Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • km 4/99 uku. 1
  • Kuzidi Kutoa Ushahidi Mwisho Ukaribiapo

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuzidi Kutoa Ushahidi Mwisho Ukaribiapo
  • Huduma Yetu ya Ufalme—1999
  • Habari Zinazolingana
  • Dumisha Hisi Yako ya Uharaka
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2012
  • Linda Hisi Yako ya Uharaka
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1995
  • Jinsi ya Kusitawisha Hisi ya Uharaka Katika Kazi ya Kuhubiri
    Huduma Yetu ya Ufalme—2014
  • “Lihubiri Neno . . . kwa Hima”
    Huduma Yetu ya Ufalme—2000
Pata Habari Zaidi
Huduma Yetu ya Ufalme—1999
km 4/99 uku. 1

Kuzidi Kutoa Ushahidi Mwisho Ukaribiapo

1 Majira ya mavuno huwa wakati wenye shangwe. Pia huwa wakati wa kazi ngumu. Kuna wakati mchache tu wa kukusanya mazao. Wafanyakazi huwa hawachezichezi katika kazi yao.

2 Akisema kitamathali, Yesu alilinganisha “umalizio wa mfumo wa mambo” na wakati wa mavuno. (Mt. 13:39) Tunaishi katika umalizio wa huu mfumo wa mambo, tukibaki na wakati mchache wa kutoa ushahidi “katika dunia yote inayokaliwa.” (Mt. 24:14) Mwisho ukaribiapo zaidi, twahitaji kuzidisha ushiriki wetu katika huduma. Kwa nini? Yesu alieleza: “Mavuno ni mengi, lakini wafanyakazi ni wachache.”—Mt. 9:37, 38; Rom. 12:11.

3 Ifanye kwa Hima: Yesu alipoanza kazi yake kuu ya kuhubiri, alikuwa na muda wa miaka mitatu na nusu tu ili kutimiza kile alichokuwa amegawiwa kufanya. Alihubiri akiwa na hisi ya uharaka, akisema: “Lazima nitangaze habari njema ya ufalme wa Mungu, kwa sababu kwa ajili ya hili nilitumwa.”—Luka 4:43.

4 Yesu alifanya wanafunzi wake waone uharaka kama huo. (Mr. 13:32-37) Ndiyo sababu “kila siku katika hekalu na kutoka nyumba hadi nyumba wa[li]endelea bila kuacha kufundisha na kutangaza habari njema juu ya Kristo, Yesu.” (Mdo. 5:42) Shughuli zisizo na maana sana hazikutangulizwa maishani mwao. Ingawa walikuwa wachache, walifaulu kuhubiri habari njema “katika viumbe vyote chini ya mbingu.”—Kol. 1:23.

5 Kuna sababu kubwa zaidi kwetu kusitawisha hisi ya uharaka kama hiyo sasa, kwa kuwa “mwisho wa mambo yote umekaribia.” (1 Pet. 4:7) Yehova ameweka siku na saa ya mwisho wa huu mfumo wa mambo. (Mt. 24:36) Kazi ya kuhubiri itakamilishwa katika wakati uliobaki. Ndiyo sababu tunazidisha jitihada zetu za kufikia watu wengi zaidi tukiwa na habari njema.

6 Kwa kuzidi kutoa ushahidi mwisho ukaribiapo, tutaridhika kumwambia Yehova, kama Yesu alivyomwambia: ‘Tumemaliza kazi ambayo umetupa kufanya.’—Yn. 17:4.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki