Habari za kitheokrasi
British Virgin Islands: Kilele kipya cha wahubiri 136 katika Mei walioongoza mafunzo ya Biblia 206, ambayo yalikuwa pia kilele kipya.
Korea: Katika Mei wahubiri 65,260 waliripoti, kikiwa ni kilele chao cha 84 kwa muda wa miezi 89 iliyopita.
Papua New Guinea: Kilele kingine katika wahubiri kilifikiwa katika Mei, 2,547 wakiripoti.
Réunion: Ripoti ya Mei ilionyesha ongezeko la asilimia 11 na kilele kipya cha wahubiri 1,926.
St. Lucia: Kilele kipya cha wahubiri 475 waliripoti katika Mei, ongezeko la asilimia 8. Mafunzo ya Biblia yalipanda kwa asilimia 22 kutoka Mei uliopita jumla ikawa 617.
U.S. Virgin Islands: Ongezeko la asilimia 19 katika Mei lilileta kilele kipya cha wahubiri 560.