Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w96 9/1 kur. 3-4
  • Je, Maisha Yako Yanadhibitiwa na Ajali?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je, Maisha Yako Yanadhibitiwa na Ajali?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1996
  • Habari Zinazolingana
  • Je, Biblia Hufundisha Itikadi Katika Ajali?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1996
  • Je! Imani Katika Ajali Hutawala Maisha Yako?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
  • Je, Maisha Yako Yameamuliwa Kimbele au Wapatwa na Tukio Tu?
    Amkeni!—1999
  • Kutafuta Mambo Yaliyokusudiwa Kimbele ya Mwanadamu
    Amkeni!—1999
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1996
w96 9/1 kur. 3-4

Je, Maisha Yako Yanadhibitiwa na Ajali?

“ALA NÒ DON.” Katika lugha ya Kibambara ya Mali, Afrika Magharibi, usemi huu wamaanisha, “Ni kazi ya Mungu.” Shime hizo ni za kawaida sana katika sehemu hiyo ya ulimwengu. Katika lugha ya Kiwolof, usemi ni, “Yallah mo ko def” (Ni Mungu alifanya). Na katika lahaja moja ya mashambani ya kabila la Dogon, wao husema, “Ama biray” (Ni Mungu aliyesababisha).

Kuna semi zizo hizo katika nchi nyinginezo. Semi kama, “Wakati wake ulikuwa umefika” na, “Yalikuwa mapenzi ya Mungu” husikiwa mara nyingi wakati wowote kifo au msiba zinapotokea. Katika Afrika Magharibi, shime kama “Binadamu hukusudia, Mungu hutekeleza” huandikwa kwa kawaida kwenye magari ya kusafirishia watu wote na huwekwa yakiwa ishara katika maduka. Kwa wengi hizo ni tamathali za usemi tu. Lakini, mara nyingi huonyesha itikadi katika nadharia ajali yenye kina sana.

Nadharia ajali ni nini hasa? Kichapo The World Book Encyclopedia chaifasili kuwa “itikadi ya kwamba matukio yanaamuliwa na kani ambazo wanadamu hawawezi kudhibiti.” “Kani” hizo ni nini? Maelfu ya miaka iliyopita, Wababiloni waliamini kwamba ajali ya mtu iliathiriwa sana na hali ya nyota wakati wa kuzaliwa kwake. (Linganisha Isaya 47:13.) Wagiriki waliamini kwamba ajali ilikuwa mikononi mwa miungu wa kike watatu wenye nguvu waliosokota, wakapima, na kukata uzi wa uhai. Hata hivyo, ni wanatheolojia wa Jumuiya ya Wakristo waliotokeza wazo la kwamba Mungu mwenyewe ndiye huamua ajali ya mtu!

Kwa kielelezo “Mtakatifu” Augustine, alikataa yale “maoni yasiyo ya kweli na yenye kuchukiza” ya wanajimu. Kwa upande mwingine, alibisha kwamba “kuungama kwamba Mungu yuko, na wakati uleule kukana kwamba Yeye ana ujuzi wa kimbele juu ya mambo ya wakati ujao, ni upumbavu ulio dhahiri zaidi.” Alidai kwamba ili Mungu awe mweza yote kikweli, ni lazima “ajue mambo yote kabla yatimie” akiacha “yote yakiwa yameamriwa kimbele.” Hata hivyo, Augustine alibisha kwa bidii ya moyo kwamba ijapokuwa kwamba Mungu ajua kimbele yote yanayotendeka, bado wanadamu wana hiari ya kujichagulia mambo.—The City of God, Kitabu cha 5, Sura za 7-9.

Karne kadhaa baadaye, mwanatheolojia Mprotestanti John Calvin alikuza zaidi wazo hilo, akibisha kwamba ingawa watu fulani “wameamriwa kimbele [na Mungu] kuwa watoto na warithi wa ufalme wa kimbingu,” wengine wameamriwa kimbele kuwa “wapokeaji wa ghadhabu yake”!

Leo, itikadi katika ajali inachukuliwa kwa uzito katika sehemu nyingi za ulimwengu. Fikiria jambo lililoonwa na Ousmane, kijana mmoja katika Afrika Magharibi. Alikuwa amekuwa mmoja wa wanafunzi bora zaidi shuleni mwake, lakini alipofanya mitihani yake ya mwisho, alianguka! Hilo lilimaanisha kurudia mwaka mzima wa shule na pia kuaibika mbele ya familia na marafiki wake. Rafiki mmoja alijaribu kumliwaza kwa kusema kwamba hayo yalikuwa mapenzi ya Mungu. Mama ya Ousmane vilevile alilaumu ajali kuwa sababu ya kuanguka kwake mitihani.

Mwanzoni Ousmane alifurahi kukubali majaribio yao ya kumhurumia. Kwa maana, ikiwa kwa kweli kuanguka kwake mitihani kulikuwa mapenzi ya Mungu, yeye asingaliweza kufanya lolote kuzuia hilo. Lakini baba yake aliona mambo kwa njia tofauti. Alimwambia Ousmane kwamba kuanguka mitihani kulikuwa kosa lake mwenyewe—si la Mungu. Ousmane alianguka mitihani kwa sababu tu alikuwa amepuuza masomo yake.

Kwa sababu imani yake katika ajali ilikuwa imedhoofishwa, Ousmane aliamua kujichunguzia mambo. Sasa twakualika kufanya vivyo hivyo kwa kusoma makala inayofuata.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki