Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w98 3/1 kur. 3-4
  • Makanisa Yaungama

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Makanisa Yaungama
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1998
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Papa Aombapo Msamaha
  • Kwa Nini?
  • Kwa Nini Yanaomba Msamaha?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1998
  • Kanisa Katoliki na Yale Maangamizi Makubwa
    Amkeni!—1998
  • Dini Yajiunga
    Amkeni!—1994
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1998
w98 3/1 kur. 3-4

Makanisa Yaungama

“Papa Aliweka Kanisa Kesini.” “Baraza la Kuhukumu Wazushi na Uhasama Kuelekea Watu wa Kiyahudi—Kanisa Latayarisha Ungamo Lake.” “Ungamo Juu ya Yale Maangamizi Makubwa.” “Wamethodisti Wawaomba Radhi Wahindi wa Magharibi ya Mbali.”

JE, UMEPATA kusoma vichwa vya habari kama hivyo? Yaonekana kwamba kwa ukawaida wenye kuongezeka, makanisa yanakubali lawama na yanaomba radhi kwa sababu ya yale ambayo yamefanya kwa karne kadhaa. Vyombo vya habari vinakazia daima maungamo mapya ya papa.

Papa Aombapo Msamaha

Kati ya mwaka wa 1980 na 1996, John Paul wa Pili ‘alitambua makosa ya kihistoria ya Kanisa au akaomba msamaha’ angalau mara 94, asema mwelezaji wa Vatikani Luigi Accattoli katika kitabu chake Quando il papa chiede perdono (Papa Aombapo Msamaha). Kulingana na Accattoli, “katika Kanisa Katoliki, ni papa tu awezaye kufanya ungamo.” Naye amefanya hilo, akirejezea matukio yenye kubishaniwa zaidi katika historia ya Katoliki—zile Krusedi, vita, kutegemeza udikteta mbalimbali, migawanyiko katika kanisa, uhasama kuelekea watu wa Kiyahudi, yale Mabaraza ya Kuhukumu Wazushi, Mafia, na ubaguzi wa kijamii. Katika taarifa iliyopelekewa makadinali mwaka wa 1994 (ambayo yaonwa na wengine kuwa hati ya maana zaidi ya ofisi ya papa), John Paul wa Pili alipendekeza “ungamo la dhambi la ujumla na la milenia.”

Maaskofu kadhaa wamefuata kielelezo cha papa. Desemba 1994 gazeti la habari la Italia Il Giornale liliripoti hivi: “Maaskofu wengi Wamarekani walionekana katika televisheni nao waliomba msamaha hadharani.” Kwa sababu gani? Kwa sababu ya kudharau tatizo la makasisi wenye kuvutiwa na watoto kingono, kufanya hivyo kukileta madhara kwa wahasiriwa wengi wachanga. Januari 1995 gazeti la habari La Repubblica liliripoti juu ya “tendo lisilo na kifani katika historia ya Ukatoliki wa sasa”—tatizo la kutosema lolote kwa Papa Pius wa 12 kuhusiana na yale Maangamizi Makubwa lilizungumziwa. Januari 1995 gazeti la habari hilohilo liliripoti kwamba jamii ya maaskofu ya Ujerumani iliomba msamaha kwa sababu ya “makosa mengi” ya washiriki wa Katoliki ya Kiroma waliounga mkono uhalifu mbalimbali wa Nazi. Makanisa kadha wa kadha ya Kiprotestanti pia yamejichambua.

Kwa Nini?

Biblia hutia moyo kuomba msamaha tukoseapo, na wengi huyapongeza makanisa yajichambuapo. (Yakobo 5:16) Lakini kwa nini makanisa yanafanya hivyo? Kufanya hivyo kwapaswa kuathirije jinsi tunavyoyaona?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki