Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • km 12/97 uku. 7
  • Pata Manufaa Zote za Shule

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Pata Manufaa Zote za Shule
  • Huduma Yetu ya Ufalme—1997
  • Habari Zinazolingana
  • Sababu Gani Ujifunze Shuleni?
    Kupata Faida Zote za Ujana Wako
  • Elimu Yenye Kusudi
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1992
  • Elimu ya Kilimwengu na Miradi Yako ya Kiroho
    Huduma Yetu ya Ufalme—1999
  • Je, Niache Shule?
    Amkeni!—2010
Pata Habari Zaidi
Huduma Yetu ya Ufalme—1997
km 12/97 uku. 7

Pata Manufaa Zote za Shule

1 Huu ndio wakati wa mwaka ambao vijana wengi huuliza: “Je, ni lazima nirudi shuleni?” Ijapokuwa huenda kukawa na magumu na mahangaiko yanayohusiana na kurudi shuleni, pia kuna manufaa nyingi zinazoweza kupatikana na vijana ambao wanajitumikisha wenyewe ili wapate manufaa bora zaidi kutokana na elimu yao.

2 Elimu nzuri ya msingi yaweza kuchangia maendeleo ya mtu ya kiroho. Lile afanyalo mtu wakati wa ujana wake lina matokeo makubwa juu ya yale awezayo kutimiza akiwa mtu mzima. Hata kwa habari ya kusoma shuleni, “lolote lile mtu analopanda, hilo atavuna pia.” (Gal. 6:7) Vijana wanaojifunza masomo yao kwa bidii nyendelevu wanaweza kujipatia stadi ambazo zitawafanya wawe watu wenye mafaa kwa Yehova.

3 Ufikirio wa kimbele watakwa ikiwa mtu atafanya machaguo yafaayo ya masomo ya shule. Yawapasa wazazi wasaidie watoto wao wachague yale ambayo yatawapa mazoezi yatumikayo zaidi ili wafikie miradi yao ya kiroho maishani. Kwa kusitawisha stadi zao, vijana watakuwa na manufaa za kuweza kujitegemeza wenyewe katika kazi ya painia. Elimu yao ya msingi yapaswa kuwasaidia wamsifu Yehova haidhuru popote wanapotumika.

4 Vijana, jaribuni kupata manufaa zote za miaka yenu ya shule. Kwa kufanya hivyo, kazieni fikira kuishi maisha yenye maana katika utumishi mtakatifu, badala ya kufuatia kazi-maisha ya kilimwengu. Jitahidini kutumia maisha yenu mkifanya mapenzi ya Yehova. Kwa njia hiyo, mtafanikisha njia yenu, kwa sifa ya Yehova.—Zab. 1:3.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki