Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w96 5/15 kur. 8-9
  • Msichana Mdogo Aliyesema kwa Moyo Mkuu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Msichana Mdogo Aliyesema kwa Moyo Mkuu
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1996
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Moyo Mkuu wa Kusema
  • Kupona kwa Naamani
  • Masomo Kwetu Sisi
  • Alitaka Kusaidia
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2008
  • Shujaa na Msichana Mdogo
    Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
  • Alikuwa Mkaidi Lakini Mwishowe Alitii
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2012
  • “Jifungeni Unyenyekevu”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1975
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1996
w96 5/15 kur. 8-9

Walifanya Mapenzi ya Yehova

Msichana Mdogo Aliyesema kwa Moyo Mkuu

KATIKA karne ya kumi K.W.K., mahusiano kati ya Israeli na Siria yalikuwa mabaya. Mapigano yalikuwa ya kawaida sana hivi kwamba miaka mitatu ilipoisha bila jeuri, ilikuwa historia.—1 Wafalme 22:1.

Vilivyokuwa vyenye kuogofya hasa wakati huo ni vile vikosi vya wanyang’anyi vya Siria, vingine vikiwa na mamia ya wanajeshi. Hao wapiganaji walikuwa wakivamia na kupora Waisraeli, wakichukua kwa nguvu na kuwatumikisha wengi—hata watoto.

Wakati wa uvamizi mmoja, “kijana mwanamke” alitwaliwa bila huruma toka kwa familia yake yenye kumhofu Mungu. (2 Wafalme 5:2) Alipopelekwa Siria, alilazimishwa kuishi miongoni mwa watu ambao huenda aliwaona kuwa wenye kuogofya na wa ajabu—watu walioabudu jua, mwezi, nyota, miti, mimea, na hata mawe. Jinsi walivyotofautiana na familia na marafiki wake, waliomwabudu Mungu wa pekee wa kweli, Yehova! Hata hivyo, hata katika mazingira haya tofauti, msichana huyo alionyesha moyo mkuu kwa njia ya pekee kuhusiana na ibada ya Yehova. Kama tokeo, aligeuza maisha ya ofisa mkuu aliyekuwa akitumikia chini ya mfalme wa Siria. Acheni tuone jinsi gani.

Moyo Mkuu wa Kusema

Huyo msichana mdogo hatajwi kwa jina katika masimulizi ya Biblia. Alikuja kuwa mjakazi wa mke wa Naamani, jemadari wa jeshi chini ya Mfalme Ben-hadadi 2. (2 Wafalme 5:1) Ingawa aliheshimiwa sana, Naamani alikuwa na ugonjwa wenye kuchukiza wa ukoma.

Huenda tabia ya huyo msichana yenye heshima ilimsukuma mke wa Naamani kusema naye kwa siri. Huenda ikawa huyo mwanamke alimwuliza huyo msichana, ‘Ni nini wafanyiwacho wenye ukoma katika Israeli?’ Msichana huyo Mwisraeli hakuona haya kusema kwa ushujaa: “Laiti bwana wangu angekuwa pamoja na yule nabii aliyeko Samaria! maana angemponya ukoma wake.”—2 Wafalme 5:3.

Maneno ya msichana huyo hayakuonwa kuwa fantasia ya kitoto tu. Tofauti na hilo, yaliripotiwa kwa Mfalme Ben-hadadi, aliyemtuma Naamani na wengine wafunge safari ya kilometa 150 hadi Samaria wakamtafute nabii huyo.—2 Wafalme 5:4, 5.

Kupona kwa Naamani

Naamani na watu wake walimwendea Mfalme Yehoramu wa Israeli, wakiwa na barua ya kuwatambulisha iliyotoka kwa Ben-hadadi na kiasi kikubwa cha zawadi ya kifedha. Si ajabu kuwa Mfalme Yehoramu aliyeabudu ndama hakuonyesha imani, kama ile ya yule mjakazi, katika nabii wa Mungu. Badala ya hilo, alifikiri kuwa Naamani alikuja kutafuta ugomvi. Nabii wa Mungu Elisha aliposikia juu ya shaka za Yehoramu, mara moja akatuma ujumbe akiomba kwamba mfalme amtume Naamani nyumbani kwake.—2 Wafalme 5:6-8.

Naamani alipofika kwa nyumba ya Elisha, huyo nabii alimtuma mjumbe aliyemwambia: “Enenda ukaoge katika Yordani mara saba, na nyama ya mwili wako itakurudia, nawe utakuwa safi.” (2 Wafalme 5:9, 10) Naamani alikasirika sana. Akitarajia kutibiwa kwa njia ya kimuujiza na yenye kutokeza zaidi, aliuliza: “Je! Abana na Farpari, mito ya Dameski, si bora kuliko maji yote ya Israeli? Je! siwezi kujiosha ndani yake, na kuwa safi?” Naamani akaondoka nyumbani kwa Elisha akiwa na ghadhabu. Lakini watumishi wa Naamani waliposababu naye, mwishowe alikubali. Baada ya kuoga mara saba katika Mto Yordani, “nyama ya mwili wake ikarudi ikawa kama nyama ya mwili wa mtoto mchanga, akawa safi.”—2 Wafalme 5:11-14.

Aliporudi kwa Elisha, Naamani alisema: “Sasa tazama, najua ya kwamba hakuna Mungu duniani mwote, ila katika Israeli.” Naamani akaapa kuwa “hatatoa tena sadaka ya kuteketezwa wala dhabihu kwa miungu mingine, ila kwa BWANA [“Yehova,” NW].”—2 Wafalme 5:15-17.

Masomo Kwetu Sisi

Naamani hangalienda kamwe kwa nabii Elisha ikiwa mjakazi mdogo hangalikuwa ameongea kwa moyo mkuu. Leo, vijana wengi wanafanya vivyo hivyo. Shuleni, huenda wakazingirwa na wanafunzi wasio na tamaa yoyote ya kumtumikia Mungu. Hata hivyo, wao hunena juu ya kile waaminicho. Wengine wao huanza kufanya hivyo wakiwa na umri mchanga sana.

Mfikirie Alexandra, msichana wa miaka mitano katika Australia. Alipoanza shule, mama yake alipanga kumweleza mwalimu itikadi za Mashahidi wa Yehova. Lakini mama ya Alexandra hakujua lililomngojea. “Tayari najua baadhi ya itikadi zenu, kutia ndani na yale Alexandra atafanya au hatafanya akiwa shuleni,” mwalimu akasema. Mama ya Alexandra alishangazwa, kwa kuwa hakukuwa na watoto wengine wa Mashahidi katika hiyo shule. “Alexandra alitujulisha juu ya itikadi zake,” mwalimu akaeleza. Ndiyo, huyo msichana mdogo alikuwa tayari amezungumza kwa busara na mwalimu wake.

Wachanga kama hao hunena wakiwa na moyo mkuu. Hivyo wao hutenda kwa kupatana na Zaburi 148:12, 13: “Vijana waume, na wanawali, wazee, na watoto; na walisifu jina la BWANA, maana jina lake peke yake limetukuka; adhama yake i juu ya nchi na mbingu.”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki