Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • km 8/95 uku. 1
  • Mwenendo wa Kikristo Shuleni

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mwenendo wa Kikristo Shuleni
  • Huduma Yetu ya Ufalme—1995
  • Habari Zinazolingana
  • Endelea Kuwa Mwenye Nguvu Kiroho, Baki Ukiwa Safi kwa Ajili ya Utumishi wa Yehova
    Huduma Yetu ya Ufalme—1992
  • Vijana Wakristo Iweni Imara Katika Imani
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1991
  • Imani Yako Itakuwa na Nguvu Kadiri Gani?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2021
  • Je, Kweli Una Imani Katika Habari Njema?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2003
Pata Habari Zaidi
Huduma Yetu ya Ufalme—1995
km 8/95 uku. 1

Mwenendo wa Kikristo Shuleni

1 Ikiwa wewe ni kijana Mkristo aliye shuleni bado, wahitaji imani yenye nguvu ili ushikilie uaminifu-maadili. Uko katika mashirika mabaya na hali zinazoweza kujaribu imani yako. Ni jambo la maana utumie shauri la Petro la ‘kuwa na mwenendo mzuri kati ya Mataifa, ili . . . wayatazamapo matendo yako mazuri, wamtukuze Mungu.’ (1 Pet. 2:12) Wahitaji moyo mkuu na azimio ili kushinda ugumu huu.

2 Ukiwa ndani au nje ya shule, unakabiliwa na mavutano yenye kuchafua ya ngono kabla ya ndoa, lugha chafu, tumbaku, na matumizi mabaya ya dawa za kulevya. Kila siku, unakabili majaribu yanayotisha kuharibu rekodi yako ya mwenendo mzuri. Kama ilivyo na watu wazima, ni lazima ‘uishindanie imani’ ikiwa utavumilia majaribu hayo.—Yuda 3; ona Mnara wa Mlinzi, Julai 15, 1991, kurasa 23-26.

3 Shuleni, kuna sherehe na sikukuu za kilimwengu. Je, wajua ni sikukuu zipi za kitaifa na za kidini zinazochochewa katika shule yako? Jambo lenye ugumu likitokea, ungeweza ‘kuwa na dhamiri njema, ili . . . watahayarishwe wale wautukanao mwenendo wako mwema katika Kristo’?—1 Pet. 3:16.

4 Huenda ukajaribiwa na uvutio wa utendaji wa michezo ya shule au vikusanyiko vya baada ya masomo. Ni lazima uwe chonjo kutambua jinsi utendaji huu wenye kuonekana wa kufurahisha uwezavyo kuridhia imani yako. Kuna uhitaji wa kuchagua mashirika unayoweza kufurahia pamoja nayo ‘badilishano la kitia-moyo,’ kila mmoja akijengwa kwa imani ya mwenzake.—Rum. 1:12, NW.

5 Unaweza Kuvumilia, kwa Msaada wa Yehova: Shetani hujaribu imani yako daima. Majaribu uwezayo kuvumilia yaweza kuwa makali zaidi, lakini thawabu huyafanya yastahili. (1 Pet. 1:6, 7) Huwezi kuvumilia wewe mwenyewe kwa mafanikio; lazima umwendee Yehova upate msaada. Yesu aliwasihi wanafunzi wake: “Kesheni, mwombe, msije mkaingia majaribuni.” (Mt. 26:41) Nidhamu na kujidhibiti ni muhimu.—1 Kor. 9:27.

6 Sikuzote kumbuka kwamba una daraka kuelekea Yehova kwa mwenendo wako. (Mhu. 11:9) Hata ingawa unayofanya hayaonwi na wengine, Yehova anajua ufanyayo naye atatoa hukumu. (Ebr. 4:13) Tamaa ya moyo mweupe ya kumpendeza yapasa kukusukuma ‘utimize wokovu wako kwa kuogopa na kutetemeka.’ (Flp. 2:12) Kusoma Neno la Mungu kila siku ni msaada mkubwa. Limejawa na shauri bora zaidi na vielelezo vizuri vya kuigwa.—Ebr. 12:1-3.

7 Wazazi, mnatimiza sehemu muhimu. Mnahitaji kuangalia watoto wenu mjue matatizo ambayo watoto wenu wanakabili, na kuandaa msaada unapohitajiwa. Je, mna uhusiano mzuri na watoto wenu? Je, mmeingiza ndani yao uelewevu wenye uthamini kwa sheria na kanuni za Mungu? Watoto wenu wanapokabiliwa na mikazo au majaribu, je, huwa wenye nguvu, au hukata tamaa kwa urahisi? Wao huvunjika moyo kwa sababu inawapasa kuwa tofauti na marika wao? Mkiwa wazazi, mna daraka la kuwasaidia. (Kum. 6:6, 7) Mkifanya kazi yenu vema, mnaweza kuwasaidia wawe washindi katika vita vya imani.—Mit. 22:6.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki