Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w05 10/15 uku. 3
  • Ni Elimu Gani Inayoweza Kufanikisha Maisha Yako?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ni Elimu Gani Inayoweza Kufanikisha Maisha Yako?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2005
  • Habari Zinazolingana
  • Elimu—Itumie Kumsifu Yehova
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1996
  • Mashahidi wa Yehova Wana Maoni Gani Kuhusu Elimu?
    Maswali Yanayoulizwa Mara Nyingi Kuhusu Mashahidi wa Yehova
  • Elimu—Gharama Yake? Faida Yake
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1982
  • Je, Biblia Inapinga Elimu?
    Amkeni!—1998
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2005
w05 10/15 uku. 3

Ni Elimu Gani Inayoweza Kufanikisha Maisha Yako?

JE, UMEWAHI kulemewa na matatizo sana hivi kwamba ukahisi ni kana kwamba unazama ndani ya maji yanayoenda kasi? Hebu wazia jinsi unavyoweza kuteseka usiposhughulikia vizuri tatizo moja au zaidi kati ya hayo! Hakuna mtu anayezaliwa akiwa na uwezo wa kutatua matatizo yote kwa mafanikio wala kufanya maamuzi mazuri wakati wote. Hiyo ndiyo sababu elimu ni muhimu. Unaweza kupata wapi elimu inayoweza kukusaidia kukabiliana na matatizo ya maisha?

Watu wengi, vijana kwa wazee huiona elimu ya shule kuwa muhimu. Wataalamu fulani hata husema kuwa “wanaamini kabisa kwamba huwezi kamwe kupata kazi [nzuri] ikiwa huna digrii.” Hata hivyo, mafanikio ya kimwili hayawezi kutimiza mahitaji mengine ya wanadamu. Kwa mfano, je, elimu ya juu inaweza kukusaidia kuwa mzazi, mwenzi, au rafiki bora? Wakati mwingine, watu wanaoheshimiwa kwa sababu ya mafanikio yao katika elimu huenda wakawa na sifa mbaya, wakakosa kufanikiwa katika maisha ya familia, au hata wanaweza kujiua.

Baadhi ya watu hutegemea dini iwaongoze ikiwa chanzo cha elimu, lakini wanakatishwa tamaa kwa sababu hawapati msaada unaofaa wa kukabiliana na matatizo ya maisha. Kwa mfano, Emiliaa kutoka Mexico anasema: “Miaka 15 iliyopita nilihisi kuwa mimi na mume wangu hatungeweza kuendelea kuishi pamoja. Tuligombana kila mara. Sikuweza kumsaidia aache kulewa. Mara nyingi nililazimika kuwaacha watoto wetu wachanga wakiwa peke yao ili nikamtafute mume wangu. Nililemewa sana kihisia. Mara kadhaa nilienda kanisani ili kutafuta suluhisho la matatizo yangu. Ingawa Biblia ilitumiwa mara kwa mara, sikuwahi kupata shauri lililonifaa; wala hakuna mtu aliyeniambia la kufanya. Kuketi kanisani kwa muda na kukariri sala fulani hakukuniridhisha.” Huenda wengine wakakatishwa tamaa wanapoona kwamba viongozi wao wa kidini hawawawekei mfano mzuri. Hivyo, wengi huacha kutumaini dini kuwa chanzo cha mafunzo au elimu wanayohitaji ili kufanikiwa maishani.

Basi, huenda ukajiuliza, ‘Ninapaswa kupata elimu ya aina gani ili nifanikiwe maishani?’ Je, Ukristo wa kweli unajibu swali hilo muhimu? Hilo litazungumziwa katika makala inayofuata.

[Maelezo ya Chini]

a Jina limebadilishwa.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki