Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • km 11/97 uku. 3
  • Habari Njema Katika Internet

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Habari Njema Katika Internet
  • Huduma Yetu ya Ufalme—1997
  • Habari Zinazolingana
  • Huduma na Vyanzo vya Habari vya Internet
    Amkeni!—1997
  • Matumizi ya Internet—Uwe Chonjo Kuhusu Hatari Zake!
    Huduma Yetu ya Ufalme—1999
  • Intaneti Kutumia kwa Hekima Kifaa cha Ulimwenguni Pote
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2011
  • Habari Inayowasaidia Watu
    Huduma Yetu ya Ufalme—2004
Pata Habari Zaidi
Huduma Yetu ya Ufalme—1997
km 11/97 uku. 3

Habari Njema Katika Internet

Katika kizazi chetu cha kitekinolojia, watu fulani hupata habari kutokana na vyanzo vya elektroni, kutia na Internet. Kwa hiyo Sosaiti imeweka habari kadhaa iliyo sahihi katika Internet juu ya itikadi na utendaji mbalimbali wa Mashahidi wa Yehova.

Mahali petu pa Web ya Internet pana anwani http://www.watchtower.org na pana trakti mbalimbali, broshua, na makala za Mnara wa Mlinzi na Amkeni! katika Kiingereza, Kichina (Sahili), Kijerumani, Kirusi, na Kihispania, na vilevile katika lugha nyingine. Vichapo vilivyopo mahali hapa pa Web tayari vinapatikana kupitia makutaniko navyo vyatumika katika huduma. Kusudi la mahali petu pa Web, si kutoa vichapo vipya, bali ni kufanya habari ipatikane kwa watu wote katika mfumo wa elektroni. Hakuna haja kwa mtu yeyote kutayarisha habari za Internet juu ya Mashahidi wa Yehova, utendaji wetu, au itikadi zetu. Mahali petu rasmi hutoa habari sahihi kwa yeyote mwenye kuitaka.

Ingawa mahali petu hapana uandalizi wa ujumbe mbalimbali wa elektroni (E-mail), panaorodhesha anwani za ofisi za tawi tufeni pote. Hivyo, watu wanaweza kuandika ili wapate habari zaidi au ili wapate usaidizi wa kibinafsi kutoka kwa Mashahidi wa mahali pao. Jihisi huru kushiriki anwani ya Internet iliyo juu na yeyote ambaye huenda akawa na mwelekeo wa kuanza kujifunza kweli ya Biblia kutokana na mfumo huu.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki