Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w97 8/15 uku. 30
  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1997
  • Habari Zinazolingana
  • Kuja kwa Yesu au Kuwapo kwa Yesu—ni Kupi?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1996
  • Jina la Mungu Katika Maandiko ya Kikristo
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1984
  • Yehova
    Kutoa Sababu kwa Kutumia Maandiko
  • Jina la Mungu na “Agano Jipya”
    Jina la Mungu Litakaloendelea Milele
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1997
w97 8/15 uku. 30

Maswali Kutoka kwa Wasomaji

Je, Tetragramatoni (zile herufi nne za jina la Mungu kwa Kiebrania) ipatikanayo katika maandishi ya Kiebrania ya Mathayo ilinakiliwa na tabibu Myahudi Shem-Tob ben Isaac Ibn Shaprut wa karne ya 14?

La hasha. Hata hivyo, maandishi haya ya Mathayo hutumia hash·Shem’ (yakiwa yameandikwa kirefu au kifupi) mara 19, kama ilivyoonyeshwa katika ukurasa wa 13 wa Mnara wa Mlinzi wa Agosti 15, 1996.

Neno la Kiebrania hash·Shem’ humaanisha “lile Jina,” ambalo bila shaka hurejezea jina la Mungu. Mathalani, katika maandishi ya Shem-Tob, ufupizo wa hash·Shem’ waonekana katika Mathayo 3:3, kifungu ambacho katika hicho Mathayo alinukuu Isaya 40:3. Ni jambo la akili kukubali kwamba Mathayo aliponukuu mstari kutoka Maandiko ya Kiebrania ambamo Tetragramatoni ilipatikana, alitia ndani jina la Mungu katika Gospeli yake. Hivyo ingawa maandishi ya Kiebrania ambayo Shem-Tob alitumia hayatumii Tetragramatoni, matumizi yake ya “Lile Jina,” kama katika Mathayo 3:3, huunga mkono matumizi ya “Yehova” katika Maandiko ya Kigiriki ya Kikristo.

Shem-Tob alinakili maandishi ya Kiebrania ya Mathayo katika kitabu chake chenye ubishi ʼEʹven boʹchan. Hata hivyo, chanzo cha maandishi yake ya Kiebrania kilikuwa nini? Profesa George Howard, ambaye amechunguza jambo hili sana, adokeza kwamba “maandishi ya Shem-Tob ya Mathayo katika Kiebrania yalikuwa ya wakati fulani kati ya karne nne za kwanza za kipindi cha Ukristo.”a Wengine waweza kukosa kukubaliana naye juu ya jambo hili.

Howard asema: “Mathayo katika Kiebrania iliyowekwa katika maandishi haya ya Shem-Tob yajulikana hasa kwa tofauti zake nyingi ilinganishwapo na maandiko yaliyokubaliwa rasmi ya Mathayo katika Kigiriki.” Mathalani, kulingana na maandishi ya Shem-Tob, Yesu alisema hivi kumhusu Yohana: “Kwa kweli, nawaambia, miongoni mwa wale waliozaliwa na wanawake hakujainuka mkubwa zaidi kuliko Yohana Mbatizaji.” Maandishi hayo huondoa maneno yafuatayo ya Yesu: “Lakini mtu ambaye ni mdogo zaidi katika ufalme wa mbingu ni mkubwa zaidi kuliko yeye.” (Mathayo 11:11) Katika njia zinazofanana na hiyo, kuna tofauti nyingi kati ya maandishi ya sasa ya Kiebrania ya Maandiko ya Kiebrania na maneno ya maandishi kama hayo ya fasiri ya Septuagint ya Kigiriki. Ingawa twatambua tofauti zake, maandishi kama haya ya kale bado yanafaa katika uchunguzi wa ulinganifu.

Kama ilivyotajwa, maandishi ya Shem-Tob ya Mathayo yatia ndani “lile Jina” ambapo kwa kweli kuna sababu nzuri kuamini kwamba Mathayo alitumia Tetragramatoni. Hivyo, tangu 1950, maandishi ya Shem-Tob yamekuwa yakitumiwa kuunga mkono kutumia jina la Mungu katika Maandiko ya Kigiriki ya Kikristo, na bado yanatajwa katika The New World Translation of the Holy Scriptures—With References.b

[Maelezo ya Chini]

a Iliyochapishwa mwaka wa 1984 na Watchtower Bible and Tract Society of New York, Inc.

b Ona pia New Testament Studies, Buku la 43, Nambari ya 1, Januari 1997, ukurasa wa 58-71.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki