Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w95 9/15 kur. 3-5
  • Unalopaswa Kujua Juu ya Wivu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Unalopaswa Kujua Juu ya Wivu
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1995
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • “Mwelekeo wa Kuhusudu”
  • Ulimwengu Bila Wivu Wenye Dhambi
  • Upendo Hushinda Wivu Usiofaa
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1995
  • Wivu kwa Ajili ya Ibada Safi ya Yehova
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1995
  • Ndugu za Yosefu Wamwonea Wivu
    Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2020
  • Je, Wakristo Wanapaswa Kuwa na Wivu?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2002
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1995
w95 9/15 kur. 3-5

Unalopaswa Kujua Juu ya Wivu

WIVU ni nini? Ni hisia yenye nguvu inayoweza kumfanya mtu ahisi hangaiko, huzuni, au awe na hasira. Tunaweza kuona wivu mtu fulani akionekana kuwa na mafanikio zaidi kwa jambo fulani kuliko sisi. Au twaweza kuona wivu rafiki apokeapo sifa nyingi kuliko sisi. Lakini, je, ni vibaya sikuzote kuona wivu?

Watu wanaoshindwa na wivu huelekea kuwa wenye kushuku wale wawaonao kuwa wapinzani wao. Mfalme Sauli wa Israeli la kale alikuwa mfano wa jambo hilo. Kwanza alimpenda mbeba-silaha wake, Daudi, hata akampandisha cheo kuwa kiongozi wa jeshi. (1 Samweli 16:21; 18:5) Kisha siku moja Mfalme Sauli akasikia wanawake wakimsifu Daudi kwa maneno haya: “Sauli ameua elfu zake, na Daudi makumi elfu yake.” (1 Samweli 18:7) Sauli hakupaswa kuruhusu jambo hilo liathiri uhusiano wake mzuri na Daudi. Lakini aliudhika. “Sauli akamwonea Daudi wivu tangu siku ile.”—1 Samweli 18:9.

Mtu mwenye wivu huenda asimtakie mwenzake madhara. Huenda yeye akachukizwa tu na mafanikio ya mwenzake na kutamani kuwa na sifa au hali kama zake. Kwa upande mwingine, husuda hasa ni aina mbaya ya wivu. Mtu mwenye husuda aweza kumnyima kisiri mambo mema yule anayemwonea wivu au aweza kumtakia madhara. Nyakati nyingine, mtu mwenye wivu hawezi kuficha hisia zake. Anaweza kusukumwa kumdhuru mwingine waziwazi, kama tu Mfalme Sauli alivyojaribu kumuua kimakusudi Daudi. Zaidi ya pindi moja, Sauli alimtupia mkuki akijaribu “kumpiga Daudi hata ukutani.”—1 Samweli 18:11; 19:10.

‘Lakini mimi sina wivu,’ huenda ukajibu. Kweli, huenda wivu usidhibiti maisha yako. Hata hivyo, kwa kadiri fulani sote tunaathiriwa na wivu—hisia zetu wenyewe za wivu na zile za wengine. Ingawa sisi ni wepesi kuona wivu wa watu wengine, twaweza kukosa kuona wivu ndani yetu wenyewe.

“Mwelekeo wa Kuhusudu”

Rekodi ya asili ya binadamu yenye dhambi kama ifunuliwavyo katika Neno la Mungu, Biblia, mara nyingi hukazia dhambi za husuda. Je, wakumbuka masimulizi ya Kaini na Abeli? Wana hao wawili wa Adamu na Hawa walimtolea Mungu dhabihu. Abeli alifanya hivyo kwa sababu alikuwa mtu wa imani. (Waebrania 11:4) Alikuwa na imani katika uwezo wa Mungu wa kutimiza kusudi Lake tukufu kuhusu dunia. (Mwanzo 1:28; 3:15; Waebrania 11:1) Abeli pia aliamini kwamba Mungu angethawabisha wanadamu waaminifu kwa kuwapa uhai katika Paradiso inayokuja ya kidunia. (Waebrania 11:6) Hivyo, Mungu akaonyesha kupendezwa na dhabihu ya Abeli. Kama kweli Kaini alikuwa amempenda ndugu yake, angefurahi kwamba Mungu alikuwa amembariki Abeli. Badala ya hivyo, Kaini “akaghadhibika sana.”—Mwanzo 4:5.

Mungu alimhimiza Kaini afanye mema ili yeye pia apokee baraka. Kisha Mungu akaonya: “Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde.” (Mwanzo 4:7) Kwa huzuni, Kaini hakuishinda hasira yake yenye wivu. Ilimsukuma amuue kimakusudi ndugu yake mwadilifu. (1 Yohana 3:12) Tangu wakati huo, mapigano na vita vimeua mamia ya mamilioni ya watu. “Baadhi ya visababishi vya msingi vya vita vyaweza kuwa tamaa ya ardhi zaidi, tamaa ya mali zaidi, tamaa ya uwezo zaidi, au tamaa ya usalama,” chaeleza The World Book Encyclopedia.

Wakristo wa kweli hawashiriki katika vita vya ulimwengu huu. (Yohana 17:16) Ingawa hivyo, kwa kusikitisha, nyakati nyingine Wakristo mmoja-mmoja hujihusisha katika vita vya maneno. Na washiriki wengine wakijihusisha, vita hivyo vyaweza kutokeza vita vya maneno vyenye kudhuru. “Vita vyatoka wapi, na mapigano yaliyoko kati yenu yatoka wapi?” mwandikaji wa Biblia Yakobo aliuliza waamini wenzake. (Yakobo 4:1) Alijibu swali hilo kwa kufunua tamaa yao ya vitu vya kimwili naye akaongezea, “Mwaendelea . . . kutamani kwa wivu,” au kuona “wivu.” (Yakobo 4:2, kielezi-chini, New World Translation) Ndiyo, tamaa ya vitu vya kimwili yaweza kutokeza kutamani kwa wivu na kuonea wivu wale wanaoonekana kuwa na vitu zaidi. Kwa sababu hiyo, Yakobo alionya dhidi ya “mwelekeo wa [binadamu wa] kuhusudu.”—Yakobo 4:5, NW.

Kuna manufaa gani katika kuchunguza visababishi hivi vya wivu? Kuvichunguza kwaweza kutusaidia kuwa wanyoofu na kuendeleza mahusiano mazuri zaidi pamoja na wengine. Kwaweza pia kutusaidia kuwa wenye kuelewa mambo zaidi, wavumilivu, na wenye kusamehe. Zaidi ya yote, kwakazia uhitaji mkubwa wa mwanadamu wa andalio lenye upendo la Mungu la wokovu na kukombolewa kutoka kwa mielekeo yenye dhambi ya binadamu.—Warumi 7:24, 25.

Ulimwengu Bila Wivu Wenye Dhambi

Kwa maoni ya kibinadamu, ulimwengu bila wivu wenye dhambi waweza kuonekana kuwa hauwezekani. Mtungaji wa vitabu Rom Landau alikiri hivi: “Hekima zilizokusanywa za vizazi vingi, na yale yote ambayo wanafalsafa hao wote . . . na wanasaikolojia wamesema juu ya habari hii, hazimpi mwongozo mtu anayesononeka kwa wivu. . . . Je, kuna daktari yeyote aliyepata kumtibu mtu mwenye wivu?”

Lakini Neno la Mungu latoa tumaini la kupata uhai mkamilifu wa kibinadamu katika ulimwengu mpya ambako hakuna mtu atakayepatwa tena na wivu usio wa kimungu au husuda. Isitoshe, amani ya ulimwengu huo mpya haitavurugwa na watu wanaoonyesha tabia kama hizo zenye uovu.—Wagalatia 5:19-21; 2 Petro 3:13.

Lakini, wivu wote si mbaya. Hata Biblia yasema kwamba Yehova “ni Mungu mwenye wivu.” (Kutoka 34:14) Hilo lamaanisha nini? Na Biblia yasema nini juu ya wivu unaofaa? Na kwa wakati uo huo, mtu anaweza kushindaje wivu usiofaa? Ona makala zifuatazo.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki