Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • km 5/01 uku. 1
  • Shiriki Kabisa Katika Mavuno

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Shiriki Kabisa Katika Mavuno
  • Huduma Yetu ya Ufalme—2001
  • Habari Zinazolingana
  • Mashamba Ni Meupe kwa Ajili ya Kuvunwa
    Huduma Yetu ya Ufalme—2010
  • Iweni Wavunaji Wenye Furaha!
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2001
  • Endeleeni Katika Kazi ya Kuvuna!
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2001
  • Wanahitajiwa kwa Haraka—Wafanya Kazi Zaidi wa Mavuno!
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1985
Pata Habari Zaidi
Huduma Yetu ya Ufalme—2001
km 5/01 uku. 1

Shiriki Kabisa Katika Mavuno

1 Manabii wa kale wa Yehova, na vilevile Yesu Kristo mwenyewe waliongea juu ya kazi ya kukusanya watu. (Isa. 56:8; Eze. 34:11; Yn. 10:16) Kazi hiyo yatimizwa sasa habari njema ya Ufalme inapohubiriwa ulimwenguni pote. (Mt. 24:14) Tofauti kati ya wale wanaomtumikia Mungu na wale wasiomtumikia ni dhahiri sana. (Mal. 3:18) Hilo lamaanisha nini kwetu?

2 Wajibu wa Kibinafsi: Twaweza kujifunza kutokana na kielelezo cha Paulo, ambaye alikuwa katika mstari wa mbele kushiriki kikamili katika huduma ya Kikristo. Alijiona kuwa mwenye wajibu wa kuhubiri ili watu wote wapate fursa ya kusikia habari njema na waokolewe. Hilo lilimfanya ajikakamue kwa bidii kwa manufaa yao. (Rom. 1:14-17) Kwa sababu ya hali hatari inayokabili wanadamu leo, je, sisi hatuna wajibu mkubwa hata zaidi wa kusaidia wale walio katika eneo letu?—1 Kor. 9:16.

3 Wakati wa Kutenda kwa Uharaka: Kazi ya kuhubiri yaweza kulinganishwa na kazi ya kutafuta na kuokoa watu walio hatarini. Lazima watu watafutwe na kusaidiwa wapate usalama kabla haijawa kuchelewa mno. Muda unaobaki ni mfupi. Maisha yamo hatarini! Si ajabu Yesu aliwasihi wanafunzi wake ‘wamwombe Bwana-mkubwa wa mavuno atume wafanyakazi katika mavuno yake.’—Mt. 9:38.

4 Wahubiri wengi wa Ufalme wakitambua uharaka huo leo, wameongeza jitihada yao ya kushiriki katika kazi hii ya kuokoa watu. Tineja mmoja anayeitwa Hirohisa pamoja na ndugu na dada wanne wachanga zaidi walikuwa na mzazi mmoja. Alitegemeza familia yao kifedha kwa kuamka saa tisa za usiku ili kupelekea watu magazeti. Hata hivyo, Hirohisa alitaka kufanya mengi katika huduma, kwa hiyo akawa painia wa kawaida. Je, kuna njia ambayo unaweza kushiriki kikamili katika kazi ya kuhubiri ambayo haitarudiwa tena kamwe?

5 “Wakati ubakio umepunguzwa.” (1 Kor. 7:29) Kwa hiyo, na tufanye yote tuwezayo katika kazi hii ya maana zaidi inayofanywa duniani leo—kuhubiri habari njema za Ufalme na kufanya wanafunzi. Yesu alilinganisha huduma hii na kazi ya mavuno. (Mt. 9:35-38) Kwa kushiriki kabisa katika kazi ya mavuno, matunda ya kazi yetu huenda yakatia ndani kusaidia mtu fulani awe sehemu ya umati mkubwa wa waabudu unaofafanuliwa kwenye Ufunuo 7:9, 10.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki