Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w11 1/1 kur. 30-31
  • Thamini Mambo Matakatifu!

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Thamini Mambo Matakatifu!
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2011
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • CHIMBA ZAIDI.
  • Uharibifu wa Sodoma na Gomora
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2008
  • Yesu Anawaponya Watu Kimuujiza
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2008
  • Yesu Awashangaza Wasikilizaji Wake
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2008
  • Musa Apokea Mgawo wa Pekee
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2012
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2011
w11 1/1 kur. 30-31

Kwa Ajili ya Vijana

Thamini Mambo Matakatifu!

Maagizo: Fanya zoezi hili katika mazingira matulivu. Unaposoma maandiko, jiwazie ukiwa katika matukio yanayozungumziwa. Wazia kikao. Sikia sauti. Hisi kama wahusika wakuu wanavyohisi. Wazia kwamba masimulizi haya ni halisi kabisa.

Wahusika wakuu: Isaka, Rebeka, Yakobo, na Esau

Muhtasari: Esau anamuuzia Yakobo, ndugu yake pacha, haki yake ya kuzaliwa.

➊ CHUNGUZA TUKIO HILI.—SOMA MWANZO 25:20-34.

Esau na Yakobo wanaonyesha sifa gani hata wakiwa bado ndani ya tumbo la uzazi?

․․․․․

Unafikiri Esau na Yakobo walionekana jinsi gani wakiwa vijana?

․․․․․

Unatambua hisia gani katika mazungumzo kati ya Yakobo na Esau kwenye mstari wa 30 mpaka 33?

․․․․․

CHIMBA ZAIDI.

Ukitumia vifaa vya kufanyia utafiti unavyoweza kupata, chunguza kuhusu haki za mtoto wa kwanza wa kiume. Kwa nini haki hizo zilikuwa za maana? Kuuza haki hizo kwa ajili ya bakuli ya mchuzi kulimaanisha nini?

․․․․․

2 ➋ CHUNGUZA TUKIO HILI.—SOMA MWANZO 27:1-10, 30-38.

Unatambua hisia gani katika sauti ya Esau anapogundua kwamba ndugu yake amepokea baraka za mzaliwa wa kwanza? _______

․․․․․

CHIMBA ZAIDI.

Je, ilikuwa ni vibaya kwa Rebeka na Yakobo kupanga njama ili Yakobo apate baraka? Kwa nini unajibu hivyo? (Dokezo: Ona Mwanzo 25:23, 33.)

․․․․․

3 ➌ TUMIA MAMBO ULIYOJIFUNZA. ANDIKA MAMBO ULIYOJIFUNZA KUHUSU . . .

Matokeo mabaya na ya kudumu ya kutosheleza tamaa papo hapo.

․․․․․

NJIA NYINGINE UNAYOWEZA KUTUMIA HABARI HIYO.

Umekabidhiwa mambo gani matakatifu?

․․․․․

Unaweza kuonyesha kwa njia gani hususa kwamba unathamini mambo matakatifu?

․․․․․

4 ➍ NI MAMBO GANI KATIKA SIMULIZI HILI AMBAYO YAMEKUGUSA MOYO SANA, NA KWA NINI?

․․․․․

Ikiwa huna Biblia, waombe Mashahidi wa Yehova wakupe moja, au soma habari zaidi katika intaneti www.watchtower.org

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki