polepole, uvutano wa Kigiriki ukaenea sana. Kumi ya miji ya kikoloni mashariki mwa Yordani na Bahari ya Galilaya yalifanyiza muungano uitwao Dekapoli. Huenda ikawa umeona jina hilo katika Biblia, inayoripoti kwamba ‘makutano mengi walimfuata [Yesu], kutoka Galilaya, na Dekapoli, na Yerusalemu, na Uyahudi, na ng’ambo ya Yordani.’ Gerasa ulikuwa mmojawapo miji hiyo ya Dekapoli.—Mathayo 4:25.

‘Sehemu ya mpango wa Aleksanda ilikuwa kuleta Wagiriki katika sehemu zote za milki. Siria ya Chini [kutia na Dekapoli], hasa, ikiwa mojawapo vitovu muhimu, ilipokea wakaaji wengi Wagiriki. Hadi leo hakuna sehemu nyingine ya ulimwengu wa mashariki iwezayo kuonyesha magofu ya Kigiriki mengi sana na yenye kuvutia sana kama ile nchi iliyoko mashariki mwa Yordani. Miji ya Kigiriki ilionyesha, kijuujuu tu, mweneo kamili wa mila na desturi za Kigiriki—mahekalu mazuri ajabu ya miungu na miungu-wake wa Kigiriki, majumba ya michezo, mahali pa kuogea pa watu wote, miadhimisho ya michezo ya kila mwaka, na katika visa vingi shule na vyuo vya kifalsafa.’—Hellenism, cha Norman Bentwich.

Ukizuru magofu ya Gerasa, utapata uthibitisho wa kutosha wa jambo hilo. Karibu na mwingilio wa kusini, kuna uwanja wa duara, au soko la watu wote, lionekanalo katika picha. Yaelekea utashangazwa na mahali-mahali pa kuogea, mahekalu, majumba ya michezo ya kuigiza, majengo ya umma, mengi yao yakiwa yameunganishwa kwa barabara za mawe zenye nguzo kila upande. Nje ya mji, waweza kuona mawe au alama za kuonyesha mwendo wa maili kando ya barabara ya zamani iliyounganisha Gerasa na miji mingine ya Dekapoli na bandari za Mediterania.

Hata baada ya Roma kutwaa Gerasa katika 63 K.W.K., uvutano wa Kigiriki uliendelea kuwako. Waweza kuwazia jinsi uvutano huo ungeweza kuathiri Wayahudi walioishi katika Gerasa na eneo hilo. Kitabu Hellenism huonelea hivi: “Polepole lakini kwa hakika Wayahudi walianza kufuata mawazo ya kidini ya watu waliowazunguka, na kuyaona Maandiko chini ya uvutano wa mawazo hayo.”

Ingawa huenda ikawa Yesu hakuhubiri katika mji huo, yeye aliingia wilaya ya Gerasa, ambayo huenda ikawa ilifika hadi Bahari ya Galilaya. Aliondosha roho waovu kutoka kwa mwanamume katika wilaya hiyo, akiwaruhusu waingie kwa nguruwe. (Marko 5:1-17) Yaelekea, wanafunzi wake wa mapema walihubiria Wayahudi katika miji ya Dekapoli, na baada ya 36 W.K., habari njema ingeweza kutolewa kwa Wagiriki katika Gerasa. Iwe mtu aliyekubali Ukristo alikuwa amekuwa mwenye kufuata sana itikadi za Kiyahudi, Myahudi aliyefuata dini ya Kigiriki, au Mgiriki, angeweza kukubaliwa na Mungu wa kweli kuwa sehemu ya mbegu ya kiroho ya Abrahamu.

[Ramani katika ukurasa wa 24]

(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)

[Hisani]

Yenye msingi wa ramani iliyonakiliwa kwa haki ya Pictorial Archive (Near Eastern History) Est.

[Picha katika ukurasa wa 24]

Picha iliyopo juu inapatikana kwa ukubwa katika 1992 Calendar of Jehovah’s Witnesses.

[Hisani]

Pictorial Archive (Near Eastern History) Est.

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 25]

Pictorial Archive (Near Eastern History) Est.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki