Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w95 9/15 uku. 5
  • Wivu Karibu Uharibu Maisha Yangu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Wivu Karibu Uharibu Maisha Yangu
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1995
  • Habari Zinazolingana
  • Upendo Hushinda Wivu Usiofaa
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1995
  • Wivu kwa Ajili ya Ibada Safi ya Yehova
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1995
  • Unalopaswa Kujua Juu ya Wivu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1995
  • Jinsi ya Kuepuka Wivu Katika Ndoa
    Msaada kwa Ajili ya Familia
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1995
w95 9/15 uku. 5

Wivu Karibu Uharibu Maisha Yangu

WIVU ulianza kuniathiri vibaya hasa nilipoolewa na mume wangu wa pili, Mark.a Kati yetu, tulikuwa tutunze watoto kadhaa wa kambo na kushughulika na wenzi wetu wa ndoa wa zamani. Nyakati nyingine hali ilikuwa ngumu sana kuvumilia. Wakati wowote kulipozuka ubishi wa kifamilia, ilionekana kama Mark hakuwa akiniunga mkono. Nikaanza kuhisi kwamba angali alimpenda mke wake wa zamani. Badala ya kudhibiti wivu wangu, niliuruhusu udhibiti maisha yangu. Niliona tisho wakati wowote mke wa zamani wa Mark alipokuwapo.

Nilikuwa nikimtazama Mark daima, hata kutazama macho yake kuona alikuwa akiangalia wapi. Niliona katika macho yake mambo ambayo hata hayakuwapo. Nyakati nyingine hata nilikuwa nikimshtaki waziwazi kwamba alikuwa angali anampenda mke wake wa zamani. Pindi moja aliudhika sana na jambo hili hata akainuka akatoka kwenye kusanyiko la Kikristo. Nilihisi hatia mbele ya Yehova. Nilifanya maisha ya familia yangu kuwa yenye huzuni kwa sababu hatimaye watoto nao waliathiriwa. Nilijichukia kwa yale niliyokuwa nikifanya, lakini hata nilipojaribu namna gani, nilishindwa kabisa kudhibiti wivu wangu.

Badala ya kunisaidia, Mark alianza kulipiza kisasi. Nilipomshtaki, alikuwa akinipigia kelele, “Wivu, unaona wivu tu.” Hata alionekana kama alikuwa anafanya kimakusudi nione wivu. Labda alifikiri hiyo ilikuwa dawa ya wivu wangu, lakini ilifanya mambo kuwa mabaya hata zaidi. Alianza kutazama wanawake wengine, akieleza jinsi walivyoonekana warembo. Hilo lilinifanya nihisi sifai kitu na kwamba sikutakiwa. Ilifikia hatua ambayo hisia nyingine—chuki—ilizuka. Kufikia wakati huo, nilichanganyikiwa sana hivi kwamba nilitaka nitengane naye na familia yake.

Biblia isemapo kwamba ‘wivu ni ubovu wa mifupa,’ ni kweli kabisa. (Mithali 14:30) Afya yangu ikaanza kuathiriwa sasa. Nikapatwa na vidonda vya tumbo vilivyochukua muda mrefu kupona. Niliendelea kufanya maisha yangu kuwa yenye huzuni kwa kushuku kila kitu ambacho Mark alikuwa akifanya. Nilikuwa nikipekua mifuko yake ya nguo, na nikipata nambari za simu, nilikuwa nikipiga nione ni nani waliojibu. Ndani kabisa moyoni niliaibika sana, nilikuwa nikilia kwa sababu ya aibu mbele ya Yehova. Lakini nilishindwa kujidhibiti. Mimi mwenyewe nilikuwa adui yangu mkubwa zaidi.

Hali yangu ya kiroho ilidhoofika kufikia kiwango ambacho singeweza kusali tena. Nilimpenda Yehova nami kwa kweli nilitaka kufanya yaliyo mema. Nilijua maandiko yote yaliyohusu waume na wake, lakini nilishindwa kuyatumia. Kwa mara ya kwanza maishani mwangu, sikutaka kuishi, nijapokuwa na watoto wazuri sana.

Wazee katika kutaniko la Kikristo walikuwa kitia-moyo kikubwa kwangu nao walijaribu kadiri wawezavyo kunisaidia. Lakini walipojaribu kutokeza suala la wivu wangu, nilikuwa nikikanusha jambo hilo kwa sababu ya kuona aibu, nisitake kukubali kwamba nilikuwa na tatizo hilo.

Hatimaye, afya yangu ilidhoofika hivi kwamba nililazimika kwenda hospitali kufanyiwa upasuaji. Nilipokuwa huko niling’amua maisha hayangeendelea hivyo. Mark nami tuliamua kutengana kwa miezi mitatu ili kuchanganua hali yetu bila kujihusisha mno kihisia-moyo. Katika kipindi hicho jambo fulani la ajabu lilitendeka. Katika gazeti la Amkeni! kulitokea makala yenye kichwa “Msaada kwa Watoto Wakubwa wa Waraibu wa Alkoholi.”b

Wajua, mama yangu alikuwa mraibu wa alkoholi. Ingawa sikutendwa vibaya kimwili, wazazi wangu hawakupata kuonyesha mapenzi yoyote ya kimwili ama kati yao ama kunielekea. Sikumbuki mama yangu akinibeba mikononi mwake au akiniambia kwamba ananipenda. Kwa hiyo kwa kweli nilikua bila kujua kabisa jinsi ya kupenda au, la muhimu pia kwa kadiri hiyo, jinsi ya kupendwa.

Mara nyingi mama yangu aliniambia juu ya mahusiano ya kimahaba ya baba yangu pamoja na wengine naye hakumtumaini. Kwa hiyo nadhani nilikua nikiwa situmaini wanaume kwa ujumla. Kwa sababu ya malezi yangu, sikuzote nilihisi kuwa wa hali ya chini kuliko wengine, hasa wanawake wengine. Kusoma makala hiyo ya Amkeni! kulinisaidia kushika umuhimu wa mambo haya. Kwa mara ya kwanza, nilielewa visababishi vya tatizo langu la wivu.

Nilimwonyesha mume wangu, Mark, makala hiyo ya Amkeni!, nayo pia ilimsaidia kunielewa vizuri zaidi. Upesi sisi wawili tuliweza kufuata shauri la Biblia kwa waume na wake wanaofikiria kutengana. Tukarudiana. (1 Wakorintho 7:10, 11) Sasa ndoa yetu ni bora kuliko wakati mwingine wowote. Sisi hufanya mambo mengi zaidi pamoja, hasa yale yanayohusu utendaji wa Kikristo. Mark huonyesha hisia-mwenzi zaidi. Karibu kila siku yeye huniambia jinsi anavyonipenda, na sasa naamini kabisa.

Nipatapo kujua kwamba tutakutana na mke wa zamani wa Mark, mimi husali kwa Yehova anipe nguvu, nikimwomba anisaidie kutenda kama Mkristo mkomavu. Na hiyo hufaulu. Hata hisia zangu za uhasama kumwelekea zinapungua. Sikazii fikira tena mawazo hasi wala sijiruhusu niwazie mambo yasiyofaa.

Ningali ninapata hisia zisizofaa za wivu. Ni uhai mkamilifu tu katika ulimwengu mpya wa Mungu utakaoniondolea kabisa wivu. Kwa wakati huu, nimejifunza kudhibiti wivu wangu, badala ya kuuacha unidhibiti. Ndiyo, wivu karibu uharibu maisha yangu, lakini kwa sababu ya Yehova na tengenezo lake, sasa mimi ni mtu mwenye furaha zaidi, na afya yangu imerudia hali ya kawaida. Mara nyingine tena nina uhusiano wenye nguvu pamoja na Mungu, Yehova.—Imechangwa.

[Maelezo ya chinis]

a Jina limebadilishwa.

b Ona Amkeni! la Mei 22, 1992, kurasa 8-12, Kiingereza.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki